Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha TRA kupitia Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa kuimarisha ulinzi mipakani kwa kuweka mifumo na vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.
Akizungumza katika maadimisho ya siku ya Forodha Duniani Januari 26.2026 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam amesema Rais Samia wamewezesha kununuliwa na kufungwa kwa Scanner za kisasa 57 ambazo zimeongeza udhibiti mipakani.
Amesema kupitia Scanner hizo 57 ambazo zimefungwa Bandarini, mipakani na katika viwanja vya ndege wameweza kuzuia bidhaa zisizoruhusiwq kujngia nchini na kudhibiti bidhaa zilizodhibitiwa kuingia nchini pamoja na kuokoa afya za watanzania dhidi ya bidhaa hatarishi.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kutupa miongozo na kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu ya kuihudumia nchi, Tunamshukuru sana na tunamuahidi kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa" amesema Mwenda.
Amesema mbali na kuiwezesha TRA kupitia uwekezaji mkubwa alioufanya katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari nyingine nchini umewezesha kuongezeka kwa mapato ya Forodha kutoka Bilioni 800 na kufikia Trilioni 1.200 na kufanya mchango wa Idara ya Forodha kwa makusanyo ya TRA kuwa asilimia 39 ya makusanyo yote jambo ambalo ni la kujivunia.
Amesema kwa upande wa teknolojia Rais Samia amewekeza kwenye mfumo wa TANCIS ambao umeboresha utendaji kazi wa Forodha na kuongeza ufanisi kwa kuwawezesha walipakodi kupata huduma kupitia mtandao.
Ametoa wito kwa watumishi wote wa TRA kuongeza ufanisi, juhudi na maarifa katika utendaji kazi wao wa kila siku huku akiwapongeza kwa kujituma na kuwezesha kukusanywa kwa kiwango kikubwa cha kodi ambacho hakikuwahi kukusanywa katika miongo iliyopita cha Sh. Trilioni 4.13 kilichorekodiwa mwezi Desemba 2025.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...