nilibahatika kuwa mjumbe wa kamati ya ushauri wa ujenzi wa ukumbi wa taifa wa maonesho (national theatre) chini ya makumbusho ya taifa, na tulitembelea nchi kadhaa kuonaa wenzetu wanafanya nini ili tuweze kuchuma jani la kufaa watanzania. hapa ni windhoek, namibia, kwenye kituo cha sanaa cha katutura maarufu kama jiko. nchi ya uswidi imekubali kugharamia ujenzi huo wa thieta ya kisasa ilipo makumbusho ya taifa mtaa wa shaaban robert. michoro tayari na mkandarasi anatafutwa. mambo yakienda vizuri tutakuwa na thieta ya taifa ndani ya mwaka mmoja. kwa taarifa yako (samehe ung'eng'e wangu) hivi sasa makumbusho ya taifa dar yanaitwa national theatre and museum. ujenzi wenyewe utakuwa ni wa ghorofa juu ya majengo ya sasa na upanuzi wa uwanja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2006

    Michuzi,
    Hivi hakuna eneo lingine ambalo mnaweza kujengea hiyo theatre zaidi ya hapo Makumbusho? manake kwa ufahamu nilionao, taasisi ya makumbusho na ukumbi wa sanaa ni maeneo mawili nyeti sana kiasi kwamba kuyaweka mahala pamoja sina hakika kama ni busara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...