NA MWANDISHI WETU.
BENKI ya NMB imedhihirisha kiwango cha juu cha ubunifu, baada ya kuwa ya kwanza nchini kuzindua Teknolojia Mpya, ya Kisasa na Salama Zaidi ya Mfumo wa Malipo iitwayo NMB TAP ‘Wearables,’ inayomuwezesha mteja kufanya malipo kupitia Pete, Bangili na Stika maalum.
Uzinduzi wa NMB TAP ‘Wearables,’ umefanyika jijini Dar es Salaam Alhamisi Januari 22, ukihudhuriwaa na Meneja Biashara wa MasterCard Tanzania, Moses Alphonce, ambaye aliipongeza NMB kwa bunifu zinazoiwekla taasisi hiyo mbele ya muda katika kuleta suluhishi za kifedha kwa wateja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano wa NMB, Innocent Yonazi, aliitaja NMB TAP kuwa ni ‘future of banking in Tanzania,’ inayokwenda kuiongezea nguvu mifumo yote ya malipo iliyoanzia katika pesa taslimu.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukifanya malipo kwa kadi na pesa taslimu, hiyo ndio ‘reality’ ya kibenki barani Afrika, hususani Tanzania. Sisi NMB lengo la kwenda na wateja wetu kwenye suluhisho zinazo kwenda na kasi ya maisha ya sasa (kidijitali) na sahihi zaidi za kibenki, tukaja na bunifu hii ya kwanza nchini.
“Mteja anahitaji kufanya malipo ya kibenki kwa haraka, unafuu, urahisi na usalama, vitu ambavyo vimo katika NMB TAP. Wanaume wengi walizoea kutembea na ‘wallet’ na wanawake wao mapochi na ‘hand bag’ za pesa, wateja wamekuwa watumwa wa mabenki, badala ya mabenki kuja na suluhisho za changamoto za kifedha.
“NMB kwa kushirikina na MasterCard tukaona haja ya kubadili hali hiyo, na kufanya mapinduzi makubwa juu ya mustakabali wa mifumo ya malipo nchini na kupitia NMB TAP, tunakwenda kumpa mteja huduma ambayo haijawahi kuwepo nchini Tanzania,” alisisitiza Yonazi.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Master Card Kanda ya Afrika Mashariki, Shehryar Ali, aliipongeza NMB kwa bunifu zinazokidhi utatuzi wa changamoto za kibenki kwa wateja na kwamba wanajivunia ushirikiano baina ya benki hiyo na taasisi yao iliyobobea katika mifumo ya malipo ya kiteknolojia.
“Kila mwaka NMB wamekuwa vinara wa bunifu mpya za huduma zinaokuja kuigwa baadaye na taasisi nyingine za fedha nchini Tanzania. Pongezi kwa ‘team’ yote iliyochakata wazo lililozaa huduma hii ya NMB TAP, ambayo ni ya kwanza na ya kihistoria nchini.
“NMB TAP ni huduma bora, ya kisasa, salama zaidi na ya kipekee, hasa katika nchi ambayo wengi wamezoea matumizi ya kadi katika malipo, ambako NMB inakuja na njia zaidi ya tano tofauti za malipo, ingawa tutaanza na tatu kati ya hizo na vingine zitafuata hatua kwa hatua.
“Tuendako, utakuwa n uwezo wa kufanya malipo kupitia simu yako, saa ya mkononi, kwa kutumia bangili yako, kwa kutumia cover ya simu yako,” alisema Moses katika maelezo yake.
Aliwatoa shaka wenye maswali kuhusu mifumo ya kiusalama ya huduma hiyo mpya, ambayo haitotumia ‘password,’ akisema huduma imeziba na kuondoa kabisa mianya ya uhalifu, kudukuliwa na upotevu wa pesa za wateja.
“Tunahakikisha usalama wa mteja kupitia mfumo huu, kwani hakuna wizi wa ‘account details’ inayoweza kudukuliwa na kuiba pesa za mteja,” alibainisha Moses katika uzinduzi huo.
Naye Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alieleza hatua mbalimbali za mapinduzi ya kimfumo hususani katika teknolijia ya malipo na kwamba wanajivunia ushirikiano wao na MasterCard International, yanayowapa nguvu ya kufanya bunifu bora, nafuu na salama zaidi.
“NMB TAP ‘Wearables’ ni huduma ya kwanza inayoakisi hatua kubwa ya kimaendeleo na kimapinduzi iliyopigwa na benki yetu tangu kuanza kwake mwaka 1997, wakati ambao hatukuwa na matumizi ya kadi, ila kitabu ‘pass book.’
“Tukapiga hatua kutoka hapo hadi kufikia kuanzisha kadi ya njano mwaka 2006, ambayo ilimuwezesha mteja kupata pesa kupitia ATM za NMB tu. UShirikiano wetu na Mastercard ulianza mwaka 2014, ambao ukaja kutupitisha katika hatua mbalimbali za mabadiliko na mapinduzi ya kimifumo.
“Tulianza ushirikiano wetu na MasterCard kwa matumizi ya kadi ya kutoa pesa kwenye ATM zote, pamoja POS, kuchanja, Lipa Mkononi, QR Code, QR Pay by Link hadi kufikia 2024 na sasa tunapozindua NMB TAP,” alibainisha Mponzih uku akiwataka wateja kutuma maombi ya kutumia huduma mpya haraka.













Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...