📍Wiki ya Huduma za fedha Kitaifa kuanza viwanja vya Usagara Tanga



Na MASHAKA MHANDO, Tanga

Wizara ya Fedha imetangaza rasmi kuanza kwa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa mkoani Tanga, yenye lengo la kuwajengea wananchi uwezo wa kusimamia uchumi wao na kuongeza uelewa wa masuala ya fedha nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa leo, Kaimu Kamishina wa Idara ya Uendelezaji wa sekta za fedha wa Wizara ya Fedha, Dionesia Mjema msemaji ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatafanyika katika Viwanja vya Usagara kuanzia Januari 19 hadi Januari 26, 2026.

Tukio hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb).

Alisema malengo ya Serikali kwa maadhimisho haya ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (2020/21 – 2029/30).

Alisema serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuhakikisha ifikapo mwaka 2025, asilimia 80 ya Watanzania wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha.

"Utafiti wa FinScope wa mwaka 2023 ulionyesha kuwa ni asilimia 53.5 tu ya nguvu kazi ndiyo inayotumia huduma rasmi za fedha. Tunataka kuwafikia wale ambao bado hawajafaidika na huduma hizi ili waboreshe maisha yao na kukuza Pato la Taifa," alisema Mjema.




Nini Kitatokea Usagara?

Chini ya kauli mbiu isemayo "ELIMU YA FEDHA, MSINGI WA MAENDELEO YA KIUCHUMI," wananchi watakaofika viwanjani hapo watapata elimu ya bure kuhusu Usimamizi wa fedha binafsi na uwekaji akiba.

Pia watajifunza utaratibu wa kukopa na kulipa madeni,Elimu ya kodi, bima, na bima ya amana,Uwekezaji katika hatifungani na masoko ya mitaji na Ulinzi wa mtumiaji wa huduma za fedha.

Alisema washiriki na Walengwa wa tukio hilo lilobeba mwavuli mpana wa wadau, likijumuisha Wizara mbalimbali kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Benki, Taasisi za bima, na asasi za kiraia.

Walengwa wakuu ni pamoja na wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs), wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu, wanafunzi, na watumishi wa umma.

Alisema mbinu mbalimbali kama semina, maonesho ya bidhaa, na majukwaa ya kidigitali zitatumika kufikisha ujumbe kwa wananchi watakaofika kwenye viwanja vya Usagara Jijini Tanga.

Alisema Wizara ya Fedha inatoa wito kwa wakazi wa Tanga na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kupata maarifa hayo ambayo yatatolewa na wataalamu wabobezi bila malipo yoyote.

"Hii ni fursa ya kipekee kwa mjasiriamali na mwananchi mmoja mmoja kuunganishwa na fursa za sekta ya fedha ili kukuza biashara na kuimarisha uchumi wa kaya," alisema.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...