je unamkumbuka ama umepata kumsikia huyu jamaa? aliwahi kuwa bw mifugo pale dom iko siku aliibiwa kichwa cha fisi alipokuwa akikisafirisha kuja dar kwa uchunguzi baada ya marehemu fisi huyo na wenzie kuwashambulia watu kijijini itiso kule dom vijijini.Nasikia yuko ughaibuni ila baadaye alikuja kuwa katibu mkuu wa chama cha volebo mkoani dom na kisha kuwa katibu mkuu msaidizi wa chama cha volebo bongo (tava) na alikuwa pia mmoja wa walimu waliobobea wa volebo bongo na mwamuzi wa kimataifa wa mchezo huo, na mratibu wa mchezo huo wa kombe la bonite linaloshindaniwa kila mwaka pale moshi. nondo zake zaidi soma www.tanzaniasports.com
Nimemuweka hapa kwa kuwa toka aondoke yeye na wenzie mchezo huu kama umekufa hapa bongo, ukiondoa jitahada za timu ya magereza ya dar na kocha wake edwini


hahahaha nipo huku Ohio siku nyingi Dah Umenikumbusha mbali sanaaa, hongera naona Blog imekucha? Nipo na huyu kichaa wangu Msami actually ni room mate wangu ana BIMA kali saana basi hashikiki, poa nakuja december nitafika kwenye goli lako hapo photo point.Msalimie Edwin na wengine. Michuzi umenikumbusha mbali saaanaaa! Dooh hii picha.....?
ReplyDeleteWe Mzee wa Dom ndio wale wale wanaoona magari ni kitu cha ajabu. Huna haja ya kutuambia fulani anaendesha gari la aina fulani. Gari ni chombo cha usafiri tu kikuezeshe kukufikisha uendako bila kujali kuwa ni VW Beetle au BMW. Gari si sawa na household item kama vile kijiko, au sifuria ndani ya nyumba. Mbona sisikii ukisema fulani ana kijiko, au ana kikombe. Gari sio alama ya mafanikio, ni moja ya basic things inategemewa, ingawa si lazima mtu awe nalo. Ukianza kubabaikia magari na kutuambia fulani ana BMW unaonyesha kama vile magari umeyakutia U.S. Usiwe kama wa Kenya wanaoshindana kuendesha magari mapya kama vile magari wameyajua U.S. Narudia tena, gari sio big deal, na kama toka ukiwa TZ mlikuwa na magari nyumbani, huwezi kuja kwenye blog na kuanza kusema unaendesha BMW. Kwa taarifa yako watu hizo BMW walishakuwa nazo toka wako TZ,miaka ile ya nyuma. Kwa hiyo ukiona mtu na gari lake wewe nyamaza tu, vinginevyo unajichora tu, na kujionyesha jinsi gani ulivyo limbukeni wa magari.
ReplyDeleteHuyu mzee wa Dom ni mzushi anapenda sifa tu. Inaonyesha pia kamtumia Michuzi picha hiyo ili iwekwe hapa aanze ulimbukeni wake wa kusifia magari. Kama ni siku nyingi hajaonana na Michuzi iweje michuzi aweke hapa picha yake iliyopigwa tarehe 30/8/2006? Ulongo mwingine mwe mnaufikiria kwanza mtakuja umbuka. Unadhani ukisema uko Ohio ndiyo sifa sana?
ReplyDeleteMimi sioni tatizo hapa liko wapi, huyu jamaa alikuwa kiongozi wa Michezo, na Yeye hajatoa maelezo yeyote juu ya gari, na kwa sisi tunaomfahamu hapa London yeye ni Mtu wa Mabasi na Treni Tu, Na wala hayuko Ohio, Wabongo bw! tuna tabia ya kulaumiana na kukosoa watu bila Facts. Michuzi unafanya kazi Nzuri Sana ya Kutuonyesha sura za zamani ila unakosea unapoweka picha za mtu mmoja mara nyingi mfano Lady J dee!....Vinginevyo kila la Kheri.
ReplyDeleteUsituzuge wewe...mbona picha inaonyesha imechukuliwa 2006???
ReplyDeleteKwani Michuzi unamatatizo gani na hawa wasomaji wako? kama ni Picha ya huyu jamaa kuwa na tarehe ya hivi karibuni ni mgogoro mbona angeweka kwenye Website yake?.
ReplyDeleteNa je kuna tatizo gani la mtu kuwa na picha ya karibuni kwenye Blog yako..hebu Michuzi nitafutie picha ya John Zambetakis na Rehema Munga na kutuwekea pia Ya Dudley Mawala wa Ymca karate club.
We anony wa september 04, 2006 1:36am hujui unachong'ang'ania kutetea. Michuzi kapost hiyo picha hapo presumably kuwa yeye ndiye aliyempiga hiyo picha. Sasa kama michuzi ndiye kaipiga maana yake walikuwa na huyo mzee wa Dom. Sasa kwanini aanze mara siku nyingi, mara niko Ohio, na kama hakuipiga Michuzi bali yeye mzee wa Dom ndo kamtumia kwanini aanze kujifanya michuzi hafahamu aliko ilhali wanawasiliana hadi kutumiana picha? It is not a big deal lakini nakubaliana na anony wa hapo juu aliyeongelea tarehe ni udadisi tu!
ReplyDeleteSio rahisi sana kupata ukweli wa kila hoja. Unaweza kuwa na picha resent ya rafiki bila ya yeye kujua hilo kwa sababu kuna namna nyingi za kupata picha. Hata hivyo hakuna ubaya kwa vile kusema habari za siku nyingi inaweza kuwa ni mazoea au namna ya "kuvunja barafu tu" Jaribu kutembelea hosptalini leo halafu uwaambie wagonjwa kumi tu "haujambo?" Lazima utapata wanaosema "sijambo" japo wako hoi. Mazoea hayo.
ReplyDelete