miss tz wa kwanza theresa shayo akiteleza ukingoni mwa bwawa la hoteli ya kilimanjaro siku ya shindano la kwanza la ulimbwende mwaka 1967. wazee kuona hivyo wakayapiga top mashindano hayo ambayo yakaja ibuka tena mwaka 1964 na kuendelea hadi hii leo.

naona ndugu wengi hawana kumbukumbu nzuri, hivyo kuanzia kesho naweka picha na habari za miss tz moja moja kuanzia 1994. stei tyunnndd....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2006

    Asante sana Michuzi, sasa je baada ya hapa kulikuwa na uwakilishi katika mrembo wa Dunia ? nasema hivi kwasababu ukweli naona tutajifunza mengi kama tutataka kufanya vizuri kwa kuangalia hawa akina TERESA walikuwa wanafanya vipi.Yuko wapi huyu kwasasa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2006

    Michuzi What's Up with Misses?? Tushachoka sasa hebu anza kuprmote Wacheza sasa enh!. Hivi unadhani hilo kombe la dunia tutacheza kweli hiyo 2010 wakati mchezaji wa taifa hajulikani hata hapo Moro. Ushauri wa kufanya: Kuanzia leo atleast tuwekee Picha ya mchezaji mmoja mmoja wa National Team na historia yake. Wakina Gulla Joshue tunawasikia tu hatujawaona. Au unataka mpaka wa make Big Time ndio michuziuanze kuwafagilia?? Oyah Miroast nilikuomba picha ya China anamtesa marehemu Gagarino. Nayo unakunja?? Acha hizo usikunje wote sisi Yanga dam dam. Na hiyo Blogg Colour yako vipi Michuzi?? Next time weka Njano na Kijani. Nasubiri picha sitoki hapa najua utazipost soon.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2006

    Unajua kwasasa kuna mabo mawili ambayo Michuzi kayazingatia na hasa kutokana na ombi lako nadhani atazingatia.Kitaifa hapa TZ kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Tz 2006 kimeanza hivyo ni chnangamoto kuweka picha za mamiss tuone tulikotoka na hata wazo la kuweka mmoja mmoja linafaa. Pia kidunia sasa tuko katika maandalizi ya kombe la dunia na hili nalo atalifanyia kazi kwa kuaza kuweka picha za wachezaji wa dunia sasa sijui kama ataanzia na za akina China ama la, TUSUBIRI,nayo ni kazi hii tumpe hongera kama shukjrani zetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2006

    Katika kinyang'anyiro cha mrembo wa dunia mwaka 1967 kilichofanyika London uingereza tarehe 16 mwezi novemba mwaka 1967, mrembo wa tanzania Theresa Shayo aliishia raundi ya kwanza.kwa upande wa bara la afrika ghana ndiyo iliingia nusu fainali lakini mshindi aliibuka mrembo wa PERU akifuatiwa na argentina na wa tatu guyana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2006

    Jamani kweli vimiguu vya wachaga huwa vinachekesha jamani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2006

    Ni kweli michuzi umeibukia kwenye mamiss vitu vya maana huleti. Ukoje wewe mbona una picha za maana nyingi tu? Tatizo liko wapi? UNABORE BWANA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2006

    Kwa sasa atakuwa na miaka 59 kama kipindi hicho alikuwa na sitini ....

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2006

    Oppppssss!!!Kwa sasa atakuwa na miaka 59 kama kipindi hicho alikuwa na 20 ....

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 25, 2006

    Nathani wanaotaka picha za michezo wachecki katika blogu ya athumani

    http://www.blog.co.tz/athumani/

    ReplyDelete
  10. Anonymous said...
    Ni kweli michuzi umeibukia kwenye mamiss vitu vya maana huleti. Ukoje wewe mbona una picha za maana nyingi tu? Tatizo liko wapi? UNABORE BWANA.

    4:47 PM, May 25, 2006

    jamani eeee. mtu kama huyu nimjibuje wakati hata simjui, sijamkaribisha na wala hanilipi. sijui inglishi ningejua ningemjibu: what's good for the goose is bad for the hen. lakini ah, dno hivyo tena, ni kweli na-bore (shimo)ama vipi mjamaa, whoever, wherever ur. wewe ndo unaboa

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 25, 2006

    We Michuzi huna haja ya kumjibu Ntu kama huyo achana naye na usipoteza muda wako kusoma. Halafu wale wanaotukana humu bana itabidi uanza kunukuu IP zao kama wakiendelea na tabia hiyo basi na wasikuje hapa.

    Kama ulivosema hujamualika sasa maneno mingi ya nini?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 25, 2006

    mICHUZI NAONA UNATUCHANGANYA MASHINDANO YATAPIGWAJE MARUFUKU MWAKA 67 HALAFU YARUDISHWE MWAKA 64. HIYO MIAKA YAKO UNAHESABU VIPI? kiarabu nini?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2006

    Anony 10:17,
    Nafikiri Michuzi alimaanisha 1994

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2006

    huyu enzi hizi hawezi kushinda, paja utafikiri maradona

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 01, 2006

    Huyu ndiye Mama Makata sasa hivi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...