Retired President Benjamin William Mkapa and wife Anna cut the cake to commemorate the 40th Anniversary of their wedding during luncheon they hosted at their Sea View residence in Dar es salaam yesterday. The couple also used the occasion to thank the Almighty God for giving them the opportunity to serve Tanzania for 10 years as President and First Lady respectively.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Haya wajameni mnaosema mama mkapa na mumewe wametengana - haya sasa hao hapo wakata keki ya kukumbuka ndoa yao ya miaka mingi JAMANI MTASUTWA

    ReplyDelete
  2. Mungu awazidishie afya,nguvu na umri mrefu.

    ReplyDelete
  3. Naona mzee kapungua kidogo, gym kwa wingi nini!!

    ReplyDelete
  4. Haya sasa wabongo mtasutwa kabisa,sasa hio nayomseme ya uongo,yaani watz bwana waongo sana!

    ReplyDelete
  5. watu waongo,eti mara ooh nyerere aliwaambia wasiachane ili mkapa aqualify uraisi,mlikuwepo?wabongo bwana ujue watu huwa wanachonga sana bila kufikiria

    ReplyDelete
  6. Mwache apumzike salama, jamaa katupotezea miaka 10 bila mipango ya maana zaidi ya kuuza nchi kwa wageni.

    I hope anaelewa kwamba Watanzania wengi wanamuona kama mbabaishaji

    ReplyDelete
  7. Jakaya mwenyewe kakiri kuwa antembea kifua mbele kwa sababu ya kazi nzuri ya huyu mzee...mnathubutu kusema kuwa katupotezea muda wa miaka kumi. Hivi anayesema hivi anaongea toka moyoni au kufurahisha genge? Au labda ni kutojua?

    ReplyDelete
  8. Wewe anony wa Aug. 29 12:55pm, Sasa jakaya akikiri ndio nini? Unategemea aanze kumponda? Na kama jamaa alifanya vizuri hivyo hiyo mikataba na barrick kwanini wameirejea? Mbona wamekiri Net solution ni wababaishaji? Kwa ujumla huyu jamaa aliuza nchi kwa uambiliki wake.

    ReplyDelete
  9. Tuacheni unafiki kwa miaka mingi tuliozea vya bure sasa kila mtu abebe zigo lake mwenyewe watu mnalalamika ,tunajua kuainisha wezi na mabaya mbona mazuri hamsemi aliyewezesha serikali kukusanya mabilioni ya pesa kila mwezi nani tuacheni fitina kwani haina posho mnatusi watu tuu ilimradi mkonge roho zenu huyu mzee kafanya kazi japo hakuna na wapenzi wengi lakini kazi kwa aina mmoja imefanyika

    ReplyDelete
  10. KAZI GANI WEWE ANONY WA 4:11AM? TAFADHALI UNAPOJARIBU KULETA USHABIKI AMBAO HAUNA KICHWA WALA MIGUU BASI LAZIMA UJUE NA KUTOA MIFANO HAI PAMOJA NA VIELEZO VINAVYOELEWEKA! UNAJUA UCHUMI HAUKUI KWA MANENO ETI KWA KUWA MKAPA KASEMA UCHUMI UMEKUWA BASI NDIO UMEKUA!KWA UFUPI HUYU JAMAA AMELETA MATESO MAKUBWA KWA WATANZANIA NDANI YA KIPINDI CHOTE CHA UTAWALA WAKE WA MIAKA 10 NA WALA USITEGEMEE KUWA KIKWETE ATASEMA WAZI SUALA HILI KWANI NI KINYUME NA UTARATIBU WA CCM NA KULINDANA HIVYO LAZIMA ASEME KUWA ANATEMBEA KIFUA MBELE KWA KAZI NZURI YA MKAPA!LAKINI WAKATI HUO HUO TUNAONA MIKATABA KAMA YA MADINI NA MENGINEYO ANAAGIZA ICHUNGUZWE UPYA!

    ReplyDelete
  11. KAZI GANI WEWE ANONY WA 4:11AM? TAFADHALI UNAPOJARIBU KULETA USHABIKI AMBAO HAUNA KICHWA WALA MIGUU BASI LAZIMA UJUE NA KUTOA MIFANO HAI PAMOJA NA VIELEZO VINAVYOELEWEKA! UNAJUA UCHUMI HAUKUI KWA MANENO ETI KWA KUWA MKAPA KASEMA UCHUMI UMEKUWA BASI NDIO UMEKUA!KWA UFUPI HUYU JAMAA AMELETA MATESO MAKUBWA KWA WATANZANIA NDANI YA KIPINDI CHOTE CHA UTAWALA WAKE WA MIAKA 10 NA WALA USITEGEMEE KUWA KIKWETE ATASEMA WAZI SUALA HILI KWANI NI KINYUME NA UTARATIBU WA CCM NA KULINDANA HIVYO LAZIMA ASEME KUWA ANATEMBEA KIFUA MBELE KWA KAZI NZURI YA MKAPA!LAKINI WAKATI HUO HUO TUNAONA MIKATABA KAMA YA MADINI NA MENGINEYO ANAAGIZA ICHUNGUZWE UPYA!

    ReplyDelete
  12. Tumuombee rais wetu mstahaafu mpumziko mazuri baada ya kuwasaidia wananchi wa tanzania kwa kipindi cha miaka kumi.

    Hila nafikiri nayeye hata ukimuuliza amefanya nini hataweza kukwambia mazuri zaidi ya kuikuta tanzania yenye amani na utulivu na kuiacha tanzania yenye amani na njaa tele. Mzee tunakubali initiative zako za kutuletea umaskini mzee asante sana.

    ReplyDelete
  13. Lakini wajameni tuache utani hili zee lina busara. Yaani pamoja na yale yote yanayosemwa kuhusu Anna aliyomfanyia kabla ya ndoa bado aliweza kusema uvumilivu ni silaha kubwa katika ndoa. Na akamalizia kwa kusema "namshukuru mke wagu Anna kwa kuwa mvumilivu miaka yote hii". Hii ni busara iliyopevuka. Wachache wanaweza kufanya hivi.

    ReplyDelete
  14. Hakuna hata Kiongozi mmoja duniani ambaye anaweza kutatua matatizo yote ya Nchi.Kila mtu anauwezo wake na mapungufu yake. Ndio maana ni muhimu hawa viongozi kubadilika kila baada ya muda fulani. Sidhani kama kuna mtu hata mmoja anayeweza akamtaja Raisi , mfalme,malkia,waziri mkuu au ayatolah yeyote aliyefanikiwa kuwa jibu la matatizo yote ya nchi yake. Tatizo la Afrika zaidi ni ukweli kuwa ni viongozi wachache ambao wanafikiria kutatua matatizo ya nchi zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...