Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametoa maeekezo kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kukaa meza moja na wazalishaji wa saruji nchini ili kuweka mikakati ya haraka itakayohakikisha saruji inapatikana kwa wingi na bei nafuu.

Ametoa maelekezo jijini Dar es Salaam alipokuwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Mzalishaji Bora Viwandani (President’s Manufacturer of the Year Awards - PMAYA), zinazoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Akieleza kero ya wananchi kuhusu gharama za ujenzi, Makamu wa Rais amesema kwamba wananchi wanalazimika kununua saruji kwa bei kubwa kutokana na usimamizi na uratibu dhaifu wa uzalishaji viwandani, jambo ambalo linaenda kinyume na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na bei ya saruji kuwa juu Makamu wa Rais Ndejembi amesema” Nakuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kaeni mmalize hili suala ili mwananchi apate saruji kwa bei iliyokuwepo awali.

Amesisitiza baada ya Wizara hiyo kukaa anataka kupata ripoti kuhusu jambo hilo huku akiwataka wajadili na kisha mwandike ripoti ambayo itakabidhiwa kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...