"TANZIA"
Showing posts with label TANZIA. Show all posts

Na Mwandishi Wetu

Tasnia ya filamu nchini imepata pigo kufuatia kifo cha msanii mkongwe, Mzee Kambi, kilichotokea leo Aprili 27, 2026.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Msemaji wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Coletha Raymond, aliyesema kuwa msanii huyo alifariki dunia ghafla alipokuwa akiendelea na shughuli zake za kazi.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Coletha alisema Mzee Kambi alikuwa ametoka mkoani Tabora kikazi na aliporejea alielekea moja kwa moja katika shughuli zake kwenye studio za Pilipili, kabla ya kuanza kujisikia vibaya.

“Ni kweli tumempoteza Mzee Kambi. Alikuwa ametoka Tabora na alipofika alienda moja kwa moja kazini katika studio za Pilipilibl. Akiwa kazini ndipo alipozidiwa ghafla na kukimbizwa hospitali, lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia,” alisema Coletha.

Aliongeza kuwa chanzo cha kifo kinahusishwa na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimsumbua, ikiwemo presha na kisukari.

Aidha, alisema Shirikisho la Filamu Tanzania linaendelea na taratibu za ndani kwa kushirikiana na familia ya marehemu ili kupanga mipango ya mazishi, ambapo taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Kifo cha Mzee Kambi kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya filamu nchini, ambapo amekuwa mmoja wa wasanii waliotoa mchango mkubwa katika kukuza sanaa hiyo kwa muda mrefu. 


On August noon in forty-four, beneath Tanganyika’s sky,
In Mwazye’s quiet parish land, a child began to cry.
The sixth of nine, yet heaven-marked before the world could see,
A shepherd chosen long before he bent his first small knee.

His sister saw the spark in him and made a solemn vow,
To guard his dream with sacrifice, though trials pressed her brow.
Her youth she gave, her wages too, his schooling to defend,
So he might serve the Lord of Life until his journey’s end.

Through Karema’s halls and Kaengesa’s rising gleam,
Through Kipalapala’s sacred books and nights of ceaseless stream,
His mind grew luminous, his spirit ardent, his purpose living beam,
A leader formed by discipline, by prayer, by sacred theme.

Ordained a priest in seventy-one, still humble, still afraid,
Yet faithful to the call of God, whatever price was paid.
In Rome he drank from ancient wells of moral truth and grace,
Then hastened home to serve his land, not seek a higher place.

A bishop young in Nachingwea, in Tunduru he stood,
To build where little yet was formed, to plant where none yet could.
Though fear would knock upon his heart whenever roles were new,
His answer was obedience, God’s will he would pursue.

In Dar he rose to guide the flock where giants once had been,
A Cardinal in scarlet red, yet simple still within.
He asked, “Why beg for distant grain when ours can fill the bowl?”
And taught the Church to stand upright in dignity of soul.

From twenty parishes he dreamed of one hundred in their place,
They doubted such a vision vast could ever run that race.
But when he laid the crozier down and passed the charge along,
One hundred eighteen stood in faith, his vision proved them wrong.

For death to him was not defeat, nor darkness, nor despair,
But simply door to promised glory beyond all earthly care.
The pilgrim laid his labors down where saints and angels sing,
And entered joy no mortal tongue could fully name or bring.

Though on 19 February he left this earthly state,
On 28 February, in solemn farewell we congregate.
Not stripped of honor, nor lost to sight,
But clothed in dignity, in hallowed rite.

A priest for decades he faithfully stood,
A guide in truth, in strength, in good.
A bishop, archbishop, cardinal upright,
A conscience steady in nation’s sight.

Eternal rest, O Lord, bestow,
Let endless light upon him glow.
May he who led with faithful hand
Now dwell within God’s promised land.

And when the final trumpet rings,
And time surrenders all its kings,
May the shepherd, his flock, and the Church above,
Rejoice in resurrected love.

His spirit whispers still,
Through every heart he touched, through every faithful will.
Though tears may fall, his love will never fade,
A shepherd, father, guide, forever ours to aid.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


- The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.


.
RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi anasikitika kutangaza kifo cha Kaka yake Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi aliyefariki leo, Alhamis Tarehe 25 Septemba 2025 Jijini Zanzibar..

