Na Mwandishi Wetu
WALEZI wa watoto katika vituo vya kulelea watoto nchini wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya kitaalamu yatakayotolewa na Chuo cha Future World, hatua inayolenga kupunguza uhaba wa wataalamu wa malezi na makuzi ya awali ya watoto nchini.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chuo cha Future World Institute Robert Mkolla katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na Ofisa ustawi wa Jamii kanda ya saba Chanika Judith Mrema kwa kushirikiana na Umoja wa Vituo vya Kulea Watoto Tanzania (UVIKUWA), chini ya uratibu wa chuo cha ufundi stadi cha Future kilichopo Chanika kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam.
“Mafunzo hayo yameandaliwa kujibu ongezeko la mahitaji ya walezi wenye taaluma, linalochochewa na kuongezeka kwa vituo vya kulelea watoto kutokana na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuongezeka kwa wazazi wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji mali.”
Aidha, Mkolla amesema programu hiyo inaendana na Sera ya Elimu ya mwaka 2014, toleo la mwaka 2023, inayomtaka kila mtoto kupitia elimu ya awali kabla ya kuanza darasa la kwanza, jambo lililoongeza mahitaji ya huduma bora za malezi na makuzi ya awali.
Amefafanua mafunzo hayo yatawawezesha walezi kupata maarifa na stadi za kitaalamu kuhusu ukuaji wa mtoto, afya, usalama na elimu ya awali ili kuboresha huduma wanazozitoa.
Ameongeza programu hiyo pia itachangia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana, hususan wahitimu wa kidato cha nne, kwa kuwapatia ujuzi unaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri katika sekta ya malezi ya watoto.
“Vituo vingi vya kulelea watoto bado vinategemea watu wasio na taaluma kutokana na uhaba wa wataalamu, hali inayoweza kuathiri ubora wa huduma zinazotolewa kwa watoto.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vituo vya Kulea Watoto Tanzania (UVIKUWA Tanzania), Shabani Kibabi, amesem mafunzo hayo yataimarisha viwango vya malezi katika vituo vya kulelea watoto na kuchangia ustawi wa watoto kwa kuwawezesha walezi kupata ujuzi na taaluma stahiki.
Pia amesema katika mkutano huo umewajengea washiriki uwezo katika ujasiriamali na mbinu za kuongeza kipato, hatua itakayowasaidia kuboresha uendeshaji wa vituo vyao sambamba na utoaji wa huduma bora za malezi.
Kibabi amesema mbali na kozi ya malezi ya watoto, Chuo cha Future World kinatoa kozi nyingine zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira, ikiwemo mafunzo ya kompyuta yanayochangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Naye Mwenyekiti wa UVIKUWA Mkoa wa Dar es Salaam, Muhina Mwarabu, amesema programu hiyo itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walezi wenye sifa katika vituo vya kulelea watoto.
Amewahimiza walezi pamoja na wamiliki wa vituo vya kulelea watoto kutumia fursa hiyo ya mafunzo, akisema ada ya Shilingi 800,000 ni nafuu na itawawezesha watu wengi zaidi kupata taaluma ya malezi ya watoto, hatua itakayoinua ubora wa huduma za malezi nchini.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...