Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha njia rasmi zinazotumika katika usambazaji wa taarifa za hali ya hewa nchini, huku ikiwasisitiza wananchi kuachana na matumizi ya taarifa zisizo rasmi zinazozagaa mitandaoni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa TMA – Ofisi ya Zanzibar, Masoud Makame Faki, alipokuwa akizungumza na wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kuwakaribisha kutembelea banda la TMA katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Nyamanzi kuanzia Desemba 29, 2025 hadi Januari 16, 2026.

Faki amesema wananchi wanapaswa kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa kupitia njia rasmi zinazotumiwa na TMA, ikiwemo vyombo vya habari vilivyosajiliwa, blogu na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz) pamoja na mitandao ya kijamii ya TMA ikiwemo YouTube, Instagram, Twitter (X), WhatsApp Channel na Facebook, ambazo akaunti zake zinapatikana kwenye ukurasa wa mwanzo wa tovuti ya Mamlaka.

“Ninawasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa kupitia njia rasmi za TMA na kuachana na tabia ya kusambaza taarifa potofu wanazozikuta mitandaoni, kwani zinaweza kuathiri mipango ya maendeleo inayotekelezwa nchini,” amesema Faki.

Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo, TMA inaendelea kutoa elimu na ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya hali ya hewa, ikiwemo hali ya fukuto la joto inayoendelea kushuhudiwa visiwani Zanzibar.

Faki ameeleza kuwa kwa sasa Dunia ipo kwenye mzunguko unaoelekea katika kizio cha kusini, hali inayosababisha kuwepo kwa jua la utosi na kuongeza kiwango cha joto. Aidha, kutokana na Zanzibar kuzungukwa na maji, unyevu huongezeka angani na kusababisha wakazi kukumbwa na hali ya fukuto la joto.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...