aisha madinda (kulia) na mumewe fikiri na jesca charles siku twanga waliporejea toka sweden. jesca sas hivi ni mjamzito na amepumzika kazi na aisha kenda umangani kutafuta malisho ya kijani (green pasture?)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2006

    sasa michuzi mumewe kabaki na nani? au ndio kamshauriaende huko? na je wana mpango gani ukiachia mbali kutafuta pesa?

    hee jesta mjamzito? ujauzito wa mzungu wake bila shaka Mungu ambariki ajifungue salama.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2006

    Nalisoma kwenye DarHotwire, kuwa aisha kaachana na mumewe, yaani Fikiri, lakini kasema katu hatoaacha kutumia ubin wa mumewe yaani MAdinda kwa hiyo sharti la huyo atakayemuoa tena basi ajue hilo jina Madinda litaendelea kuwepo kutokana na jinsi ambavyo maLOVE yalimchukua.. Hivyo ndo alidai mwenye Aisha..

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2006

    nasikia jamaa jambazi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2006

    Duh Anony hapo juu acha mpakazo unaweza kusababisha akina Tibaigana wahamie nyumbani kwake bure maana nasikia siku hizi wakihisi tu wana wewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2006

    Kulingana na taarifa nilizonazo toka ndani ya jeshi la polisi, huyu yumo ndani ya listi ya watu ambazo wapo kwenye uangalizi mkali sana, mda si mrefu watamrukia. Ndio maana siku hizi Mapedeshee hawataki tena kuimbwa, hakuna cha papa msofe wala kizaizai

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2006

    ndo maana aisha anamkimbia kashaona hapa
    bora aanze mapema mambo ya kwenda segerea kucheki mume wapi na wapi?

    tafadhali michuzi unaweza kunisaidia picha ya nguza viking na wanawe walio jela PICHA ZA MUDA ZA SASA? maana niliona picha moja walipoenda kukata rufaa ilikuwa inatia uchungu na nilishindwa kumrikoginaizi vikingi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2006

    jamaa ukimwangalia anaonekana jambazi bila hata kuambiwa mhhh michuzi isije ikawa noma hawa watu wakaona unawaanzishia habari maana siye uwanja firriiiiiiiiiii entiri endi ekzitiii chochote twachotaka twasema tu ukizingatia mikono na komputa mali yetu kama unaona si nzuri tuambie tupunguze makali brooo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2006

    Michuzi hebu tufafanulie hivi kwani aisha bado ni MKE wa Fikiri?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 09, 2006

    Jamaa kweli noma, sasa Michuzi tunaomba picha ya Vikogo walio majambazi yule mchaga wa manzese na yule check bob mzee msingida....

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 10, 2006

    aise huyu mchaga sio yule wa manzese mwizi ni yule wa kariakoo, A.M umechanganya mambo hata mimi nimeomba sana picha zao lakini hatuwekewi sijui kwanini?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 10, 2006

    unacheza na jambazi nini wewe michuzi hata usijaribu sasa naona watu wana utani na life lako.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 10, 2006

    huyu jamaa kanikumbusha mapedeshee wa bongo kama yule aliyeuawa kule kasoro bahari, aisee Michuzi Papa Osama yuko wapi mbona hasikiki kabisa na hata pale Dom nikienda mitumbani simuoni ama?

    ReplyDelete
  13. inasemekana Aisha alishaachana na Madinda na hata jina siku hizi anaitwa Aisha Mbegu AKA queen Aisha kwa hiyo sikweli kwamba hataki kubadili jina la mumewe wa zamani halafu inasemekana hawakuoana bali walikuwa wanaishi pamoja tu

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 10, 2006

    Aisha kwa sasa yupo SAUDIA,na wametengana na Fikiri(Mungu si Peter wanaweza kujivinjali tena).Michuzi hebu lete habari za maendeleo ya kunengua Twanga bila Aisha.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 11, 2006

    rhxoqsa pengine soma hapa na pia ufanye utafiti zaidi...


    Sitaachana na Madinda- Aisha

    2006-04-15 08:21:11
    Na Swedy Kachenje
    Licha ya kuwa jina lake halisi ni Aisha Mohamed, mnenguaji Aisha wa African Stars ’Twanga Pepeta International’, ametoa sharti gumu kwa mwanaume yeyote anyewania kumuoa akisema kuwa kamwe hataacha kulitumia jina la barafu wake wa moyo aliyemwagana naye kitambo, Fikiri Madinda.

