Na mwandishi wetu
DODOMA. Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, amewataka watumishi wapya 328 kutumia mafunzo ya kijeshi na ukakamavu waliyopitia kujenga nidhamu, uadilifu na weledi katika kulinda rasilimali za misitu na nyuki nchini.
Profesa Silayo amesema hayo leo, Jumatatu, Septemba 14, 2026, wakati akifungua mafunzo elekezi kwa watumishi hao katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP-Mipango), Dodoma.
Watumishi hao wamepitia mafunzo ya awali ya kijeshi na ukakamavu katika Kituo cha Mafunzo cha TFS, Mlele kwa miezi sita, kabla ya kuanza majukumu katika vituo mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Profesa Silayo amesema mafunzo hayo hayakuwa mepesi, lakini yamewajengea nidhamu na ukakamavu unaohitajika katika kutekeleza majukumu yao kama askari wa uhifadhi.
Amewataka kufanya kazi kwa bidii, ubora na utu, huku wakiepuka rushwa, tamaa, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka.
“Tufanye kazi hii kwa bidii, tuifanye kwa ubora wa hali ya juu, lakini tufanye kwa utu,” amesema.
Amesema watumishi hao wana taaluma mbalimbali, zikiwamo uhandisi, afya, manunuzi, uhasibu, misitu na nyuki, lakini wameunganishwa na dhamira moja ya kulinda na kuendeleza rasilimali za misitu na nyuki.
Pia amewataka kuheshimu viongozi na mfumo wa uongozi, kujifunza kutoka kwa watumishi waliowatangulia na kutumia taaluma zao kwa manufaa ya TFS na Taifa.
Baada ya kukamilisha mafunzo hayo elekezi, watumishi hao wanatarajiwa kupangiwa vituo mbalimbali vya kazi nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...