adam lusekelo akiwa india hivi majuzi akila pozi na bawabu katika hoteli alofikia. huyu bwana ni mmoja ya watu walioniinspaya sana kuingia fani ya uandishi kutokana na makala zake za kuvunja mbavu kwenye sande nyuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kweli Michuzi Mie sio mwandishi lakini hujasema uongo huyu jamaa ni mzuri kweli kwa makala zake. Alinifurahisha sana kwa makala yake moja sikumbuki ni tarehe gani lakini alikuwa akiwaponda TAMWA walipomkandia Mama Salma Kikwete alipoenda Swazz kuhudhuria sherehe za King Mswati kuchagua mke. Ile ilikuwa nzuri sana au unasemaje Michuzi uliiona au ilikupita pembeni?

    ReplyDelete
  2. Kuna waandishi wa habari wa gazeti la serikali la Daily News ambao wanaonyesha kuwa si waandishi wa his/her masitas voisi, kwa mfano, Adamu Lusekelo na Makwaia wa Kuhenga. Labda ni mfano mzuri wa uandishi wa magazeti! Hukosoa hata serikali, konstructivuli!

    ReplyDelete
  3. Tikei(ahsante,safi,poa kwa kihindi)

    ReplyDelete
  4. Kweli kabisa, huyu Lusekelo makala zake zinakubalika na bongo sidhani kama ana mpinzani (labda Valentine Nkwame wa Arusha Times). Umahiri wake na kalamu nauweka level moja na akina Charles Onyango Obbo wa Uganda.

    ReplyDelete
  5. ...lakini nadhani huyu bwana aliisha achana na Deil Nyuz na ni kama Columnist tu, ingawa sina hakika sana labda Michu atufafanulie.

    ReplyDelete
  6. nakubaliana na nyote hapo juu...huyu bwana amebobea katika fani yake.

    Nafikiri angepewa nafasi ya kuwapiga msasa waandishi wa habari wa siku hizi kama wale wanaoandika ippmedia.com, samahani bwana Mengi kama unasoma hii blog...site yako ina habari nzuri lakini kwaliti ya yale yanayoandikwa humo hairidhishi kabisa.

    ReplyDelete
  7. Anon wa Monday, October 23, 2006 4:00:05 PM-----------Charles Onyango Obbo alikuwa anafanya kazi huko Uganda (Uganda Monitor - gazeti la Aga Khan). Alirudishwa Nairobi (baada ya kuandika mamabo ambayo hayakumpendeza Makofia M-7) kwao Kenya kuendelea na gazeti la Daily Nation na The East African (yote ya Aga Khan).

    Insidentali, Anon, soma Charles Onyango Obbo alivyoandika kuhusu midia autletisi za Bongo: Let's face it, the Tanzania media is not being very neighbourly....katika toleo la hivi sasa la The East Africa.

    ReplyDelete
  8. This guy makes me buy the daily news paper, he has such a unique and humorous way of looking at things!! Before discovering his column i used to read kenyan news papers just to get a lighter view of issues, but now....Way to go bro!!

    ReplyDelete
  9. Ni kweli ni mwandishi mzuri hilo halina mjadala. Ila kama kweli aliandika makala kutetea kitendo cha festi ledi kwenda kwenye sherehe ya kijinga ya Mswati basi hapo alichemka. No way ufirauni ule wa Mswati unaweza kukubalika.

