kwa mlio ughaibuni longi taimu mjue ubalozi wa uingereza upo nyumba ya umoja pomoja na ofisi za dfid, eu na kadhalika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2006

    hilo jengo lipo mtaa gani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2006

    Lipo Garden Avenue, mkumbukage kurudi nyumbani mara moja moja. Hilo jengo lina zaidi ya miaka mitano toka likamilike

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2006

    Mzee Michuzi naona kwenye hili jengo, bendera ziko nusu mlingoti au ni macho yangu. Mzee ukipata nafasi utukumbushe na Manzese.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2006

    Aliye nacho huongezewa...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2006

    Viza wanatoa lakini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2006

    Anony wa 10:05Am tunapenda sana kurudi kwetu lakini wengine tulizamia kuja huku ina maana tukirudi ndio itakuwa basi tena. Wengine tumebanwa na Milungu hata hatukumbuki tena kwetu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2006

    aisee michuzi ondoa hii color ya pink. vitu vya aibu...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2006

    ni kweli hata mimi nilisema mwanzo ile rangi ya blach bomba sana. classic

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2006

    Bwn Michuzi kwanza hongera kwa kuifanyia hii blog fesi lift. Mpangilio wake sasa unaendana na hadhi yako Mheshimiwa michuzi.

    Rangi pia nzuri sana sema tu kwa wale walioko ughaibuni hii rangi inatafsiri sio nzuri sana kwani rangii hii mara nyingi hutumiwa na mashoga.

    kuna msemo usemao "it takes courage for a man to wear/use pink"

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2006

    Kwa wale mlio ughaibuni, hivi katika balozi mbali mbali bendara ya nchi mwenyeji huwa hazipeperushwi?

    Kwa hapa sijaona bendera ya Tanzania ndio maana nimeuliza hilo swali!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 22, 2006

    Nyumbani is getting better big time in the unbelievable rate growth. Hopefull we will be in that rate for while. "Mungu ibariki Tanzania".

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 22, 2006

    MICHUZI MPENZI NAOMBA UWEKE RANGI NYEUSI KAKA

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 22, 2006

    Katika Dunia hii sio rahisi kumridhisha kila binadamu. Mzee michuzi katika swala la backgound/ rangi hata uweke ipi lazima utapata malamiko. Mkumbuke kuna tofauti ya colour perception kati ya binadamu, kuna wengine hata hiyo rangi unayo iona wewe kuwa ni ya pink, mwingine anaweza kuiona kama light blue. Kuna kitu kinaitwa colour Blindness. Hivyo maoni yangu wewe stick kwenye hiyo ambayo utashauri na watu wako wakaribu kwamba iko bomba.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 22, 2006

    Ona sasa nyie mlioomba tubadilishiwe rangi ya pink.. mnaona sasa matokeo yake tunaletewa michanganyiko ya kizaire sasa. Kijani na crazy blue wapi na wapi?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 22, 2006

    We MK hebu rudisha pink bwana! mnatuletea rangi gani za zaramo?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 22, 2006

    Kama mmeshindwa bora mrudishe blogu kama ilivyokuwa mwanzo, maana tulikuwa hatujalalamika.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 22, 2006

    Apo poa acheni hii pink mtalizasha nani na kuacha nani.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 22, 2006

    We MK tuwekee rangi za kawaida bwn, hizo crazy colour zinachosha macho!!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 22, 2006

    Acheni rangi hii, Msije mkafanya makosa tena. Msisikilize watu wengine wana mawazo yao mara hivi mara vile basi zogo tupu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 22, 2006

    Wee Grill rudi kusalimia wazee homu. Wenzako kila mwaka tunaenda. Eboooo!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 22, 2006

    Rangi ya Pink ina maana tofauti hasa Marekani na Uingereza. Lakini kwa Tanzania haina ubaya, ingawa kwa upande wangu ningeweka rangi tofauti, pengine rangi ya Olive (darker).

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 22, 2006

    Upande wako kwani blogu yako? ACheni kujishaua kawa ambieni ipp au cnn au web yoyote kama wata wasikiliza.fungueni zenu na mlete sheria mbuzi.kila mtu ana maamuzi yake. washamba nyie.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 22, 2006

    Watu wengine acheni unoko. Kama rangi ina waumiza macho mnaweza kupunguza brightness kwenye screen zenu za compyuter. Kwani unavyo surf kwenye sites nyingine unaangalia yanye rangi unayopendelea? Acnana na hawa wanoko mzee michuzi, songambelee lete maviruzi.............

