
TX Moshi William wa msondo ngoma katutoka leo saa tatu kasorobo asubuhi katika wodi ya sew haji hospitali ya taifa ya muhimbili baada ya kuuguza mguu aliouvunjika ajalini februari 2005, na alipojaribu kuondoa mchuma aliowekewa siku ya wapendanao mwaka huu akaanza kuugua. hakupona tena hadi leo asubuhi alipotutoka. ameacha mke na watoto wanne, mjukuu mmoja na albamu 13 zenye nyimbo zake kibao, ikiwa na zile zilizompa tuzo za utunzi bora mara tatu mfululizo toka 2003, 2004 na 2005. mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amina!


Mara ya mwisho nilimuona ukumbi wa Mkapa Mbeya mwezi wa sita mara baada ya kutoka hospitali. Alikuwa akipafomu huku amekaa kwenye kiti. Watu walitokwa na machozi kumuona katika hali hiyo. Kumbe alikuwa njiani kuelekea kunako jicho la haki.
ReplyDeleteLeo nitasikiliza nyimbo zake tu.
Mungu aiweke roho yake mahali pema pepono amina.
Tumesikitishwa sana na hii habari ya Kifo chake. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amina.
ReplyDeletePole kwa familia yake, Jamii yake, Wapenzi wa Miziki yake, pamoja na jamaa na marafiki zake.
Tumshukuru Mungu kwa Yote,
©2006 MK
Oh Israel mtoa roho kafanya vitu vyake.Mungu amrehemu sana.Ndio maisha,kuzaliwa na kufa.
ReplyDeleteNitaimisi sauti yake sana.Naenda kulala na itanibidi nisikilize kaseti nzima nimkumbike.
Wallah kifo cha huyu Bwn kimenigusa.. Duu wala siamini. Mungu aiweke roho yake mahali pema Mbinguni
ReplyDeleteInasikitisha sana, kuanzia familia yake na hata kwa sisi wapenzi wa muziki wa dansi. Hata ushindani kati ya Msondo na Sikinde utapwaya sana.
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema shujaa huyu katika muziki Tanzania.
mungu iweke pema peponi roho ya shujamaa huyu.
ReplyDeleteMoshi William ni mmoja wa wasanii wetu ambao taifa halikuweza kutambua mchango wao wakati wakiwa hai. Pole ziendee familia yake. Nami kama Mwaipopo nikiweka kituo hapa ninaendea kaseti yake.
ReplyDeleteKama kuna mtu mwenye historia yake anaweza kusaidia kuandika kwenye kamusi elezo kama njia ya kumuenzi. Nimeanzisha ukurasa wake tayari.
Uko hapa: http://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi_William
huzuni huzuni ulioje inauma, inashitusha.
ReplyDeleteBASI APANGALO MUNGU MWANADAMU HAWEZI KUPANGUA..
TUNAMUOMBA MUNGU ATUEPUSHIE ADHABU ZA DUNIA NA ZA KABURINI PIA.
WEWE MBELE SISI NYUMA.
E MWENYEZI IPOKEE NAFSI YA MWENZETU
TUSAMEHE NA MAZAMBI YETU.
Mwenyezi Mungu hana makosa lakini hapa katupiga wazee wa rumba mzito
ReplyDeleteKullu nasfin dhaaikatul maut.
ReplyDeleteMungu amuweke pema.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lkiimidiwe.
ReplyDeleteLondo
Mungu amulaze mahali pema peponi.Amina
ReplyDeleteMwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi,amina. Isaac Mgwassa
ReplyDeleteMichuzi, nimetumia hii picha kwenye ukurasa wa Moshi William wa kwenye kamusi elezo huria ya Kiswahili. Naamini hatuhitaji kukulipa!! Mwenye lolote juu yake, kwa mfano kuna mtu kaandika jina lake halisi (shukrani uliyefanya hivyo), tafadhali asisite kujazia kwenye ukurasa wake kwa kubonyeza pale juu panaposema "hariri."
ReplyDeleteItazame hapa:
http://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi_William
ndesanjo nimekupata, nimekusoma, usiwe na hofu. wewe una ruksa kutumia chochote humu bloguni bila malipo.
