Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Faris Burhan, amewasili Zanzibar na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mara baada ya kuwasili, Faris alikutana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, kwa lengo la kujitambulisha na kuimarisha mahusiano ya kiuongozi ndani ya chama hicho.
Akiwa Kisiwandui, Faris alitembelea kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, na kumuombea dua kwa kutambua mchango wake katika historia ya Zanzibar.
Baadaye, Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alitembelea ofisi za umoja huo zilizopo katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar, ambako alizungumza na vijana waliojitokeza kumpokea.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha mshikamano, kuendeleza mawasiliano na vijana pamoja na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya UVCCM katika kukijenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...