• Mazoezi yajenga afya, mahusiano na tija kazini
• Ushirikiano wa taasisi waimarishwa kupitia michezo
• Eng. Samamba asisitiza uwajibikaji na uadilifu kusukuma matokeo
DODOMA
Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake wamehimizwa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kama njia ya kuimarisha afya, kujenga mshikamano na kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
Wito huo umetolewa leo Januari 24, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, alipofungua Bonanza la tatu la michezo lililowakutanisha watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake, ikiwemo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini pamoja na Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).
Akizungumza katika uzinduzi wa bonanza hilo, Mhe. Mavunde amesema kuwa, mazoezi ya viungo ni nguzo muhimu ya afya njema kwa mtumishi, ufanisi na tija kazini hivyo kuna umuhimu wa watumishi kujitokeza kwa wingi katika shughuli za michezo ili kuimarisha afya zao na kuendeleza mshikamano kazini.
Aidha, Waziri Mavunde amezitaka taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Madini kuendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuleta tija na matokeo chanya katika Sekta ya Madini mbele ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa.
“Tunayo dhamana kubwa ya kuwatumikia Watanzania. Michezo inatupa fursa ya kuimarisha afya, kudumisha amani, mshikamano na upendo, na kujenga umoja wetu kama familia moja ya sekta ya madini,” amesema Mavunde.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya Samamba, amewataka watendaji wa sekta hiyo kusimamia rasilimali za madini kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu ili kuhakikisha sekta inaendelea kuwanufaisha Watanzania na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.
Mhandisi Samamba amefafanua kuwa, Sekta ya Madini imeendelea kufanya vizuri, ambapo mpaka sasa mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umefikia asilimia 10.1 na makusanyo Serikali kufikia shilingi trilioni 1.071.
Ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na usimamizi madhubuti wa Wizara kwa kushirikiana na Taasisi zake.
Ameongeza kuwa juhudi za kuimarisha usalama katika shughuli za uchimbaji zimezaa matunda, huku akisisitiza kuendelea kuzingatia kikamilifu taratibu za afya, usalama na mazingira.
Eng.Samamba amewaelekeza Maafisa Madini Mkazi , kusimamia sehemu zenye mashimo hatarishi zisimamishwe mara moja na migogoro ya wachimbaji itatuliwe kwa haraka, hasa wakati huu ambapo bei ya dhahabu inaendelea kupanda.
Naye, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, ametoa wito kwa watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kuendelea kudumisha amani, mshikamano na upendo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa manufaa ya Taifa.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...