NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini katika kutekeleza ilani kwa vitendo na kukiimarisha na kukijenga chama imeamua kufanya ziara na sekretarieti kwa lengo la kuweza kukagua uhai wa chama hicho pamoja na jumuiya zake ikiwa sambamba na kupata fursa ya kufanya mikutano kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wao.
Katika ziara hiyo ambayo inaongozwa na Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya pamoja na jopo la sekretarieti ya chama hicho wameweza kushirikiana na viongozi mbali mbali wa Kata ya Kibaha na kujadili mambo mbali mbali ikiwemo suala ziama la uhai wa chama hicho.
Katibu huyo amesema kwamba wameamua kufanya ziara hiyo ya kupita katika kata mbali mbali na kukutana na wanachama wa ccm pamoja na viongozi wa kata ya Kibaha ikiwa ni kuangalia mwenendo mzima wa uhai wa jumuiya zake leengo kubwa ikiwa ni kukiimarisha chama na kujijenga.
"Tupo katika ziara yetu nikiwa nimeambatana na wajumbe wa sekretarieti ya chama wakiwemo kuutoka jumuiya ya wazazi, jumuiya ya umoja wa wanawake, pamoja na jumuiya ya umoja umoja wa vijana lakini wote kwa pamoja ni kutembea na kuweza kujionea hali halisi ya jinsi uhai wa chama ulivvyo pamoja na uhai wa jumuiya zake kwa hivyo hilo ndilo kubwa la ziara yetu hii,"amebainisha Katibu Kalleiya.
Kalleiya amesema kwamba kwa sasa muda wa uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo hakuna budi kushikamana kwa pamoja kati ya chama pamoja na kumuiya zake ili kuweza kujiandaa na chaguzi nyingine zinazokuja ndio maana wameona kuna umuhimu mkubwa wa kuwatembelea wanachama wao katika maeneo mbali mbali.
Ziara ya sekretarieti ya Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini imefanya ziara yake katika kata ya Kibaha pamoja na Kata ya Viziwaziwa ambapo lengo lake kubwa ni kutembea katika kata mbali mbali kwa ajili ya kuweza kuwatembelea wanachama wake pamoja na kuangalia suala zima la uhai wa chama jinsi ulivyo pamoja na kuweza kuangalia uhai wa jumuiya zake mbali mbali.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...