Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa kuhusu masuala ya usalama dhidi ya majanga ya moto na namna ya kuchukua tahadhari katika maeneo mbalimbali.
Katika maonesho hayo, wananchi wamepatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto pamoja na hatua za kuchukua wakati yanapotokea majanga hususani Jikoni wakati wa kupika kwa kutumia Nishati ya gesi, Jeshi hilo pia limeendelea kutoa elimu ya huduma za uokoaji na umuhimu wa wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona majanga mbalimbali ikiwemo moto.
Zoezi hilo ni muhimu katika kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu kinga na tahadhari dhidi ya moto, huku wananchi wakihimizwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu na kuchukua hatua za usalama katika maeneo ya makazi, biashara na shughuli nyingine za kiuchumi.




.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...