    Aisha amemueleza mwandishi wa habari hii katika mahojiano ’spesho’ ya maisha nje ya sanaa kuwa kamwe, hatakuwa tayari kulitupa jina la Aisha Madinda ambalo sasa ni maarufu mno midomoni mwa wapenzi wa muziki nchini, hasa wale wa bendi yake ya Twanga Pepetea.

    ’Nitaendelea kuitwa Aisha Madinda kwa sababu limenikaa na linaendana mno na mie... Halafu ndio ninaloendelea kulitumia katika kazi na hata kwenye shughuli zangu za kila siku, siwezi kuliacha kamwe,’ akasema Aisha ambaye alidodoswa na mwandishi sababu za yeye kujiita kwa jina hilo la pili ambalo ni la mwanaume anayedai kuwa ameshatengana naye.

    Zaidi, katika namna ya kuzuga ili asionekane ni kama anayejipigia debe tena kwa mahabuba wake wa zamani, Aisha akasema: ’Nakubali kuwa nimemmisi sana Madinda (Fikiri)... Lakini nahisi sijapungukiwa na chochote kwakuwa mbali naye. Bado nadunda na mambo yangu ni shwari.’

    Aisha ambaye amejitwalia umaarufu mkubwa kutokana na namna anavyoipamba safu ya unenguaji Twanga kutokana na jumbile lake ’tamu’ na cheza yake ya kupagawisha, akapigilia msumari wa moto kwa mwanaume yeyote atakayejitokeza kwake hivi sasa kwa nia ya kumuoa akisema: ’Nasisitiza kuwa nikimpata mwanaume wa kupendana naye, nitamuomba akubali niendelee kulitumia jina la Madinda kwa namna yoyote ile.

    Hata kama atapania kunioa, nitamkubalia kama atazingatia makubaliano haya... Vinginevyo, ni bora niendelee kuwa ’singo’ kwa sababu kazi ninayoifanya pamoja na biashara zangu kibao nje ya kazi hunifanya nisiyumbishwe na changamoto za kimaisha katika kujihudumia mwenyewe na familia yangu.’

    Kuthibitisha kuwa mambo yake ni swafi na kwamba kamwe hatababaishwa na mwanaume atakayepinga dhamira yake ya kujitambulisha kwa jina la Madinda, Aisha akamfichulia siri ’kiduchu’ mwandishi juu ya kile kinachompa jeuri kimaisha: ’Namshukuru Mungu kwa kila hali.

    Nina vibanda viwili safi vya kulala, usafiri ninao, saluni ya kike, kiwanja.
    • SOURCE: KOMESHA

    ReplyDelete
  16. Aksante sana kwa hiyo taarifa ya Aisha, sasa michuzi tuwekee na picha Lilian internet maana huyu ndio alikuwa kiboko ya huyu Aisha

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 15, 2006

    ILA FIKIRI ANA MOYO,AMEACHA AU AMEACHWA?WE FIKIRI HEBU REKEBISHA KICHWA HICHO!HUMU WATU WOTE WANAPATA TUSI ANGALAU MOJA LAKINI SIO AISHA,INA MAANA WATU WANAMKUBALI.MICHUZI EBU JARIBU KUMSHAURI FIKIRI AFIKIRIE VIZURI!AISHA ANA DISPILINI YA MWANAMKE,ILE KAZI SI MCHEZO KWA MTU MJINGAMJINGA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 19, 2006

    Lakini kweli,mtoto kama huyo unaacha au unaachwa?Kwanza wanaompenda Aisha wapo kibao na mie ndani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 19, 2006

    Huyu Jesca ni mzuri ila mkorogo ndo unamharibu,anakuwa kama kizee.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 20, 2006

    mmh!husimfananishe Jesca na Aisha, Aisha ana viwango!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 21, 2006

    FIKIRI RUDISHA MTOTO HUYO!ACHA HIZO!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 24, 2006

    Michuzi,kontakti za Aisha uarabuni unaweza ukazipata?Kama ndio naomba jibu nami ntawasiliana na wewe laivu na sio kama anony,nina ajenda ya siri na dada huyu!Fikiri si anajidai amesusa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...