Na WAF, Dodoma

Waziri wa afya Mhe. Mohamed Mchengerwa leo amekutana na wawekezaji wa vifaa tiba kutoka kampuni ya A to Z iliyopo nchini Tanzania waliojitokeza kwaajili ya kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua sekta ya viwanda vya dawa nchini

Akizungumza jijini Dodoma Januari 12, 2026 Waziri Mchengerwa ameahidi kuwepo kwa ushirikiano mkubwa baina ya serikali na wawekezaji wa viwanda vya dawa nchini huku akisisitiza upatikanaji wa hati ya viwango kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa wenye nia ya kuwekeza

“Wawekezaji wamesema wapo tayari kushirikiana na serikali na wanafanya uwekezaji mkubwa ambao utatosheleza soko la ndani na sisi tumewapokea na tuko tayari kushirikiana nao lakini takwa la kwanza ni lazima wapate hati ya viwango kutoka WHO, lakini wamenithibitishi kwamba ndani ya mwaka mmoja watakuwa wamepata”

Amesema, Mpango wa serikali ni kuwa na viwanda kwa muda mrefu, huku akithibitisha kuanza kwa mchakato kwa wawekezaji hao wa kufuatilia hati za viwango za Good Manufacturing Practice (GMP) ambazo zinategemewa kupatikana ndani ya mwaka mmoja 

“Serikali ina mpango wa kuwa na viwanda vingi vyenye ubora vitakavyodumu kwa muda wa miaka 100, hatutaki kiwanda leo kipo, kesho imekuja seikali nyingine kimeshakufa, ndiyo maana tunashirikiana nao, tunawaunga mkono kwa ukaribu ili tujue palipo na changamorto tuzitatue”

Waziri Mchengerwa amewakaribisha A to Z na wawekezaji wengine kwenye Jukwaa la Uwekezaji katika Uzalishaji wa Dawa Tanzania lililoandaliwa na Wizara ya Afya kwa lengo la kuwakutanisha wawekezaji wa ndani na wa kimataifa katika sekta ya dawa, wazalishaji, washirika wa maendeleo pamoja na wadau muhimu kutoka sekta za afya na uwekezaji litakalofanyika Januari 19, 2026








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...