    ReplyDelete
  10. Watu wanaomlinganisha huyu jamaa na Charles Onyango Obbo wa daily nation nadhani hata hamjui kuchanganua uandishi wa habari na maswala ya kisiasa yanayoikabili Tanzania kabisa. Hakuna mwandishi wa habari bongo ambaye unaweza kumfananisha na Obbo, kwani kama angekuwepo, tungesikia ameshawekwa lupango mara kibao ana kesi kibao za kujibu zinamsubiri. Huyu jamaa ameandika habari ya kumtetea mama Salma Kikwete kwa ziara yake ya Swaziland ndio mwamlinganisha na Obbo? Pamoja na heshima zote nilizonazo kwa waandishi wa habari wa Tanzania, lakini nafikiri wameachwa sana kitaaluma na kiupeo na wenzao wa Kenya na Uganda. Mfano mzuri ni ile press conference waliofanya na Kikwete alipotoka USA. Wakati nchi ina matatizo sugu kama ya maji, umeme, shilingi inashuka thamani kila siku,taarifa kibao za wakaguzi wa mahesabu zinawashika wahasibu wa serikali, wakina Prof. Mahalu/Muhalu(balozi aliyekua Italy) wakitembea wanacheka, lakini rais hakupewa muda mgumu katika kutueleza nchi inakwenda wapi, badala yake tunaambiwa safari yake ilikuwa ya mafanikio sana. Mwekezaji gani wa marekani atakuja Tanzania kama hali ya umeme itaendelea kuwa ya kubabaisha kama hivi leo? Ushirikiano wa Africa Mashariki unakaribia ku-idhinishwa miaka michache ijayo, Tanzania katika hizi nchi tatu ndio inaonekana kabisa labour force(samahani kwa kutumia kidhungu lakini nataka nisipoteze ujumbe) ni inferior kwa hizo nchi mbili, na wala hatuoni mikakati ya msingi ya muda mfupi, wa kati na mrefu ya kurekebisha hayo mambo! wao ni viongozi kazi zao haziwezi kuchukuliwa, lakini sisi wananchi wa kawaida ndio tutakao umia, serikali ilitakiwa ifanye juhudi za kuyashughulikia mambo kama hayo. Hivi vitu muhimu ndio waandisha wetu wa habari (Michuzi ukiwa mmoja wao) mngetakiwa mnamuuliiza rais na mawaziri wake, mpaka atoe majibu yanayoeleweka, na asipotoa kama hivi juzi kwenye kubadilisha baraza la mawaziri, mnamshikia bango mpaka aone umuhimu wa kulielezea taifa sababu za msingi. Kabadilsha mawaziri kamili kumi na manaibu nane, sio bure, kwahiyo longolongo ziishe na waandishi wa habari fanyeni kazi zenu.

    ReplyDelete
  11. Adam uli support mama kikwete kwenda kwenye ushenzi wa kudhalilisha wanawake, wasichana na watoto? huu ni usenge na upumpavu.watoto wanakaa uchi ili mfalme achague totoz la kutuliza nyege.Kama wewe ni mwanaume wa msimamo...mpeleke mtoto wako kwenye usenge huu mwaka kesho mwezi wa 7, ni ujinga, ukimwi na ufirauhuni.Tunampenda kikwete, akikisea tumsahishe, tusimlambe miguu wakati wote.Adam wewe mlevi, JIREKEBISHE NIMEKUDHARAU SANA

    ReplyDelete
  12. I, too, enjoyed his articles on the newspapers while in Bongo. I was equally delighted to listen to his taken on Media in Africa on BBC Radio 4 a year or so ago (Needless to say I heard but only the part he interviewed Mengi whilst driving. I reckon it was a 4-part series. Does anyone know where I could access the whole series?). He needs to be commended for his insightful perspective on life in Tanzania. Pongezi nyingi, Luse.

    ReplyDelete
  13. I like Lusekelo articles too,he is funny and drives points home at the same time. There was another dude writing a column in Sunday News, alikuwa anaitwa Wilson Kaigalura na column yake ya " Yours Truly" . Kuna mtu anajua jamaa anaandikia gazeti gani nowadays? Michuzi should have more information on this.