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 22, 2006

    wapakeni haoooooooooooooo kila siku tunawaona na tuna wajua wamezidi kwa sana tu mara vile mara hivi mara macho sijui nini kwani nyie ndo nani. fungueni zenu na mlete sheria mbovu. kila mtu ana penda anacho taka na brogu sio yenu fungeni domo. kama alivyo sema anony hapo, mwambieni mengi kama atawasikiliza. pumbaf mnakera kama nini na tunawajua nyie kwa tabia zenu mbofu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 22, 2006

    Ama kweli nyani haoni kundule, Sasa nyie mmnaowakataza wenzenu wasitoe maoni yao hamuoni na nyinyi mnaleta sheria zenu mbofu mbofu?

    kama kweli mngekuwa mnataka kumpunguzia kazi mzee Michuzi, basi musingeandika kitu kwani kwa kuandika mnampa kazi ya kusoma maoni yenu amabayo nayo si mazuri.

    Hata hao CNN na IPp nao pia husikiliza maoni ya watu wanaotembelea Tovuti zao na ndio maana huzibadilisha kukidhi mahitaji ya walio wengi.

    Michuzi ni mtu wa watu na watu ndio sisi tunaotoa maoni yetu, Yeye Michuzi na MK wakitaka watachukua ushauri wetu na kama hawataki wataacha. Maoni sio lazima yafuatwe.

    Kala pesepsheni kwa kweli hiyo haipo kama rangi ni redi ni redi tu sasa wewe ukianza kuita redi ni greeni basi umuhimu wa kala hamuna tena kwani kila ana tafisiri yake!

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 22, 2006

    Hivi wewe anony hapo juu ulibahatika kuona hiyo kijani aliyokuwa ameweka mwanzo kabla hajabadilisha na kuweka hii iliyopo sasa? Ungekimbia nakwambia!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 22, 2006

    Anony 8:17 pm asante kaka kwa kumwaga point tupu. Watu wengine sijui wanajipendekeza kwa Michuzi? Mtu kutoa maoni kuna ubaya gani? Micguzi mwenyewe hajalalamika na ndio maana akabadilisha ile rangi nyeusi. Sasa hatuelewi wanaaochonga ni kwa faida ya nani. Hakuna shinikizo lolote la kumtaka abadilishe bakigraundi ila ni maoni tu. Hata CCN huwa wanapokea mawazo ya wasomaji wao ati kwa sababu wewe hujawahi kutoa maaoni huko ndio kusema hawashauriwi.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 22, 2006

    Wewe anon 9:51pm una ubongo sana wewe usikubali mtu yeyote akuambie vinginevyo na hakuna atakayeandika maoni bomba kuhusu hii insu zaidi yako wewe. Yeyote ambaye bado hajaelewa basi tena itamchukua karne nzima kuelewa. Hopufuli ktk harakati zao za kuelwa hawataporomosha matusi.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 23, 2006

    sasa hayo mabishano na hilo jengo kuna koneksheni gani acheni hizo!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 24, 2006

    Big up Lizzy, Michuzi kakaa chini, katoka na blogu, very interesting, picha kali..kumbukumbu..na nini..watu mjionee na kutoa comments..lakini wapi..watu mmeamua ku-devieti..mnapiga kelele ohh..kalaz za mashoga...kalaz zinaumiza macho...kalaz sio nzuri, kwani hii blogu ni kalaz blogu au... umelazimishwa kushiriki...kama macho mabovu vaa miwani acha uzushi, kama huna assosiesheni na mashoga, rangi haiwezi kukusumbua.
    Bwa' Michuzi, Hivi Mafuta House likoje sasa hivi, mimi nilivyotoka bongo ndio kwanza ilikuwa ghorofa ya tatu...lete utamu achana na wachimba chumvi wasio na shukurani fanya kipendacho roho ... au sio

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 25, 2006

    Lizy na anon 12:52 na nyinyi sasa maoni yenu na hilo jengo yana uhusiano gani?

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 25, 2006

    Hapo Ubalozi ndani(ofisini) kuna wafanyakazi wahindi, wazungu na weusi wachache lakini sidhani kama ni WATZ maana mmoja yule kapanda kama Mnigeria ama Muganda, inawezekana ni sera zao kuajiri walinzi tu wa Kitz kulinda na kupangisha watu foleni lakini si katika kutoa visa.Hapo kuna nyanyaso sana ingawa wapo sehemu moja na ubalozi wa Ujermani amabapo mambo yao safi sana. Serikali ipitie balozi kuangalia nyanyaso wanazotoa kwa ananchi sawa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...