Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,ametoa tuzo kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa kampuni na wadau wengine katika juhudi zao za uhifadhi wa mazingira na kuliletea taifa maendeleo endelevu.

Tuzo hiyo ya kihistoria Pongezi ambao ni ya kwanza kwa SBL kutolewa  na kingozi mkuu wa nchi, zinaonesha dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika utekelezaji wa mipango ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG).

Kupitia programu zake mbalimbali, SBL hadi sasa imefanikiwa:

* Kupanda miti zaidi ya 10,000 katika Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati

* Kutekeleza miradi ya maji safi na salama zaidi ya 28 kwa jamii zinazozunguka maeneo yake ya uzalishaji

* Kuwekeza katika kilimo endelevu kwa kuunga mkono vijana zaidi ya 300 kupitia mpango wa Kilimo Viwanda

Aidha, SBL imeanzisha mpango wa Shamba ni Mali, unaolenga kuwapatia wakulima mbolea, mbegu bora, teknolojia ya kisasa na elimu ya kilimo, na lengo la kuwafikia wakulima zaidi ya 4,000 ifikapo mwaka 2030.

Utambuzi huu unaakisi mchango wa SBL kama mdau anayejali mazingira na kuthamini jamii anazozihudumia, sambamba na kuunga mkono ajenda ya Taifa ya maendeleo endelevu


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...