Na Mwandishi wetu Dodoma.

Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye ni Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ametoa Rai kwa Vijana wa Kitanzania,Wazazi na Walezi kutorubuniwa na yeyote kutoa fedha kwaajili ya kununua nafasi au fursa ya kujiunga na nafasi za JKT zilizotangazwa leo hii.

Brigedia Jenerali Mabena ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Januari 20,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akitoa Taarifa ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele ya kuwataarifu Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani kuhusu nafasi za kjiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2026 ambayo mchakato wake utaanza Januari 26,2026.

Na kuwasisitiza Vijana wa Kitanzania kwenda katika ngazi ya Halmashauri,Wilaya na Mikoa ambako ndiko mchakato unakofanyika kwa kushuka chini hadi ngazi ya Tarafa na Vijiji ili kupata fursa hiyo kwa wale ambao watakidhi vigezo na mahitajio kama ilivyoeleelezewa katika tovuti ya JKT. 

"Msisitizo wangu ni kwamba nafasi hizi haziuzwi kwahiyo pasije pakatokea mtu yeyote akataka kutumia fursa hii kwa kusema kwamba anaweza akampatia Mtanzania yeyote nafasi ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuweza kutoa kiasi cha pesa iwe kwa kutumiwa ujumbe wa simu au ana kwa nana".

Aidha amesema kuwa utaratibu wa vijana kuomba nafasi hiyo na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi hivyo ni vema kwenda huko ili kuepukana na utapeli wa mitandaoni.

Pamoja na kubainisha kuhitajika kwa vijana wenye taaluma za Diploma in Information Technology, Diploma in Business Information System, Diploma in Computer Science,Diploma in Information and Communication Technology (ICT) pamoja na taaluma zinginezo nyingi na mahitajio kama ilivyoanishwa katika tovuti ya Jeshi la Kujenga Taifa ya www.jkt.mil.tz.

"Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi".

Jeshi la Kujenga Taifa huwa linaendesha mafunzo ya aina tatu kama vile mafunzo ya lazima,mafunzo ya kujitolea kama haya yaliyo tangazwa na pia mafunzo kwa makundi maalum pale inapohitajika kwa wale wanaofanya kazi na jamii.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...