Na.Vero Ignatus, Arusha 

Wakala wa vipimo mkoani Arusha WMA wametoa onyo Kali Kwa wauzaji wa vitunguu kuacha kutumia vipimo vya  Rumbesa badala yake watumie vipimo vya mizani ili kupata thamani ya pesa na ujazo kamili bila kumuumiza mkulima wa zao la kitunguu.

Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Wakala wa  Vipimo mkoani hapa,Jassson Theonest  Wakati akitoa elimu Kwa wakulima wa vitunguu wa Bonde la Eyasi wilayani karatu,mkoani Arusha, amesema matumizi  sahihi ya mizani  ni msaada mkubwa kwa wakulima, kwani yanahakikisha kila kilo inafikishwa sokoni ipasavyo, kuongeza mapato yao na kuimarisha biashara zao.

Amesema kuwa endapo mtu yeyote atakiuka maagizo hayo hatua Kali za kisheria  zitachukuliwa na sambamba na akutozwa fain kuanzia milion Moja mpk milion 20 Kwa mujibu wa sheria.

Nasisitiza tena kwenu wakulima na mlitambue jambo hili kwamba matumizi sahihi ya mizan ni msaada mkubwa kwenu wakulima, kwani yanahakikisha kila kilo inafikishwa sokoni ipasavyo, kuongeza mapato yenu na kuimarisha biashara zenu"alisema.

Sambamba na hilo wakala ya Vipimo imefanya mafunzo kwa wakulima wa vitunguu katika maeneo ya Karatu na Mang’ola, yakilenga kuwafundisha kuepuka kutumia mizani batili na kuhakikisha wanapata kilo halisi za mazao yao.

Wakulima wa vitunguu Moshi Hitler na  Joyce Elia wamesema kwamba kutumia mizani isiyo sahihi iliwanyima haki zao, kwa kuwa mara nyingi walipoteza kiasi kikubwa cha mazao yao kwa kuuzwa chini ya kilo halisi, hali iliyosababisha kupoteza mapato na kushusha morali yao. Baadhi walisema walihisi kunyonywa na wakuu wa masoko ambao walitumia mizani batili kuwazidishia hasara.

Wakulima hao waliishukuru Mamlaka Hiyo kwa kutoa elimu hii muhimu na kuahidi kuanza kutumia mizani sahihi kila wanapouza vitunguu vyao.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...