Morning rush hour along Ali Hassan Mwinyi road in Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Watu wanapenda kwenda na magari yao ofisini kwani maofisi mengi hayatoi mabus ya wafanya kazi kama wale wa Bank kuu. Wafanyakazi wengi wa bank kuu huwa wanatumia mabasi ya ofisni na sio magari binafsi hiyo ndio moja ya sababu ya kuongezeka foleni mijini. Hayo magari mengi yana watu 2 ka sio mtu mmoja

    ReplyDelete
  2. Mabasi ya kampuni, na kuchukua wafanyakazi ni system ya kijamaa. Kwenye nchi za west, wewe mfanyakazi ni jukumu lako kufika kazini, si la mwajiri.

    ReplyDelete
  3. Acheni kufikiri kila kitu kinachofanyika ughaibuni kinaweza kufanyika bongo. Mazingira ya yetu car pooling ni ndoto. Bongo mkipanga sehemu ya kukutania ndio mmeshafika mjini (kazini)car pooling ya nini, pili hamwezi kuacha magari kwenye parking za wazi maana yote yanaweza kuibiwa. Tatu si kila familia ina gari, utafanya poolling na nani. Watu wanaofanya kazi ofisi moja mwingine anakaa kijichi, mwingine Tabata mwingine Ukonga Mwingine kimara n.k sasa hawa watafanyaje car pooling?

    ReplyDelete
  4. Hayo mawazo yote hapo juu ni mema. Lakini wazo jingine, ni kwanini Serikali isijaribu kufikiria nje ya box na kutafuta alternative to Surrender Bridge kwa mfano, ku-improve miundo mbinu ili kurahisisha maisha ya watu, na kuongeza uzalishaji kwa ku-save time??!!

    ReplyDelete
  5. Ama kweli anany... wa August 31, 2006 5:41 PM
    amechemka kufananaisha nchi za west na zetu. Hujui serikali inapoteza kiasi gani kwa kupean transport allowance au fuel allowance. west wakurugenzi wako kwenye treni wanakwenda maakazini sio kwetu kila mkurugenzi na gari yake. Nafikri mabasi ya kwenda kazini suluhisho zuri na sio Ujamaa

    ReplyDelete
  6. We hapo juu hukumbuki kuwa idea ya mabasi ya kazi ili prove failure? Kama ni costs, ni kubwa zaidi ukiwa na mabasi, pia kuwepo kwa mabasi kutazidisha mwanya wa Transport Officer kula na magereji, na petrol stations, na maduka ya spare. Bado nakukumbusha, hizo ni idea za kijamaa, ambao tulijaribu kuwaiga, nao wanayumba tu sasa(Soviet Union, China). Kufika kazini ni wajibu wa mfanyakazi, sio wa mwajiri. Hata U.S. wafanyakazi wenye certain positions only wanapewa gari ya kazi, tena hawakai nalo nyumbani. Wanalitumia baada ya kufika kazini kwa business trip only. Baada ya kazi wana park gari kazini na kuchukua gari zao. Ndio maana TZ si kitu cha ajabu kukuta gari ya public institution, au private company ime park bar after office hours. Huo ni uzembe, na misuse of tax payers' money, au company property (private firm). Solution ni bara bara pana zaidi. Kwa mfano: Kawawa Rd ikawa four lane, A.H.Mwinyi Rd ikawa six lane, na Morogoro Rd nayo ikawa six lane, all the way to down town, traffic jam itapungua sana, kama sio kuisha.

    ReplyDelete
  7. mimi nafikiri tatizo lililopo hapa ni mrundikano wa office zote sehemu moja,
    kwanini tusifikirie uwezekano wa kutanua mjia zaidi na kuhamishia maofisi sehemu nyingine za mji,
    huu msongamano wote unaishia posta na kariakoo na ukifika hukohata sehemu ya kuegesha hakuna.

    ReplyDelete
  8. mimi nafikiri tatizo lililopo hapa ni mrundikano wa office zote sehemu moja,
    kwanini tusifikirie uwezekano wa kutanua mjia zaidi na kuhamishia maofisi sehemu nyingine za mji,
    na piya tujaribu kuangalia wawekezeji katika sekta usafiri hasa katika jiji letu hili,
    tunahitaji kuwa na vitu kama city trams na pia kama alivyosema anony mmoja hapo management ya usafiri ni muhimu sana kwa maana ya kuwepo utaratibu wa kupanga rroot kutegemeneana na naina ya usafiri,
    unapoweka lory,daladala na magari madogo kwenye msafara mmoja ni kucreate chaoss!!

    ReplyDelete
  9. Wandugu mawazo mazuri sana na mimi ningependa kuchangia kidogo.
    Western countries, mpaka wakurugenzi wanapanda mabasi kwa sababu systems za mabasi na city trains zinaaminika, ni salama na zinaokoa muda. Lakini kwa sasa hivi, Tanzania hiyo haiwezekani kwa sababu kwanza public transport is not safe, not reliable and a total chaos. Kama mwanablogu hap juu alivyosema, kukiwa na business lane kwa ajili ya mabasi na taxes, mabasi hayatakuwa yakikaa kwenye foleni na hivyo kufika mwisho wa safari haraka zaidi ambayo itakuwa motisha kwa watu kutumia mabasi zaidi na hivyo kupunguza foleni. Pili, kama nilivyowahi kusema hapo mwanzo, usafiri jijini inabidi uwe Unified, yaani itafutwe kampuni moja au mbili kubwa wa ajili ya kutoa usafiri jijini. Hiyo itarahisisha udhibiti wa sheria za barabara na usafirishaji na pia kuongeza ufanisi. Mabasi yanaweza kuwa yanakwenda na wakati, having mor busses on rush hours and fewer busses on down times. Hii isiwe UDA tena bali itafutwe private company, ya nje au ndani. Watu kama Scandnavia wanaweza kupewa kipaumbele. Hii pia itaondoa ghasia na kero za usafiri kwa wanafunzi. Vitu kama monthly or annual bus passes can be introduced. Kwa mtaji huu tutaona watu wengi zaidi wakitumia mabasi kuliko magari yao binafsi.
    kitu kingine pia, majengo mapya ya ofisi yafunguliwe nje ya City center ili kupunguza msongamano wa watu mjini. Electronic means of communications kama email and phone services ziwe zinatumika zaidi kuliko "Mamesenja".
    Haya basi watanzania wenzangu, kama ilivyo ada, unaruhusiwa kutoa ukosoaji wako, By the way Big Up Michuzi, hakuna nafasi za wabunge wa kuteuliwa zilizobaki upate moja?..lol

    ReplyDelete
  10. I am a Tanzanian who lives in somewhere in US; I have not been home in abt. 17 yrs (shame on me!). Your photos are wonderful, they bring good memories about home. Actually, the photos made me home sick! Thank you so much for your effort and the time you put into this.

    God Bless you-

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...