Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, ameahidi kuendeleza ushirikiano kati ya taasisi hiyo na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP-Mipango).

Profesa Silayo amesema hayo leo, Jumatatu, Septemba 14, 2026, jijini Dodoma, alipomtembelea Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Hozen Mayaya, katika Main Campus ya IRDP-Mipango, kabla ya kushiriki katika ufunguzi wa programu ya mafunzo kwa watumishi wapya walioajiriwa na TFS katika kampasi ya Miyuji.

Amesema ushirikiano kati ya TFS na IRDP-Mipango ni muhimu katika kuimarisha mahusiano ya kitaasisi na kuwezesha taasisi hizo kushirikiana katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote.

Kwa upande wake, Profesa Mayaya amemshukuru Profesa Silayo na TFS kwa ushirikiano uliopo, akisema chuo hicho kimekuwa kikifaidika na huduma na msaada mbalimbali kutoka TFS.

Ameutaja miongoni mwa ushirikiano huo ni upatikanaji wa miche ya miti kutoka TFS kila inapohitajika kwa ajili ya kupandwa katika maeneo mbalimbali ya chuo na katika jamii.

Profesa Mayaya amesema ushirikiano huo umeendelea kuchangia juhudi za utunzaji wa mazingira na kuongeza uoto wa miti katika maeneo ya chuo na jamii inayokizunguka.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...