Hii ndo Bongo ya sasa! Comments please...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Duh!Najaribu kujenga taswira nyingi kichwani kwangu ila bado nashindwa kukamilisha safari hii ya fikra.Bongo sasa kuna ngamia?Au macho yangu ndio yashaanza kunitupa mkono?

    ReplyDelete
  2. Ng'ombe na ngamia nao wanafaidi matunda ya demokrasia. Ni lazima wafaidi upepo wa bahari! Michuzi bwana hizi picha umeziunganisha kinamna.

    ReplyDelete
  3. Unanifanya nicheke saa saba za usiku!
    Kaka una jicho zuri.

    ReplyDelete
  4. Nafikiri Idya amesema kweli. hizi picha zimeunganishwa. mbona hakuna nyayo upande wanyama hawa waliotokea, na kivuli cha mtoto aliyepiga magoti kiko wapi? wacha dhaka michuzi bwana.

    ReplyDelete
  5. hiii picha ni nzuri sana ni wewe kweli muhusika? kama ndi basi umebobea.

    ReplyDelete
  6. Ningekuwa na hasira nisingepost tena picha kwa mtindio wenu wa imani, hasa we Ida Nkya. sijawahi kuchezea picha na sina mpango huo mbeleni.ujapo dar tembelea kigamboni, hususan south beach, ambako maajabu haya yapo. naweza sema ilikuwa ni bahati pamoja na 'jicho' la picha ndivyo viliniwezesha kubamna taswira hii inayoonekana kama ya kuunganisha. kwanza niunganishe picha ili nipate nini ambacho sina. wee Ida Nkya, ntakuchaaaapa..

    ReplyDelete
  7. Michuzi hii picha nimeipenda mno, kazi safi sana ndugu, si rahisi kupiga picha itokee vizuri hivi hata kama kamera ni nzuri hiki ni kipaji kaka. kingine kilichinifurahisha zaidi ni picha ya bahari napenda sana bahari yaani moyo wangu umepoa sana kuona picha hii.

    ReplyDelete
  8. Ndiyo nimewahi kuona ng'ombe wakifaidi upepo wa baharini pale kigamboni. Michuzi unanikumbusha enzi zako za upigaji wa picha kwenye daily news na sundaynews. Kweli ujuzi huuzeeki.

    ReplyDelete
  9. @Michuzi: usimtandike Nkya. Ukiona picha zako zinaleta mzozo na majadiliano ujue kuwa kazi yako inaheshimiwa. Mimi naona panapotokea hisia kama hizi (kuwa labda picha imechezwa) mambo ndio yameiva.

    Picha hii niliitazama kwa muda mrefu sana. Niliamua kuiweka katika muhtasari nilioandika katika blogu ya mradi wa Sauti za Dunia. Unaweza kuona muhtasari huo hapa:

    http://cyber.law.harvard.edu/globalvoices/2005/11/24/kiswahili-blogosphere-this-week-3/

    ReplyDelete
  10. Hawa Ng'ombe na Ngamia wanafanya nini kwenye maji chumvi,wale Ngamia kule nyuma wanachungwa na Nani,Huyu mtoto hapa mbele haogopi kukanyagwa na hawa wanyama.....!!! hii pic kali.

    ReplyDelete
  11. Michuzi,

    Naona kwa kuwa watu wamekatazwa kuchunga mifugo katika vyanzo vya maji Kule Mtera wameamua kurambaza na mifugo baharini. Inawezekana wanyama hao waka fall in love na maji chumvi. Kwahiyo jamaa anawapitisha ili warambe rambe maji chumvi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...