TX Moshi William wa msondo ngoma katutoka leo saa tatu kasorobo asubuhi katika wodi ya sew haji hospitali ya taifa ya muhimbili baada ya kuuguza mguu aliouvunjika ajalini februari 2005, na alipojaribu kuondoa mchuma aliowekewa siku ya wapendanao mwaka huu akaanza kuugua. hakupona tena hadi leo asubuhi alipotutoka. ameacha mke na watoto wanne, mjukuu mmoja na albamu 13 zenye nyimbo zake kibao, ikiwa na zile zilizompa tuzo za utunzi bora mara tatu mfululizo toka 2003, 2004 na 2005. mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amina!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Mara ya mwisho nilimuona ukumbi wa Mkapa Mbeya mwezi wa sita mara baada ya kutoka hospitali. Alikuwa akipafomu huku amekaa kwenye kiti. Watu walitokwa na machozi kumuona katika hali hiyo. Kumbe alikuwa njiani kuelekea kunako jicho la haki.

    Leo nitasikiliza nyimbo zake tu.

    Mungu aiweke roho yake mahali pema pepono amina.

    ReplyDelete
  2. Tumesikitishwa sana na hii habari ya Kifo chake. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amina.

    Pole kwa familia yake, Jamii yake, Wapenzi wa Miziki yake, pamoja na jamaa na marafiki zake.

    Tumshukuru Mungu kwa Yote,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  3. Oh Israel mtoa roho kafanya vitu vyake.Mungu amrehemu sana.Ndio maisha,kuzaliwa na kufa.
    Nitaimisi sauti yake sana.Naenda kulala na itanibidi nisikilize kaseti nzima nimkumbike.

    ReplyDelete
  4. Wallah kifo cha huyu Bwn kimenigusa.. Duu wala siamini. Mungu aiweke roho yake mahali pema Mbinguni

    ReplyDelete
  5. Inasikitisha sana, kuanzia familia yake na hata kwa sisi wapenzi wa muziki wa dansi. Hata ushindani kati ya Msondo na Sikinde utapwaya sana.
    Mungu amlaze mahali pema shujaa huyu katika muziki Tanzania.

    ReplyDelete
  6. mungu iweke pema peponi roho ya shujamaa huyu.

    ReplyDelete
  7. Moshi William ni mmoja wa wasanii wetu ambao taifa halikuweza kutambua mchango wao wakati wakiwa hai. Pole ziendee familia yake. Nami kama Mwaipopo nikiweka kituo hapa ninaendea kaseti yake.

    Kama kuna mtu mwenye historia yake anaweza kusaidia kuandika kwenye kamusi elezo kama njia ya kumuenzi. Nimeanzisha ukurasa wake tayari.
    Uko hapa: http://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi_William

    ReplyDelete
  8. huzuni huzuni ulioje inauma, inashitusha.

    BASI APANGALO MUNGU MWANADAMU HAWEZI KUPANGUA..

    TUNAMUOMBA MUNGU ATUEPUSHIE ADHABU ZA DUNIA NA ZA KABURINI PIA.

    WEWE MBELE SISI NYUMA.

    E MWENYEZI IPOKEE NAFSI YA MWENZETU
    TUSAMEHE NA MAZAMBI YETU.

    ReplyDelete
  9. Mwenyezi Mungu hana makosa lakini hapa katupiga wazee wa rumba mzito

    ReplyDelete
  10. Kullu nasfin dhaaikatul maut.
    Mungu amuweke pema.

    ReplyDelete
  11. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lkiimidiwe.
    Londo

    ReplyDelete
  12. Mungu amulaze mahali pema peponi.Amina

    ReplyDelete
  13. Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi,amina. Isaac Mgwassa

    ReplyDelete
  14. Michuzi, nimetumia hii picha kwenye ukurasa wa Moshi William wa kwenye kamusi elezo huria ya Kiswahili. Naamini hatuhitaji kukulipa!! Mwenye lolote juu yake, kwa mfano kuna mtu kaandika jina lake halisi (shukrani uliyefanya hivyo), tafadhali asisite kujazia kwenye ukurasa wake kwa kubonyeza pale juu panaposema "hariri."
    Itazame hapa:
    http://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi_William

    ReplyDelete
  15. ndesanjo nimekupata, nimekusoma, usiwe na hofu. wewe una ruksa kutumia chochote humu bloguni bila malipo.

