Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wameonesha kuridhishwa kwao na utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Mfano kwa Wachimbaji Wadogo cha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichopo Lwamgasa, Wilaya ya Geita Manispaa.
Akizungumza mara baada ya kamati hiyo kukamilisha ziara yake, Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Subira Mgalu (Mb), ameipongeza STAMICO kwa jitihada kubwa inazofanya katika kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ikiwemo viwanda vya nishati safi rafiki (briquettes) na vituo vya mfano vya wachimbaji wadogo kama vile Katente na Lwamgasa.
“Kamati imefurahishwa na namna STAMICO inavyotekeleza miradi yake kwa kutumia teknolojia za kisasa, kutoa ajira kwa makundi mbalimbali ya wananchi, na kuchochea mapato ya Serikali kupitia kodi, mirabaha na gawio,” amesema Mhe. Mgalu.
Ameongeza kuwa, miradi hii inatoa mchango chanya katika kuchochea maendeleo ya jamii na kuwezesha wachimbaji wadogo kushiriki kikamilifu katika sekta ya madini kwa njia endelevu.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb), amewashukuru Wajumbe wa Bunge kwa ushauri, maoni na maelekezo yao, akisisitiza dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ushiriki wa wananchi katika sekta hiyo.
“Wizara ya Madini na taasisi zake itaendelea kujiboresha na kuweka mazingira bora kwa wanufaika wote wa rasilimali madini, sambamba na utekelezaji wa dira ya #Vision2030 – Madini ni Maisha na Utajiri,” amesema Mhe. Mavunde.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Bw. Deusdedith Magala, aliipongeza Kamati kwa ushirikiano na hamasa waliyoonesha katika kipindi cha ziara hiyo, akibainisha kuwa mapokeo chanya ya wabunge ni chachu kwa STAMICO kuongeza ubunifu na uwekezaji kwenye miradi yake.
“Tunashukuru kwa ushirikiano wa Kamati na tunajivunia kuona miradi yetu ikipata mrejesho chanya. STAMICO itaendelea kuwa kinara katika matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza tija kwa wananchi tunaowahudumia,” amesema Bw. Magala.
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeendelea kuwa taasisi ya mfano katika kukuza uchimbaji wa kisasa, ushirikishwaji wa wachimbaji wadogo, na uendelezaji wa teknolojia rafiki kwa mazingira inayochangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...