Ibada ya kumsalia Marehemu itafanyika katika Msikiti wa Zanzibar ( جميع ) - Msikiti wa Qaboos baada ya sala ya Ijumaa na baada ya hapo maziko yanafanyika Mangapwani katika eneo ambalo amezikwa Mzee Ali Hassan Mwinyi - ambapo watu waliopo maeneo ya Mangapwani, Bumbwini, Fujoni na maeneo ya karibu watapata kutabaruku kabla ya kuzika.

Visomo Msikitini vitaanza saa 4 asubuhi.


I met him first in twenty-eleven’s glow,
At Chef’s Pride Restaurant, where humble spirits show.
Othman Michuzi bridged our fates that day,
A greeting warm, his light led the way.

Through Kigamboni’s sunlit streets,
He fought for justice, never defeat.
With courage firm, he stood his ground,
His wisdom a compass, his resolve profound.

Family first, his golden creed,
In every moment, he saw their need.
No birthday missed, no milestone ignored,
In love's pure light, his spirit adored.

Music flowed within his soul,
Professor Jay’s lyrics made him whole.
Dancing, laughing, with his kin,
A melody of life played deep within.

To Martha, his light, his shining star,
He taught her dreams could take her far.
"Give your best, never settle for less,"
A father’s lesson, a life to impress.

To Melvin, his son, he left a flame,
A legacy built on honor and name.
"Be brave, be kind, let truth be your guide,
In every storm, let faith abide."

As Africa called, he answered its plea,
A vision for health, for humanity.
First among Tanzanians to rise,
To WHO’s halls beneath global skies.

But fate, relentless, had plans untold,
Took him away, a story left unrolled.
Before his path could fully unfold,
His spirit ascended, pure and gold.

We'll rise again, though hearts may ache,
To honor his dreams, for his great sake.
As Samia vowed, we'll proudly maintain,
A Tanzanian voice in WHO's domain.

Now, we mourn, yet celebrate too,
The life he lived, the dreams he pursued.
For Faustine’s light, though dimmed in time,
Still shines in hearts, a hope sublime.

Oh, Tanzania, lift your head,
For even in grief, his life is widespread.
In every soul he touched, we see,
The power of love and legacy.

Rest now, dear leader, father, and friend,
Your journey may stop, but it shall not end.
In hearts we hold and steps we've trod,
You live in us, a gift from God.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


— The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.




In the morning light of Mara’s land,
Where grasses whispered across red sand,
A child of sun and soil was born,
To rise, to serve, to bear the horn.

A herder first, of goats and dreams,
He wandered fields and watched the streams.
Yet fate, with plans both strange and wise,
Had bound his path to broader skies.

In 1942, with Africa’s call,
He left the fields, he gave his all,
From Butiama’s soil to KAR’s might,
In fields of valor, he learned to fight.

Through islands thick with jungle heat,
To lands where oceans’ powers meet,
He marched with brothers, bound by code,
And carved his path on war’s dark road.

Through gunfire, wounds, through loss and gain,
Where echoes stilled but scars remained,
He fought like thunder, fierce and bright,
Through darkest hours, he held the light.

Madagascar’s siege, a storm-wrought test,
Where young men proved their might, their best.
With every mile, his courage grew,
And through each step, the legend too.

In Burma’s mire, through fire and steel,
Where soldiers walk and wounds don’t heal,
He bled, he fought, he held his ground,
In silent strength, his name renowned.

Not just in rank, but heart and grace,
A sergeant rose with measured pace.
To lead, to teach, to stand as guide,
A gentle strength, with honor tried.

Through winds of war, in Simba’s hills,
Where battle roared, and time stood still,
He earned a name, “Mutukula’s” fame,
A spirit fierce, an unquenched flame.

When Amin fled and battles ceased,
Musuguri stood as peace’s priest,
Two days a ruler, by duty’s hand,
Then back he went to his cherished land.

For every year he lived and more,
From sea to field, from peace to war,
In every breath, in every stand,
He served with heart, his promised land.

A soldier’s honor, a timeless grace,
In the land of heroes, your spirit we trace.
So rest, great General, the world will keep,
Your story’s light, where legends sleep.