    ReplyDelete
  14. adam umechemsha kuuunga umalaya wa mswati, usikubali njaa yako ikuondoe kwenye maadili, nani atapenda mtoto wake ajianike uchi ili mswati amfanyie mbaya?...simamia ukweli

    ReplyDelete
  15. b gates feki wewe ndo umechemsha. Tukianzia na jina lako, unaonesha dhahiri we ni limbukeni. halafu inaoneha umekurupuka tu, kufuata upepo wakati hata yaloandikwa na Lusekelo hujayasoma (kama ulisoma yalikuwa kwenye gazeti lipi; achana na tarehe, sema tu lipi) halafu mchemsho wako mkubwa ni pale wewe unaposahau ukeketwaji wanawake huko Bongo, ambapo Mswati na wenzie Waswazi hawajatia neno, kwani ni mila (potofu) ya nchi ingine, isiyowahusu. Na je, b gates, wewe unayechapa nje kila siku msichana mpya (kwa kificho) una maana ni bora kuliko Mswati anayefanya hadharani, tena kwa uhalali? Wabongo acheni hizo. ya kwenu yanawashinda, mnajifanya kujua kurukia ya wengine. Tafuteni umeme kwanza kabla hamjarukia ya watu. Limbukeni wakubwa nyie, hasa wewe b gates na watu dizaini yako.

    Lusekelo achana nao hao. Sie tulioko huku tunajua wewe huna mshindani hapo Bongo, hasa ukizingatia mtu kama lugha haijapanda (kama maimuna b gates)kuchekesha kwa kimombo si mchezo, wao wenyewe wanakwambia hivyo.

    Halafu nyie TAMWA na mnaojifanya wanaharakati, naona mmeishiwa sera na mnataka kuhalalisha kijanja pesa za wafadhili mnazozila bila kufanyia yale yalokusudiwa. Nyie TAMWA mnajua fika kwamba wanachama wote wamewakimbia kwa sababu hawaoni faida ya hicho chama. Hivi ni lini mtaanza kutetea waandishi wa kike hapo Bongo ambao asilimia 80 yao ni deiwaka na wanafanya kazi katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na kunyanyaswa kijinsia??? Kama alivyosema Lusekelo, ni lini nyie mkawa mawakili ya haki za mwanamke badala ya kuwa mawakili wa haki za mwandishi mwanamke? Acheni kuingilia kazi za watu kwa kisingizio eti wanawake. Mkomboeni mwandishi wa kike wa Bongo kwanza kabla ya kurukia yasiyowahusu na msiyoyajua. Hamasisheni kila mwandishi mwanamke awe mwanachama, pigeni vita waajiri wasiotaka kuwapa ajira, wapelekeni shule (sio mmoja mmoja, tena kwa kujuana)na pia muanzishe gazeti la kinamama kama wanavyofanya vyama vya waandishi wanawake kama wa Swaziland ambao (ajabu!) wala hawana neno na mila ya Mswati. Oneni haya na muyazingatie hayo kama mnataka kurejesha heshima ya enzi zile za kina Rose Kalemera, Fatma Aloo, Leila Sheikh, Halima Shariff, Jamila Mwanjisi, Agnes Kabigi, Irene Bwire, Jaquiline Liyana na wengine waliobobea lakini wamewatema. Najua mtashangaa lakini japo tuko huku tuna data kibao za kuwaumbua, ila basi tu. Na wewe b gates feki koma ujinga wako. kama mwanamme/mwanamke kweli jitokeze jitambulishe na wewe tukuchambue. Samahani kama nimewakwaza, lakini nimeona mficha maradhi ugonjwa utamuumbua. Na wewe Michuzi upuuzi kama huo wa Maimuna b gates uwe unafuta. Unachefua ati...

    Ndimi mwanachama wa TAMWA wa enzi hizo TAMWA ilipokuwa TAMWA.

    XXX

    ReplyDelete
  16. Arrest Abby Kandoro!
    Adam Lusekelo
    Sunday News; Sunday,October 08, 2006 @00:05

    lUSEKELO TUNAZIFAGILIA KAZI ZAKE,HEBU ONA HII

    SOMEONE should arrest Dar Regional Supremo, Abbas Kandoro. And I mean now! The guy should be arrested and be detained in Mafia Island -- just like they did in the olden days of colonial dictatorship.

