Home
Unlabelled
kusikiliza wazee
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
michuzi unampamba sana JK,inamaana huyu hakuna upande mwingine wa shilingi? Rais JK akosolewi hata siku moja kaa sadam enzi zake!
ReplyDeletekama hakuna cha kukosoa nitie umbea? acha unaa mjomba! halafu sidhani kama ni dhambi kufagilia mtu kama ambavyo si dhambi watu kama nyie kuachwa kama mlivyo, kwani si lazima kila wazo langu (au lako) likubalike nawe (nami). what's good for the goose, is bad for the hen. sina kawaida kujibu pumba ila nahisi kuna watu wananitafuta ubaya. utadhani nawalazimisha kufungua blog hili. hapo ni dezo, je mngekuwa mnalipa ingekuwaje. mark, semkae, ndesanjo, idya (ida?), baragumu, jeff na wengineo naomba ulinzi!!!!
ReplyDeletemichuzi usije juu baba!ukiona watu wanakukosoa ujue lipo jambo. Maendeleo hayaji bali kwa kukosoana.
ReplyDeleteMichuzi tunakushukuru kwa kutuwekea picha za nyumbani na viongozi wetu. Keep up the good work. Mimi nafungua hii blog kila siku, hakuna ubaya wowote wa wananchi kupenda viongozi wao.
ReplyDeleteMichuzi najua unatetea unga pale Daily Noise. Si haba waweza kuwa Information officer ubalozini siku moja. Hata ikiwa hivyo ni haki yako. It's time nao wakatambua kazi yako.
ReplyDeleteTunaogopa kutaja majina kwani u-mkali kukosolewa. Kwani wewe Malaika?
UNAPROVOKE NINI BWANA MICHUZI!
ReplyDeletewe ni journalist,utakiwi kuwa bias bwana,kuwa kama wenzako wa huku ughaibuni (tena umefika ukaona mwenyewe), angalia soon mtaanza kumuimba JK kwenye radio kama MOI enzi zake. Rais anaweza pasuka kichwa halloo.!
wakongwe kama nyie ndio mnatakiwa kuwa wachambuzi wa mambo,both sides of our President.
usiogope,ukifungwa tutaandamana.
umeweka site hewani, ni mali yetu sasa sio ya kwako tena, wala sio lazima niweke picha kama bwana semkae,ndesanjo ndio nikulinde.
more challege to come!!
Kwani Ndugu wewe ulitaka Michuzi aseme nini?? inawezekana una wazo bora,, upeo wako si sawa na upeo wangu au wa Michuzi, kama wewe unalo la kukosoa nadhani ungesema tu.
ReplyDeleteWazee wakimpatia wasaa kijana JK baada ya kuchukua jukumu la kutuswaga wabongo kama ng'ombe kutoka Dodoma yaani hamna hata tofauti Njaa, Ukame , Upungufu wa dawa sasa tunatofauti gani na kitoweo kile
ReplyDeleteHahahahahaaaaaa! kumbe mnamaindi kuprovokiwa! hahahaha!!!!!! jamani mi nilikuwa natania tu. sina kinyongo na mtu anayenikosoa. nilitaka nione mtawaka vipi. nafurahi wengi mko upande wangu.endeleeni kusifia na kuponda. simaindi kabisa. i accept it as 'occupational challnge' kama nimepatia ung'enge'. ila saa ingine mtu huukati mkono unaokulisha
ReplyDeletemichuziiiiii ulinzi guaranteed!! naona pia hawa watu pia hawajajua style zako za kuchokoza mada kama aliivyokugundua bwana majaliwa nadhani pale kwenye ishu ya wazee wa ulinzi na usalama!!!! teh teh teh!! - lakini ndio uandishi huo kama ubunge...samuel 6 kadai siku nyingine makofi nyingine ......
