Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Duh!Najaribu kujenga taswira nyingi kichwani kwangu ila bado nashindwa kukamilisha safari hii ya fikra.Bongo sasa kuna ngamia?Au macho yangu ndio yashaanza kunitupa mkono?
ReplyDeleteNg'ombe na ngamia nao wanafaidi matunda ya demokrasia. Ni lazima wafaidi upepo wa bahari! Michuzi bwana hizi picha umeziunganisha kinamna.
ReplyDeleteUnanifanya nicheke saa saba za usiku!
ReplyDeleteKaka una jicho zuri.
Nafikiri Idya amesema kweli. hizi picha zimeunganishwa. mbona hakuna nyayo upande wanyama hawa waliotokea, na kivuli cha mtoto aliyepiga magoti kiko wapi? wacha dhaka michuzi bwana.
ReplyDeletehiii picha ni nzuri sana ni wewe kweli muhusika? kama ndi basi umebobea.
ReplyDeleteNingekuwa na hasira nisingepost tena picha kwa mtindio wenu wa imani, hasa we Ida Nkya. sijawahi kuchezea picha na sina mpango huo mbeleni.ujapo dar tembelea kigamboni, hususan south beach, ambako maajabu haya yapo. naweza sema ilikuwa ni bahati pamoja na 'jicho' la picha ndivyo viliniwezesha kubamna taswira hii inayoonekana kama ya kuunganisha. kwanza niunganishe picha ili nipate nini ambacho sina. wee Ida Nkya, ntakuchaaaapa..
ReplyDeleteMichuzi hii picha nimeipenda mno, kazi safi sana ndugu, si rahisi kupiga picha itokee vizuri hivi hata kama kamera ni nzuri hiki ni kipaji kaka. kingine kilichinifurahisha zaidi ni picha ya bahari napenda sana bahari yaani moyo wangu umepoa sana kuona picha hii.
ReplyDeleteNdiyo nimewahi kuona ng'ombe wakifaidi upepo wa baharini pale kigamboni. Michuzi unanikumbusha enzi zako za upigaji wa picha kwenye daily news na sundaynews. Kweli ujuzi huuzeeki.
ReplyDelete@Michuzi: usimtandike Nkya. Ukiona picha zako zinaleta mzozo na majadiliano ujue kuwa kazi yako inaheshimiwa. Mimi naona panapotokea hisia kama hizi (kuwa labda picha imechezwa) mambo ndio yameiva.
ReplyDeletePicha hii niliitazama kwa muda mrefu sana. Niliamua kuiweka katika muhtasari nilioandika katika blogu ya mradi wa Sauti za Dunia. Unaweza kuona muhtasari huo hapa:
http://cyber.law.harvard.edu/globalvoices/2005/11/24/kiswahili-blogosphere-this-week-3/
Hawa Ng'ombe na Ngamia wanafanya nini kwenye maji chumvi,wale Ngamia kule nyuma wanachungwa na Nani,Huyu mtoto hapa mbele haogopi kukanyagwa na hawa wanyama.....!!! hii pic kali.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteNaona kwa kuwa watu wamekatazwa kuchunga mifugo katika vyanzo vya maji Kule Mtera wameamua kurambaza na mifugo baharini. Inawezekana wanyama hao waka fall in love na maji chumvi. Kwahiyo jamaa anawapitisha ili warambe rambe maji chumvi.