mzee rashidi mfaume kawawa na mkewe. kama julius nyerere tulimwita baba wa taifa je simba wa vita huyu ambaye amefaifanyia makubwa tanzania tumwiteje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mbona simba wa vita ni jina zito tu??? mengine tuwabakizie na wazee wetu pia walifanya mengi sema hawakuwa waroho wa madaraka!!!

    ReplyDelete
  2. Baba yake Freeman mbowe sijui kwanini hatajwi?????????!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Mzee Kawawa ni "Baba Mdogo wa Taifa" :)
    -Mzee Mbegu

    ReplyDelete
  4. Lakini hizi fikra Bw. Michuzi kwa nini unazifikisha hapa kwa sababu iwapo tutataka kunasibisha majina ya waasisi na kuhusiisha na nasabu za wananchi itakuwa tunaikosea jamii, basi kama ni hivyo basi wale wazee wetu wa enzi zile akina Kinjeketile,Zongendaba, Mkwawa,Mirambo, Mangi Meri na wengine wengi kwa nini tusiwape heshima ya utukuzo kama aliyopewa Mwalimu mimi nadhani mawazo haya hayana nafasi kwa sasa, tuwape heshima zao kulingana na yale waliyoyatenda wakiwa viongozi wa nchi yetu.

    Mimi naamini kwa busara za Mwalimu hili jina la kuitwa Baba wa Taifa iwapo Mungu angempa uhai hadi sasa angelikataa, kuna haja ya kusoma ishara ya nyakati, wakati tulionao si ule wa zama zile za UJIMA na ujamaa na kujitegemea na Azimio la Arusha na watu kujitokeza kukimbiza Mwenge unaogharimu mafuta na fedha nyingi kwa watu kuukimbiza nchi nzima ilhali kuna baadhi ya wananchi wanakufa njaa na wengine wanakosa dawa za matibabu huku watoto wakishindwa kulipa ada za shule, kuna umuhimu wa kubadilika katika zama hizi tulizo nazo dunia hairudi nyuma bali tunaenda mbele, tuangalie wanetui wasije kupiga viboko makaburi yetu kwa uamuzi ambao tunmaweza kuupitisha na kuleta athari hapo baadaye.

    Unajua Bw.Makongoro, Rosemary akina MADARAKA na watoto wengine wa Mwalimu wanaweza kujifaharisha kujiona wao ndio watoto bora wa Taifa hili, sasa tunataka kumfanya BW. Vita Kawawa naye aanze kujiona kwamba yeye naye..... hapana Bw. Michuzi hii mada naona haina mantiki kwa zama hizi sijui wengine maoni yao yakoje

    WAKATABAHU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...