Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Kilimo Hai Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo (TOAM) linaratarajia kufanya Mkutano MKuu wa Nne Machi 3hadi Machi 5 ,2026 jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na wadau kuhusiana na kilmo hai nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bakari Mongo amesema mkutano huo ulitakiwa kufanyika Januari mwaka huu lakini waliahirisha kutokana sababu mbalimbali na kuahidi malengo waliotaka yatafikiwa katika mkutano huo wa mwezi machi.

Amesema wadau wajitokeze katika kufanikisha mkutano huo kwa kutoa udhamini katika kukidhi matarajio ya kilamo hai nchini.

Mongo amesema Mkutano Mkuu huo unatarajia kuwa wadau 400 wakiwemo wakulima ,Watunga Sera,Watafiti ,Wasomi,Sekta Binafsi ,Vyama vya Kiraia pamoja na Wabia wa Maendeleo.

Mongo amesema kuwa mkutano huo ni fursa ya kubadilisha maarifa na uzoefu ili kuboresha mifumo endelevu ya uzalishaji wa chakula cha kutosha ,kulinda mazingira na kuongeza mazao kwa wakulima nchini.

Aidha amesema katika mkutano huo wataangalia maudhui ya Usalama wa Chakula na Lishe Mbinu na Teknolojia za Kilimo Ikolojia Hai na Ustamilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi ,Manufaa ya Kiuchumi ya Kilimo Ikolojia Hai kwa Wakulima ,Maendeleo ya Kiteknolojia na Mfumo ya Uzalishaji wa Chakula pamoja na Mazingiea ya Kisera na Mifumo katika kuendeleza Kilimo Ikolojia Hai.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...