Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania Plc wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Happyness Lyimo ( wa pili kulia) pamoka na afisa wa kampuni hiyo Wema Mpwanga ( kulia), wakikabidhi Kapu la Voda kwa mzazi Martin Daud Sanga (Kushoti) na Mwanafunzi Jastin Daud Sanga (wa pili Kushoto).
Tukio hili ni muendelezo wa kampeni ya "Tupo nawe Tena na Tena" ambayo inalenga kugawa makapu yenye vifaa vya shule kwa wateja wao, ambapo msimu huu unalenga wazazi na wanafunzi wanaorudi mashuleni . Kampeni hiyo imeendelea kugawa makapu hayo sehemu mbalimbali nchini, na ikilenga kuwaunga mkono wazazi wanaopeleka watoto wao shuleni kwa mwaka mpya wa masomo kwa kuwapa baadhi ya vifaa vya shule vitakavyo wawezesha watoto kuendelea na masomo yao. Hafla hii imefanyika jijini Mbeya, Mwishoni mwa wiki.




.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...