With solemn pride, I offer my salute,
In tribute to you, a hero so true.
A gun salute will sound, echoing high,
For your valorous heart, we honor and cry.

Thank you.

Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396


— The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.


 



Safari ya mwisho ya Raymond Moyo Isaac Anderson Mwamusiku huko Maryland nchini Marekani

Ni mnyakyusa wa Usale,Kyela,Mkoani Mbeya

Mwili wake kuletwa nchini wiki ijayo kwa maziko


Yalikuwa majira ya usiku mwingi,lakini kwa Raymond huo ulikuwa ndiyo muda wa kawaida wa kutoka kazini siku zote.Baada ya kutoka kazini alikuwa akiendesha muda mrefu kurejea nyumbani kwake.

Alikuwa anaishi katika mji Columbia,ambayo ni sehemu ya Jiji la Baltmore,jimbo la Maryland nchini Marekani.Ameishi mjini hapo kwa takriban miaka 16, akiwa mkazi wa nchi hiyo mwenye Ukazi maalum wa kiwango cha Green Card.

Siku hiyo aliendesha gari lake aina ya Subaru Imprezza nyeupe,
mpaka alipofika mahali njiani mwili ukawa umechoka.Akaamua kupaki gari kwa muda kidogo hapo ili apumzike kwani alikuwa anajisikia usingizi pia.Akalaza kiti cha gari na kujipumzisa kidogo, na hapo hapo usingizi mzito ukampitia,akalala mazima.

Kwa kawaida watu wanaoamua kulala au kupumzika kando ya barabara au sehemu kama hizo, wanayaacha magari yakiwa yanaunguruma, huku heater ikiwa imewashwa kama ni msimu wa baridi, au AC ikiwa imewashwa endapo ni msimu wa joto.Ndiyo kusema kwamba lazima gari liwe na mafuta ya kutosha kwa maana ya full tank.

Lakini kwa ndugu yetu kwa sababu ya uchovu ule na kama alivyosimulia yeye mwenyewe baadaye akiwa hospitalini, ni kwamba alipolaza tu kiti kile, usingizi mzito ulimjia na akalala moja kwa moja.

Alisema alichokumbuka yeye ni kwamba gari lake ilikuwa na mafuta nusu tenki tu na gari ilikuwa ikinguruma na alikuwa anajipumzisha tu kidogi ili baadaye aendelee na safari yake.

Cha ajabu usingizi ule ulikuwa wa muda mrefu mpaka alipokuja kustuka baadaye na kuona kwamba miguu yake na sehemu za mbavu tayari zimegandishwa na barafu ambayo ilidondoka usiku ule.Pia baadhi ya sehemu za mikono yake nazo zilikuwa zimeanza kuganda,kasoro vidole tu vya mikononi ndivyo vilikuwa vinafanya kazi.

Ndipo kwa taabu aliinua kiwiliwili chake kutoka kwenye kiti cha gari na kuichukua simu yake.Akapiga simu za dharula, ambapo kikosi ya maafa kilikuja na kumchukua na kumkimbiza kwenda katika Hospitali ya Howard County General hospital,ambako alipelekwa moja kwa moja ICU

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari yake ya kukaa hospitalini hapo kwa matibabu kwa zaidi ya miezi 7 huku akipumulia mashine, akijiuguza mapafu yake ambayo madaktari walisema yalikuwa yamejaa maji.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake mpaka Mungu alipomchukua Septemba 12, 2024.

Nchini Marekani ameacha mtalaka na mtoto wa miaka 14 aitwaye Mpoki.Nchini Tanzania pia aliacha mtoto wa kiume aitwaye Rodgers.

Akiwa hospitalini aliacha ujumbe kwa madaktari kwamba Mpwa wake aitwaye Julius Mwakaleja anayeishi Jimbo la Texas ndiye amsimamie hapo hospitalini wakati wote.

"Julius ukiona nimezidiwa hapa hospitalini wewe ndiye utakayekuja kuzima mashine ya upumuaji ili niondoke zangu," alimwambie mpwa wake huyo na Julius ambaye alimjibu kwamba hilo halitakaa litokee.
"Sitaweza kuzima mashine yako Uncle,nakuahidi, utapona tu,mwamini Mungu," alisema Julius.

