Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, ameendelea na ziara katika Jimbo la Tumbatu kwa lengo la kukagua uhai wa Chama, kusikiliza changamoto za wanachama na wananchi, pamoja na kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya Chama.

Katika ziara hiyo, Ndugu Abdi ametembelea Matawi ya CCM ya Mkokotoni, Mto wa Pwani, Kiongele na Pale, ambako amezungumza na wanachama na wananchi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.

Ndugu Abdi amewataka viongozi na wanachama wa CCM kuendelea kudumisha umoja na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa wanachama kutimiza wajibu wao wa kulipa ada za Chama ili kuwezesha shughuli za CCM kutekelezwa kwa ufanisi kuanzia ngazi ya tawi hadi jimbo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Zanzibar, Ndugu Ali Issa Ali, amesema ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano baina ya viongozi na wanachama kuanzia ngazi ya tawi hadi jimbo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndugu Khadija Salum Ali, amesema Wizara inaendelea kuchukua hatua na kuweka mipango ya kuhakikisha changamoto zinazokabili sekta ya elimu katika maeneo ya Kiongele na maeneo mengine zinapatiwa ufumbuzi.

Aidha, Ndugu Abdi ametumia ziara hiyo kuwatembelea na kuwajulia hali baadhi ya Wazee wa Chama, hatua aliyoieleza kuwa ni sehemu ya kuendelea kujenga mshikamano, upendo na utamaduni wa kujali hali za wanachama na viongozi wa CCM.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...