kuna ndugu kaomba hii picha. naomba kuwakilisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2006

    Mimi naamini kama wewe Michuzi huwa hupati muda wa kuongea na JK basi JK huwa anasoma Blog yako. Ujumbe naotaka aupate ni kwa YEYE NA LOWASSA WAKAZE MWENDO KUSAFISHA SERIKALI MAMBO YALISHAOZA HAPA MPAKA WATANZANIA WOTE WANANG'ANG'ANIA KUIKIMBIA NCHI.

    Asafishe vigogo wote ambao wamejineemesha fedha zetu halafu sasa wanabaki kutumwagia maji barabarani mvua ikinyesha ama kututimulia vumbi mvua isiponyesha, wakati fedha hizo wametuibia wenyewe.

    Jana mimi nilikuwa napita maeneo ya Mbezi nikamuona mtoto mmoja wa miaka kama 13 hadi 15 hivi wa kizito, ambaye ana utajiri unaotisha, anaendesha BMW utadhani 50cent halafu akawafanyia ujeuri wa kuwamwagia maji wamachinga walikuwa wamekaa pembeni ya mti kuepuka adha ya manyunyu ya mvua. Iliniuma sana na mpaka leo hata kazi nashindwa kufanya kila ninapokumbuka. Watoto kama hawa baba zao wakiadabishwa kwa kunyang'anywa fedha walizolimbikiza tutaheshimiana vinginevyo Watu hawataipenda nchi yao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2006

    Kuna hilo za hela za import support walizokuwa vigogo wanajigawia kupitia kwa huyo Mhindi Yusuph manji. Hiki ndio kipimo cha JK tutaona litashughulikiwaje, likizimwa kimya kimya basi tena bora tufie huku huku tulipo na tuzikwe huku huku sio TZ. Inauma sana kwa kweli.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2006

    Anony hapo juu, mimi naweza kukujibu sasa hivi katika hiyo issue, hakuna kitakacho shughulikiwa. Lazima uelewe kwamba pamoja na kwamba JK ni mtu mwema na mwenye nia nzuri na nchi yetu, mikono yake imefungwa. Hiyo ni part ya sababu kwanini BM alikazana kuhakikisha anakuwa yeye Rais, kuwalinda na kutetea the "status quo". Yaani kuendeleza na kulinda maslahi ya wakubwa wenzie na waliotangulia!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2006

    Mimi nadhani kwa Watz mtu wa kuweza kuongoza nchi yetu na kufikia popote ni MCH. CRISTOPHER MTIKILA. Hii Missm inalindana tu hizo hela za import support nasikia hata jk na el wapo kwenye list ya waliokuwa wamesainishwa mkataba na huyo Gabanjoli Manji. Sasa kuna kitakachoendelea tena hapo, Ndio maana Manji anakuwa na kiburi kama nchi yake wakati yeye ni gabacholi tu. Michuzi tunaomba utuwekee picha ya huyo Manji sisi wengine hatumjui,

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2006

    Nilikuwa sijapita hapa hila nimesikitishwa na maswala mengi kwanza ni Anony 3.03Pm june13. Hilo bwana hawa watoto mtu mmoja alishawahi kuandika humu kuwa watoto wa wakubwa wanakuwa na madaraka kuliko watoto wao. Halafu kibaya sana baba zao walisoma lakini hawataki kuwasomesha watoto wao. Hilo linafanya watoto wawe na fikra finyu na kutumia madaraka/uwezo wa baba zao vibaya, wamgelikuwa wameelimika hilo lisingelikuwepo.

    JK nafikiri kuna sehemu nimesema Inabidi hiyo kasi aliyotumia kupunguza nguvu majambazi itumike katika upande wa pili by the way mimi nafikiri gabacholi siyo mtu wa kukaa hata kuongelewa katika nchi kama tanzania. Huyu bwana mambo yakiwa mabaya alipo ana urahia wa nchi kibao. Muda wowote yeye ni kutuaribia nchi na kukimbilia nchi nyingine. Kwa hiyo suala la kumushughulikia lisiwe na mjadala.

    Kama wengine walivyosema hicho ni kipimo kwa JK. Mzee BMW alitaka ushaidi, JK alisema ushaidi hataki wakikusema tu yuko na wewe sasa Michuzi mwambie Manji wameisha mtaja. Lakini siyo manji tu watu wameimeza Tanzania wachunguzwe hata na mzee BMW make nasikia katika madini yeye hana 10% kama wengine yeye ana 90%.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...