Hospitali ilijaribu mara kadhaa kusema apelekwe kituo cha kulelea wagonjwa na kwamba hospitali hapamfai tena,lakini hilo nalo Julius alilipinga sana.

Ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba hatimaye amempumzisha mtumwa wake Raymond kwa uamuzi wake Mungu mwenyewe pasipo shinikizo lolote la hospitali wala mtu mwingine yoyote.

Kama ilivyo kawaida ya misiba inayotokea nchini humo,kufuatia msiba huu,jumuiya mbalimbali za Diaspora huko Marekani,zikiongozwa na Julius na marafiki zake zinapambana changisha pesa ili mwili wa marehemu uweze kurejeshwa nchini Tanzania. Lengo likiwa ni kuupumzisha kwenye makaburi ya familia yaliyopo kwenye Kitongoji cha Sumbi,Kijiji cha Usale,Kyela mahali ambapo ndipo alipolala Baba yake Mzee Isaac Anderson Angindike Mwaibila Mwamsiku.

Kwa hapa Tanzania familia ya Asyukile Mwakilima Mwakanyamale wa Kijiji cha Isaki na Thompson Mwakasisi wa Kijiji cha Talatala,Kyela ndizo zinazoratibu msiba huo,wakiongozwa na David Mwakasisi, ambaye marehemu ni mdogo wake kwa Mama mdogo.

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kuletwa nchini Tanzania kuanzia wiki inayoanza Jumatatu Septemba 23,2024.Wale wote wanaomfahamu Raymond pokeeni taarifa za kifo chake.

Rambirambi zinapokelewa na

Kwa walioko nje ya nchi rambirambi itumwe kwa

Julius Thompson Mwakaleja

CashApp: $JuliusMwakaleja

Zelle (913)-271-3767-Julius Mwakaleja

Kwa Tanzania rambirambi itumwe kwa:

Salome Mwakasisi 0755 699 202
Jackson Mwakanyamale 0744841628

Historia ya maisha yake

Raymond alizaliwa Juni mwaka 1969 katika Kitongoji cha Sumbi,Kijiji cha Usale wilayani Kyela, katika familia ya Mama Evelyn Eselina Mwakilima na Mzee Anderson Mwamsiku,ambapo yeye alikuwa ni mtoto wa kwanza.

Elimu ya msingi aliipata katika shule ya msingi Sumbi.Baada ya hapo alisoma shule ya sekondari Ipinda kidato cha kwanza na cha pili, kabla ya kuhamia Sekondari ya Kyela ambayo kwa sasa inaitwa Itope.Shule zote mbili wakati huo zilikuwa zinamilikiwa na Jumuiya ya Umoja wa Wazazi ya CCM. 

Kutoka Kyela sekondari alifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda shule ya serikali ya Kantalamba,Sumbawanga mkoani Rukwa kwa masomo ya HGL.Hapo Kantalamba alipata elimu ya kidato cha tano na cha sita.Baada ya kupata mafunzo ya JKT alienda kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu na kuhitimu masomo ya Ualimu kikiwemo Kiingrereza na Jiographia.

Baada ya kumaliza masomo hayo alipangiwa kufundisha sekondari ya Kibiti mkoani Pwani ambako alifundisha kwa muda kisha akaona asiendelee ualimu ambao ndio ilikuwa fani yake.Badala yake akatafuta kazi tofauti na ualimu.Alijikuta anafanya kazi sehemu mbalimbali ikiwemo kampuni ya simu ya Airtel na magazeti ya New Africa na Afrika Leo, ambayo yalikuwa ni magazeti ya kwanza ya mitandaoni nchini Tanzania,nayeye akiwa miongini mwa Wahariri wake.

Akiwa huko kazini aliomba na kupata nafasi ya kusoma digrii ya upili katika chuo kikuu cha North Virginia ambapo alihitimu Masters Degree in Project Management.