ReplyDeleteWanapotokea watu wakakukosoa Michuzi, mimi nafurahi sana. kwanini? Kwanza inaonyesha kuwa wanachukulia unayosema kwa makini. La sivyo usingekosolewa au kuungwa mkono. Pili, inaonyesha kuwa blogu yako sio chombo cha habari ya mstari mmoja: yaani wewe kutupa picha tu na maoni yako. Bali ni chombo cha majadiliano. Unasema jambo, wasomaji wako nao wanapata nafasi ya kujibu. Hii ndio tofauti na magazeti ya kuuzwa mtaani ambapo hupati nafasi ya kujibizana hoja kwa hoja na wasomaji wako. Wakitazama picha yako gazetini wakaipenda, wakawa na swali, wakataka picha fulani, n.k., kwa teknolojia ya magazeti ya kuuzwa mtaani inakuwa vigumu sana kuwasiliana nawe. Kushiriki kwenye majadiliano na gumzo na mpiga picha wao.
ReplyDeleteNirudi kwa Kikwete na wazee. Mwinyi naye alipoingia madarakani alikuwa na tabia ya kukutana na wazee. Sijui ni lini marais watakuwa wanakutana na vijana, watoto, wanawake, wanafunzi, walemavu, n.k.
Kukutana huku ni moja ya mbinu zinazotumiwa mara nyingi na watwawala pendwa. Unakumbuka Mrema alikuwa akikutana na akina mama ofisini kwake wakimweleza siri za ndoa zao. Naye alikuwa waziri pendwa.
Ninachosema: Michuzi endelea na kazi. Wanaokuunga mkono waendelee, wanaokukosoa waendelee, wasio na upande waendelee hivyo hivyo...hii ni alama mojawapo ya ujenzi wa demokrasia. Yote ni sawa na sahihi. Tena wakati mwingine ni vyema zaidi kusikia wanaokupinga zaidi ya wanaokuunga mkono. Lakini pia ni vyema kusikia wote. Majuzi niliandika kwenye blogu yangu nikasema kuwa teknolojia ya blogu inafanya nyanja ya habari kuwa sio nyanja ya kutoa habari bali pia eneo la majadiliano.
ni kweli kaka Ndesanjo. umeongea kitu kimoja kizuri sana. kuna haja sasa raisi anapokutana na wananchi kuwe na uwakilishi wa makundi yote.kimsingi kila kundi lina matatizo yake. mfano kwa wazee wanazungumzia pensheni wakati vijana na kina mama ni ajira uchumi na kujenga taifa....
ReplyDeletenaunga mkono pia blogu ni kiwanja cha kujifunza kupingwa. hii itatusaidia kutengenezsa taifa la watu wanaoweza kupingana / kushindana bila kupigana / kuhamaki!! isije ikafika wakati tukarudia kupata raisi anayeunga mfumo wa serekali yake iliyooza au kuficha maovu ya watendaji wake!
Ndesanjo na Msaki 'asavali' mmenisemea niliyokuwa nayo moyoni (ingawaje labda nisingeweza kuyasema kwa ufundi mkubwa mlionao). Nilikuwa naogopa kusema maana Michuzi kwa kucharuka, unawezasahau kuwa uko naye mbali na kudhani yuko mgongoni kwako tayari kukubamiza rungu!
ReplyDeleteNdugu yangu Michuzi mimi napongeza sana juhudi za kazi yako na endelea na moyo huo wa kujitolea lakini ndugu yangu angalia sana siasa kwani ni mchezo mchafu leo hii unafanya kazi yao na wanakupenda kesho waweza kuwa matatani kama mwandishi na mpiga picha mimi ni mwanafunzi wa Marehemu Joe Masanyilo yule baba wakati ananifundisha kazi miaka 15 iliyopita aliniambia mengi juu ya kazi yangu itikadi ya chama na kunionya juu ya yale yanayoweza nifika na kunipa mifano ya akina Grey likungu Mataka sikutishi lakini nenda nao taratibu hao wanasiasa maana siku zote wanataka kusikia mazuri tuu
ReplyDelete