Wakulima Kanda ya Kati wamehimizwa kutumia huduma za kifedha kidijitali zinazotolewa na Mixx by Yas ili kurahisisha upokeaji wa malipo ya mazao, kupata mikopo na kufanya miamala kwa usalama.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Biashara wa Mixx by Yas Kanda ya Kati, Bw. Charles Gasper, wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.
Amesema kupitia huduma ya Mixx Kilimo, wakulima wanaweza kupokea malipo ya mazao moja kwa moja kupitia simu, kupata mikopo ya Kilimo Pesa inayofikia hadi shilingi milioni tatu, pamoja na kunufaika na huduma za bima ya afya ya mifugo.
Kwa upande wake, Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka amesema ushirikiano kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Ushirika na Mixx by Yas umeongeza matumizi ya malipo ya kidijitali kwa wakulima na vyama vya ushirika mkoani humo.
Amesema wakulima wengi sasa wanapokea malipo ya mazao yao kwa njia ya simu baada ya minada, hatua inayopunguza usumbufu wa kusafiri kufuata fedha mbali na kuongeza usalama kwa wakulima.
Aidha, amesema huduma za Mixx zimeendelea kuwezesha vyama vya ushirika na SACCOS mkoani Dodoma kufanya miamala kwa urahisi, huku akiipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake katika kuimarisha ujumuishaji wa huduma za kifedha kidijitali kwa wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...