Akiwa nchini humo alishiriki zoezi la kuomba green card,fursa ambayo iko wazi kwa watu mbalimbali duniani kuishi na kufanya kazi nchini Marekani, ambapo alifanikiwa kupata fursa hiyo na ndipo aliamua kubaki nchini humo na kuishi nchini miaka zaidi ya 16 mpaka kifo chake.

Kwa ufupi hayo ndiyo maisha ya Raymond hapa duniani.Mbele yake nasisi zamu yetu inakuja.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa.

Ameen

Imeandikwa na 

Benjamin Andongolile Thompson Mwakaleja,
Mpwa wake na Marehemu,
Dar es Salaam,
Tanzania





 

KILIMANJARO Marathon Company Limited imeelezea kuhuzunishwa kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa mbio maarufu ya Kilimanjaro International Marathon, Bwana John Bayo ambaye alifariki Jumanne asubuhi Jijini Arusha.

Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa Kilimanjaro International Marathon imemuelezea marehemu Bayo kama mtu mwema na moja ya mihimili mikuu ya Kilimanjaro Marathon ambayo ni mbio kubwa kuliko zote Tanzania.

KMCL, kupitia taarifa hiyo imetuma salamu za rambirambi kwa familia yake marehemu Bayo, ndugu, jamaa, marafiki na kwa wadau wote wa riadha ndani na nje ya Tanzania.

“Mtu mwema kiasi hiki anapofariki, inakuwa vigumu sana kuzungumza kwani tumepoteza muhimili mkubwa mno katika Kilimanjaro Marathon na rafiki wa kipekee,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa waandaaji hao, Bw. Bayo alikuwa mmoja wa waanzilishi wa mbio hiyo ya Kilimanjaro Marathon mwaka 2003 ambapo washiriki wasiozidi 500 walikimbia mbio za kujifurahisha tu lakini zaidi ya miaka 20 baadaye, mbio hiyo sasa inawavutia zaidi ya washiriki 12,000 kutoka nchi zaidi ya 55 duniani.

Bayo alikuwa mchapa kazi hodari ambaye alitumia ujuzi wake wote na uzoefu katika Kilimanjaro Marathon hadi umauti unamchukua.

“Alishirikiana pia na waandaaji wa mbio nyingine nchini Tanzania na kuwafundisha namna ya kuandaa mbio kwa weledi,” walisema waandaaji hao.

Waandaaji hao waliendelea kusema kuwa Bw. Bayo, katika uhai wake aliwahimiza wakimbiaji wengi wa kitanzania kushiriki katika mbio mbalimbali nje ya nchi.

“Kwetu sisi alikuwa kama ndugu, mstaarabu na hodari katika kazi yake ambayo aliifanya kwa weledi mkubwa, tutamkumbuka mno,” walisema.
In loving memory of the late

MOSES TITO KACHIMA

27th January 1945 - 29th January 2013

Every anniversary reminds us of the great memories created. We remind ourselves of the good moments we have had, the wisdom and lessons you have shared with us. It’s been ten years now but the memories live on.

We are grateful for the moments of your presence. We celebrate you and the life you have lived. We know you are in a better place, watching over us and your spirit lives on.

Eternal rest grant to him, O lord and let perpetual light shine upon him, May he rest in peace.
Amen

 

Taarifa ya familia imeeleza kuwa Marehenu Balozi Lweno amefariki leo alfajiri Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu na mazishi yatafanyika leo saa kumi Alaasiri.


Balozi Shani Lweno alisoma Shule ya Tabora Boys miaka ya 1960 na baadaye kuhitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka  1971 na mwaka huo huo aliajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje   kama Afisa Ubalozi Conakry - Guinea. Baada ya hapo alifanya kazi katika Balozi za Tanzania Cairo -  Misri, Khartoum -  Sudan, Stockholm - Sweden,  New York - Marekani na Addis Ababa - Ethiopia kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje. Mnamo mwaka 1993 aliteuliwa kuwa Balozi wetu Lusaka, Zambia mpaka alipostaafu  mwaka 2003.

Baada ya kustaafu Alijiunga na timu ya Kitengo cha Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika  iliyokuwa inasimamia Suala la Uhuru wa Sahara Magharibi.  Baada ya mkataba wake kumalizika alirejea nyumbani.  Balozi Lweno ameacha mke na watoto. 

Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin