Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Ramadhan Kimara, ameonya kuwa hatamvumilia mtumishi yeyote wa halmashauri atakayehusika na utoroshaji wa korosho, akisema vitendo hivyo vinaikosesha halmashauri mapato yanayostahili.
Kimara ametoa onyo hilo Oktoba 13, 2026, wakati akizungumza na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha halmashauri hiyo, baada ya kukamilika kwa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Zao la Korosho wilayani Kibiti.
Amesema korosho na ufuta ni miongoni mwa mazao yenye mchango mkubwa katika kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri, hivyo ni muhimu kuimarisha usimamizi wake ili kuzuia utoroshaji na upotevu wa mapato.
“Halmashauri yetu ili iongeze mapato ya ndani inategemea mazao kama korosho na ufuta. Hivyo, kama sisi tutakuwa tunasinzia au tunakosa usimamizi mzuri na kusababisha korosho kutoroshwa, mapato yatapotea. Sitamvumilia mtumishi yeyote atakayekuwa miongoni mwa wanaotorosha korosho,” alisema Kimara.
Alifafanua kuwa atazungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti kwa lengo la kuimarisha usimamizi na doria za kudhibiti utoroshaji wa korosho, akisisitiza kuwa yuko tayari kushiriki doria hizo usiku na mchana inapohitajika.
Aidha, Kimara amesisitiza umuhimu wa wakulima kulipwa stahiki zao kwa wakati ili kupunguza malalamiko na kuimarisha imani yao katika mfumo wa biashara ya korosho.
Amewataka wakulima kutumia vizuri mapato wanayopata kutokana na mauzo ya mazao yao kwa kuzingatia mahitaji ya msingi ya familia na kuwekeza katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi ili kuboresha maisha yao.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...