
nilibahatika kuwa mjumbe wa kamati ya ushauri wa ujenzi wa ukumbi wa taifa wa maonesho (national theatre) chini ya makumbusho ya taifa, na tulitembelea nchi kadhaa kuonaa wenzetu wanafanya nini ili tuweze kuchuma jani la kufaa watanzania. hapa ni windhoek, namibia, kwenye kituo cha sanaa cha katutura maarufu kama jiko. nchi ya uswidi imekubali kugharamia ujenzi huo wa thieta ya kisasa ilipo makumbusho ya taifa mtaa wa shaaban robert. michoro tayari na mkandarasi anatafutwa. mambo yakienda vizuri tutakuwa na thieta ya taifa ndani ya mwaka mmoja. kwa taarifa yako (samehe ung'eng'e wangu) hivi sasa makumbusho ya taifa dar yanaitwa national theatre and museum. ujenzi wenyewe utakuwa ni wa ghorofa juu ya majengo ya sasa na upanuzi wa uwanja


Michuzi,
ReplyDeleteHivi hakuna eneo lingine ambalo mnaweza kujengea hiyo theatre zaidi ya hapo Makumbusho? manake kwa ufahamu nilionao, taasisi ya makumbusho na ukumbi wa sanaa ni maeneo mawili nyeti sana kiasi kwamba kuyaweka mahala pamoja sina hakika kama ni busara.