sijui daraja la kigamboni linalotarajiwa kujengwa karibuni litakuwa hivi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi hili daraja tumesikia story zake miaka nenda rudi, litajengwa kweli? hebu tupe siri ya jikoni huko! mara tunasikia kivuko kipya kitanunuliwa, kikubwa na cha kisasa, which is which????????????????????? mbona mnatuchanganyia habari wajameni????????????

    ReplyDelete
  2. tatizo ni nini hapo? wampe mwekezaji ajenge, then tuwe awe anatutoza kupita na michuma yetu hadi mshiko wake utakaporudi!

    ReplyDelete
  3. Anon hapo juu usiwe na wasiwasi kuhusu habari za darala la Kigamboni-Ferry. 10 per cent ndio itakayoamua lijengwe daraja au kinunuliwe kivuko kipya.

    ReplyDelete
  4. NDOTO ZA KIMWELI! wabongo tuwe na daraja kama hili, Nyerere alikataa lisijengwe miaka ya 70s kwa sababu za kijinga, eti watu watakuwa wanachungulia IKULU!!

    ReplyDelete
  5. SUBUTU NAZANI HIZI ZITAKUWA NI HABARI TU ZA ABUNUWASI NA NDOTO ZA KUWA POPULAR KAMA SHENA SINARE, ALIYEZUSHA KUWA PETER RUPIA ALIMWAHIDI KUMUOA. PUNDE BAADA YA PETER KUMTOSA KWA KUSHINDWA NA TABIA ZAKE SHENA AKAJIMWAGA HAPA BULOGUNI NA WATU WAKE KUJITAMBA NA KUZUA KUWA PETER KAMTISHIA KUMUUA. WAKATI HATA FAMILIA INAJUA KUWA SHENA NDIO KUTWA ALIKUWA AKITISHIA KUJIUA YEYE MWENYEWE.
    KWA HIYO BWANA MICHUZI NINA WASIWASI KAMA DARAJA LITAKUWA KAMA HILI, NI UZUSHI NA NDOTO ZA ABUNUWASI TU. LAKINI NGOJA TUONE SEREKALI HII SI WAMESEMA KASI MPYA NA ARI MPYA? LABUDA LAKINI,,,,MH! SIJUI.

    ReplyDelete
  6. Anony wa 11:31, Mashaallah. Ni hapo watakapopata ten pasenti ndipo watakapo amua ama daraja au kivuko. Bila shaka kwa sasa bado wanaendelea kutafuta kivyko sekandi hendi huko Burma au Marekani, kwani njini mwetu ni marufuku kununua chombo kipya cha usafiri. Rejea pantoni zote za Kigambo, tule tu ferry twa ziwa victoria na hata hako kadege ka rais.

    ReplyDelete
  7. WE UMEME TU UNATUSHINDA ITAKUWA DARAJA KAMA HILI, HAPO MPAKA DUNIA IGEUKE, SISI TUTAKUWA NA MV KIGAMBONI MPAKA IZAME IUE, NDIYO TUTAANGALIA KUNUNUA NYINGINE TENA KWA 10%. HIYO NDIYO BONGO BWANA UBINAFSI MBELE KWANZA....!!!

    ReplyDelete
  8. Mbona mnaenda mbali washikaji? Hicho kivuko kimetushinda itakuwa daraja la aina hiyo? Hizo barabara zina mahandaki ya kuficha ndege za Jumbo Jet na kila wakati wa mvua hugeuka kuwa mito, itakuwa daraja la kifahari kama hilo? Hizo dawa za UKIMWI tu hazijawafikia walengwa wote kwa kuwa mijaaa inachota kwa ajili ya matumbo yao utadhani wataishi milele... itakuwa hilo daraja la Kigamboni? Hizo ni ndoto za Alinacha! Kisha mambo mengi serikali hii inaahidi kufanya... mara bandari ya Bagamoyo .. mara kila kijiji Kata itakuwa na zahanati / hospitali ... mara kila Kata itakuwa na shule ya sekondari... Hivi, yule Mhasibu aliyetoroka na Fedha zaidi ya Dola Laki nane za Marekani [$800,000] za Wizara ya Miundo Mbinu amerudisha? Au katafuna hizo fedha na wakubwa waliomsaidia kufeki shinikizo la damu na kumtorosha chini ya ulinzi wa askari magereza akiwa mgonjwa taabani...? Sasa Wizara gani itakayojenga hilo daraja? Msilete utani hapa Watanzania!

    ReplyDelete
  9. hahaha its cool 2 have dreams though

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...