Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu kutenda mambo mema ili kutajwa kwa wema ndani ya jamii pale wanapotangulia mbele ya haki.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 16 Januari 2026, alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti wa Bamita Chumbuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Dkt. Mwinyi amesema Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kote, ikiwa ni juhudi za Serikali kuhakikisha inatimiza matarajio makubwa ya wananchi.

Naye Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutafuta elimu zaidi ili kujijengea heshima ndani ya jamii.

Msikiti wa BAMITA uliwekewa jiwe la msingi na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, mwaka 1981.

Alhaj Dkt. Mwinyi anaendelea na utaratibu wake wa kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa kwa kusali katika misikiti mbalimbali mijini na vijijini.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...