    ReplyDelete
  16. Du tumempoteza Mzee wa Kimanzichana, lakini mapenzi ya Mola tuombe matumbo ya akina mama wa Afrika yazidi kutoa vizazi kama yeye, Amin - Mpambalioto

    ReplyDelete
  17. Hili ndugu zangu ni pengo kubwa katika muziki wa dansi.Nadhani kifo chake kimemshtua kila mpenzi wa muziki wa aina yoyote Tanzania. Hakika Moshi tutamkumbuka kwa mema daima milelee
    Nadhani wanamuziki wa Tanzania waige mfano wa huyu bwana ili nao tuwaenzi kama tutakavyomuenzi Marehemu Moshi william.Mungu ailaze marehemu mahali pema peponi.AMEN

    ReplyDelete
  18. Kifo cha TX kweli ni pigo kwa Msondo, wapenzi wake na wapenzi wote wa muziki TZ. Kikubwa pia tujiulize ni nini kilichoisibu Msondo hadi kupoteza wanamuziki wake mahiri watatu (TX, Mbwembwe na Momba) katika kipindi cha takribani mwaka mmoja?

    ReplyDelete
  19. tujiulize kitu gani hiyo ni mipango ya mungu mwanadamu utauliza nini zaidi ya kukaa kimya na kushukuu.

    ReplyDelete
  20. Sikuju Moshi William anagusa watu wengi namna hii. Kumbe alikuwa lulu ya Taifa. Mungu ailaze mahali pema peponi. Lakini wengi wanahusisha kifo chake na kujichubua ngozi. Hilo laweza kuwa funzo kwetu sote.

    ReplyDelete
  21. kujichubua kuna husika vipi na wewe kama sio bwege.
    kila mtu anapenda hawe anavyotaka yeye , chagua lake, liheshimie.
    tena omba radhi kwa wapenzi wote wa muziki.neno chafu sana umetoa.
    wewe utakufa mdomo wazi.

    ReplyDelete
  22. We Reginald kumbe zuzu unawezaje kusema maneno kama haya unahaya ujui vibaya hujui wapi pakusema nini,

    mdomo wako ni kama mtu aliyeshikwa na uharisho hwezi kujizuia ana hara hovyo.

    unamdomo mchafu sana.

    tena mpuuzi mkubwa umechafua roho za watu.

    unaweza kumuongelea mtu aliyekufa maneno machafu.

    tutafunga mungu asituchukue mpaka tuone na wewe utakufa vipi???

    Mungu atakuchukua kifo cha gesti huku ukiliwa na wajanja hayo matako yako.

    ReplyDelete
  23. Jamani, kama Miruko amekosea kwanini asielezwe kwa adabu? Kama ametumia maneno machafu, hakuna haja ya kutumia maneno machafu kumshauri au kumweleza makosa yake.

    ReplyDelete
  24. aha anatakiwa aelewe utamu wa uchafu wa maneno kama yeye ndo angeambiwa angejisikiaje au mtu wake wa karibu,

    ajifunze kuna vitu unaweza ukawaambia watu walio hai ambao wanaweza kujitetea mtu asieweza kujitetea unamtukania nini?

    aelezwe na nani?

    kama anatukana na yeye atatukanwa tuu.

    wala asitetewe.

    ReplyDelete
  25. untukana wafu na walio hai unawafanyaje?

    mungu akushushie laana zake, tx kakusea nini? kujichubua kwakwe kunakunyima nini?

    utakufa, uoze na watu wasikugundue ulipo mpaka unuke.

    inshaallah.

    ReplyDelete
  26. Kama kutukana ni kosa, kumtukana aliyetukana inakuwa sio kosa? Kwanini ufanye kosa ili ili kuonyesha makosa ya mwingine? Kama kutukana ni kosa, basi iwe umetukana aliye hai au aliyefariki, yote ni kosa.

    ReplyDelete
  27. mungu ailaza roho yako mahala pema peponi. amina.

    ReplyDelete
  28. kaka ndesanjo wewe muungwana sana na mstaarabu mno nakupenda sana na nitazidi kukupenda.

    kijana mdogo,
    mwenye kipaji,
    cha kupambana na vichaa pamoja na wazima,
    uzidi kubarikiwa mpenzi wetu.

    ReplyDelete
  29. nilikupenda sana tx ktk uimbaji wako.

    ReplyDelete
  30. msondo ilianza kunikatisha tamaa alipooondoka mbwembwe mmoja wa sauti nilizokuwa nasikia tangu niko shule ya msingi miaka ya themanini!!!msondo ilikuja kuchukua mapenzi yangu yote ilipofika miaka hii ya 2000 kweli bendi imefanya mambo makubwa sana nilianza kuipenda zaidi na zaidi,si muda mrefu akaondoka mwingine maina kam sikosei hapo ndipo nilipoanza kuona sasaa msondo inaisha nikawa naomba MUNGU awape maisha waliobaki sasa kuondoka kwa Tx nimeumia kwa kipimo nisichoweza elezea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...