ReplyDeleteDu tumempoteza Mzee wa Kimanzichana, lakini mapenzi ya Mola tuombe matumbo ya akina mama wa Afrika yazidi kutoa vizazi kama yeye, Amin - Mpambalioto
ReplyDeleteHili ndugu zangu ni pengo kubwa katika muziki wa dansi.Nadhani kifo chake kimemshtua kila mpenzi wa muziki wa aina yoyote Tanzania. Hakika Moshi tutamkumbuka kwa mema daima milelee
ReplyDeleteNadhani wanamuziki wa Tanzania waige mfano wa huyu bwana ili nao tuwaenzi kama tutakavyomuenzi Marehemu Moshi william.Mungu ailaze marehemu mahali pema peponi.AMEN
Kifo cha TX kweli ni pigo kwa Msondo, wapenzi wake na wapenzi wote wa muziki TZ. Kikubwa pia tujiulize ni nini kilichoisibu Msondo hadi kupoteza wanamuziki wake mahiri watatu (TX, Mbwembwe na Momba) katika kipindi cha takribani mwaka mmoja?
ReplyDeletetujiulize kitu gani hiyo ni mipango ya mungu mwanadamu utauliza nini zaidi ya kukaa kimya na kushukuu.
ReplyDeleteSikuju Moshi William anagusa watu wengi namna hii. Kumbe alikuwa lulu ya Taifa. Mungu ailaze mahali pema peponi. Lakini wengi wanahusisha kifo chake na kujichubua ngozi. Hilo laweza kuwa funzo kwetu sote.
ReplyDeletekujichubua kuna husika vipi na wewe kama sio bwege.
ReplyDeletekila mtu anapenda hawe anavyotaka yeye , chagua lake, liheshimie.
tena omba radhi kwa wapenzi wote wa muziki.neno chafu sana umetoa.
wewe utakufa mdomo wazi.
We Reginald kumbe zuzu unawezaje kusema maneno kama haya unahaya ujui vibaya hujui wapi pakusema nini,
ReplyDeletemdomo wako ni kama mtu aliyeshikwa na uharisho hwezi kujizuia ana hara hovyo.
unamdomo mchafu sana.
tena mpuuzi mkubwa umechafua roho za watu.
unaweza kumuongelea mtu aliyekufa maneno machafu.
tutafunga mungu asituchukue mpaka tuone na wewe utakufa vipi???
Mungu atakuchukua kifo cha gesti huku ukiliwa na wajanja hayo matako yako.
Jamani, kama Miruko amekosea kwanini asielezwe kwa adabu? Kama ametumia maneno machafu, hakuna haja ya kutumia maneno machafu kumshauri au kumweleza makosa yake.
ReplyDeleteaha anatakiwa aelewe utamu wa uchafu wa maneno kama yeye ndo angeambiwa angejisikiaje au mtu wake wa karibu,
ReplyDeleteajifunze kuna vitu unaweza ukawaambia watu walio hai ambao wanaweza kujitetea mtu asieweza kujitetea unamtukania nini?
aelezwe na nani?
kama anatukana na yeye atatukanwa tuu.
wala asitetewe.
untukana wafu na walio hai unawafanyaje?
ReplyDeletemungu akushushie laana zake, tx kakusea nini? kujichubua kwakwe kunakunyima nini?
utakufa, uoze na watu wasikugundue ulipo mpaka unuke.
inshaallah.
Kama kutukana ni kosa, kumtukana aliyetukana inakuwa sio kosa? Kwanini ufanye kosa ili ili kuonyesha makosa ya mwingine? Kama kutukana ni kosa, basi iwe umetukana aliye hai au aliyefariki, yote ni kosa.
ReplyDeletemungu ailaza roho yako mahala pema peponi. amina.
ReplyDeletekaka ndesanjo wewe muungwana sana na mstaarabu mno nakupenda sana na nitazidi kukupenda.
ReplyDeletekijana mdogo,
mwenye kipaji,
cha kupambana na vichaa pamoja na wazima,
uzidi kubarikiwa mpenzi wetu.
nilikupenda sana tx ktk uimbaji wako.
ReplyDeletemsondo ilianza kunikatisha tamaa alipooondoka mbwembwe mmoja wa sauti nilizokuwa nasikia tangu niko shule ya msingi miaka ya themanini!!!msondo ilikuja kuchukua mapenzi yangu yote ilipofika miaka hii ya 2000 kweli bendi imefanya mambo makubwa sana nilianza kuipenda zaidi na zaidi,si muda mrefu akaondoka mwingine maina kam sikosei hapo ndipo nilipoanza kuona sasaa msondo inaisha nikawa naomba MUNGU awape maisha waliobaki sasa kuondoka kwa Tx nimeumia kwa kipimo nisichoweza elezea.
ReplyDelete