Na Belinda Joseph-Dodoma.
Matumizi ya Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania (TIPS) yameendelea kuleta mageuzi katika sekta ya fedha kwa kurahisisha miamala, kuongeza usalama wa fedha, kupunguza matumizi ya fedha taslimu (cash) na kuimarisha uwazi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Akizungumza na Michuzi TV Agosti 4, 2026, kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma, Afisa Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Fredriki Mwakuu, amesema BoT inaendelea kuhamasisha Watanzania kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali, hususan Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania (TIPS), ili kuendana na maendeleo ya teknolojia na kupunguza utegemezi wa fedha taslimu.
Amesema kupitia mfumo huo, wananchi sasa wanaweza kutuma fedha kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine, kutoka simu kwenda benki na kutoka benki kwenda kwenye mtandao wa simu kwa urahisi, jambo ambalo limeondoa changamoto zilizokuwepo awali katika kufanya malipo kati ya mitandao na taasisi za kifedha.
Mwakuu amesema matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali yameongeza usalama wa fedha kwa kuwa kila muamala huhifadhiwa kwenye mfumo na unaweza kufuatiliwa endapo kutatokea changamoto, tofauti na matumizi ya fedha taslimu ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa fedha kutokana na wizi au mazingira mengine.
Aidha, amesema mifumo hiyo inaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato kwa kuwa miamala yote huwa na kumbukumbu zinazoweza kufuatiliwa, hivyo kupunguza mianya ya udanganyifu.
Ameeleza kuwa BoT kwa kushirikiana na watoa huduma za kifedha imefanikiwa kupunguza gharama za kutuma fedha kati ya benki na mitandao ya simu, huku juhudi zikiendelea kuhakikisha gharama hizo zinapungua zaidi ili kuwahamasisha wananchi kutumia malipo ya kidijitali.
Kwa upande wa Mfumo wa Malipo Makubwa (TISS), amesema BoT imepunguza gharama za miamala ambapo kiwango cha chini cha ada kimeshushwa kutoka mfumo wa awali hadi shilingi 2,000, huku kiwango cha juu kikiendelea kuwa shilingi 10,000.
Amesema BoT ina jukumu la kuanzisha, kusimamia na kuboresha mifumo yote ya malipo nchini pamoja na kutunga kanuni, kufanya ukaguzi wa taasisi zenye leseni za huduma za malipo na kuhakikisha mifumo hiyo inalinda maslahi ya watumiaji.
Mwakuu amesema mifumo inayosimamiwa na BoT ni pamoja na Mfumo wa Malipo Makubwa (TISS) unaohudumia miamala inayozidi shilingi milioni 20, Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania (TIPS) kwa miamala isiyozidi shilingi milioni 20 unaounganisha benki na mitandao ya simu, pamoja na mifumo ya uchakataji wa hundi na huduma nyingine za malipo ya kielektroniki ikiwemo ulipaji wa mishahara.
Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali kwani ni salama, rahisi na yenye kuaminika, ambayo ina ufanisi na zinazokidhi mahitaji ya wananchi na ukuaji wa uchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...