"CCM"
Showing posts with label CCM. Show all posts

Na Emmanuel Masaka,Michuzi TV

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, ametoa rai Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 Oktoba, mwaka huu huku akisisitiza kufanya hivyo ni haki yao ya kikatiba.

Abdulla ametoa rai hiyo wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba, kwenye viwanja vya ZSM Mjimbioni.

Amesema, “Watanzania jitokezeni kwa wingi mkapige kura, kwani kupiga kura ni haki yenu ya msingi kama raia wa Tanzania.”

Aidha,Abdulla amewataka wananchi kuwapa kura wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi mbalimbali, ili kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa na Serikali chini ya uongozi wa chama hicho.

Awali Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Abdallah Kassim, kupitia tiketi ya CCM, ameeleza kwamba katika Jimbo la Mtambile ni sherehe za ushindi ndizo zinaendelea na hakuna dalili zozote za maandamano.

Pia amesema wananchi wa Jimbo la Mtambile wako tayari kumpa kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Akihitimisha hotuba yake,Hemed amewataka Watanzania wote kuendelea kuilinda na kuithamini amani ya nchi kama walivyoikuta, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo na ustawi wa taifa.

“Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kubaki nchi ya amani. Tuihifadhi amani hii tuliyoirithi kutoka kwa waasisi wa taifa letu, kwani bila amani hakuna maendeleo,” amesema Hemed.

Kampeni hizo za CCM katika Jimbo la Mtambile zimefungwa rasmi kwa amani, hamasa kubwa na mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza wakati wa kufunga kampeni Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akimnadi na kumuombea kura kijana Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Abdallah Kassim,
(Picha  zote na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)











MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi amesema kuimarika kwa Uzalishaji wa Korosho mkoa wa Lindi ni matokeo ya jitihada za Dk.Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira mazuri, kuipa nguvu sekta ya kilimo kwa kuongeza wigo mpana kwenye ruzuku ya mbolea,mbegu na dawa.


Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 03, 2025 alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Maegesho, Kata ya Boma, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi,ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Urais kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025.

Akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Nachingwea alipokuwa akinadi sera za CCM na kuomba kura,Dkt.Nchimbi amesema yote hayo yamewezekana ni kwasababu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aliweka kipaumbele kwenye sekta ya kilimo.

Ameongeza Dkt.Samia katika sekta ya kilimo ameongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka Sh.bilioni 294 mwaka 2020 na kufikia zaidi ya trilioni moja mwaka 2024.

"Kingine ambacho nataka kusema hapa mazao ya Korosho katika mkoa wa Lindi yalipanda kutoka tani Elfu thelathini hadi kufikia tani elfu tisini ndani ya miaka minne ya utendaji kazi wa Dkt Samia Suluhu Hassan,”amesema.

Aidha baada ya kuwahutubia Wananchi hao,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa Jimbo la Nachingwea,Ndugu Fadhili Ally Liwaka pamoja na Madiwani.

Dkt.Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni nchini kote kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Pamoja na kuomba kura pia ameendelea kunadi  sera na Ilani ya chama hicho,iliyolenga kuboresha maisha ya Wananchi na maendeleo kwa ujumla,ambapo mpaka sasa amefika mkoa wa 17 tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam.





 


KATIBU Msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM, Ndg. Bulugu Magege, leo tarehe 30/09/2025 amekutana na vijana wa Kata ya Mlowo na kuwasisitiza kuhakikisha kura zao zote wanampa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wa CCM katika ngazi zote.

Katika mazungumzo hayo, Bulugu aliwaeleza vijana kuwa Ilani ya CCM imewapa kipaumbele kikubwa vijana ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, ajira, elimu bora na uwezeshaji kiuchumi. Alisisitiza kuwa Dkt. Samia ni Rais mwenye upendo mkubwa kwa vijana, anayetamani kuwaona wakibadilisha maisha yao kupitia fursa alizozileta.

Bulugu aliambatana na Ndg. Haji Shabani Mwalimu, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbozi na Ndg. Noel Donald Mkwemba, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Songwe. Vijana wa Mlowo walimhakikishia kuwa wako tayari kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.
#OktobaTunatiki✅✅
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazoZoteTunawashaKijani





Picha mbalimbali za matukio ya Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika leo Septemba 29,2025 katika viwanja vya Malamba Mawili,Jimbo la Kibamba wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.










 

 


Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mariam Ibrahim, leo Septemba 19, amemuombea kura Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimbo la Kibaha Vijijini, mkoani Pwani.


Akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo, Mariam aliwataka kumuunga mkono Rais Samia pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kuendeleza kasi ya maendeleo.
“Naomba tumpe kura za kishindo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, sambamba na wagombea wetu wa ubunge na udiwani. Kipeni kura Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Kibaha Vijijini,” alisema Mariam.