    The repressive law is still there and Abby should be hauled in for competence. I mean it! He should be arrested under the Preventive Detention Act which basically forbids competence.
    Over the years Bongo has been promoting mediocrity. This has been taking place for such a long time. If someone goofs in one job, then he is promoted to another job to go and goof again.

    I have been on trips in foreign lands. That story will be told in the future. Because the moment I arrived back to my beloved Bongo there was something disturbingly normal.

    Later I found out that there has been a clean up campaign in Dar, courtesy of Abby Kandoro. People have been making noise about the unfairness of the Dar regional honchos.

    This is very dangerous. Kiosks have been pulled down. Some of them have collapsed voluntarily the moment they saw Abby with his green fatigued boys.

    There was our councillor in Ubungo who plotted to have his kiosk to be left untouched. The green fatigued boys hesitated a little, but then the ordinary wananchi pulled the thing down.

    I went for a haircut, the 'Cutz' salon was not there. I hear the owner pulled it down and went to a nearby 'gongo' place to get himself bombed in frustration. Most vibaka thugs are crying foul. They have not found alternative places to hide and mug passer-byes.

    So they claim that Abby Kandoro and his group should be sacked for competence. The most annoying thing is he has not spoken anything about it. Even Habitat Director General, Anna Tibaijuka has not spoken a word.

    Some say Abby Kandoro is looking for a job. But others counter that he already has a job. Other say that he wants to consolidate his job.

    "Why doesn't he do things like Makamba, speak all day and nothing happens." asked one former kiosk owner.
    "You mean Makamba did not have a speed governor in his mouth? I don't believe that he believed what he said. No wonder the cholera, the beggars and the kiosk guys ignored him." said another kiosk owner as they went on packing their stuff.

    ReplyDelete
  17. Annony 9:02:28 AM, ni vizuri ukaangalia kwa kina huo utamaduni wa Mswati, kufanya jambo hadhalani, sio kwamba ndio jambo jema hata USHOGA unafanywa hadhalani na umehalalalishwa nchi nyingi. Kuwa kwetu na mila mbovu sio tiketi ya FIRST LADY kutumia pesa za nchi kwenda kusupport udhalilishaji wa mwanamke na hili ndio tunalipigia kelele kwa nguvu zetu, mtu gani mwenye kuweza kuwatosheleza wake 17, au wake 60 kama baba yake, nchi yenye maambukizi ya ukimwi kwa 40%, na kama sikosei ni ya pili duniani kitakwimu baada ya Boswana, Umasikini uliokidhili.B GATE amefanya makosa kutumia matusi ila amesema ukweli. tuchanganue MILA NZURI NA MBAYA, tuache ushabiki kwa VIONGOZI, tunakuwa na mengi ya kujibu KWA Mwenyezi Mungu. Kesho anaweza kualikwa na U.S.A VICE PRESIDENT, kuhudhulia harusi ya binti yake ambaye ni LESBIAN na baba yake anasupport ushoga na amekuwa akipingana G BUSH, kwa kuwa ni kitu kimekubalika kikatiba ni mila yao pia, MAMA SALMA akialikwa nae aende kwa sababu ni mualiko wa kitaifa? kumbuka watu wanakufa atuna dawa mahospitalini na KODI ya wananchi inatumika vibaya hata kama huyu ni MAMA YAKO MZAZI ni bora ukanyamaza.

    ReplyDelete
  18. Hayo ya Uswazi yamepitwa na wakati. Leo hii kuna taasisi mbalimbali zinazotekeleza wajibu wa kulea mabinti zetu, na kuwatayarisha kushiriki kikamilifu kama wakina mama. Hivi kazi za mashule na madhehebu yetu ni nini, kama sio kutekeleza huo wajibu?

    ReplyDelete
  19. Ni wazi lusekelo ni mwandishi mahiri. ila kama alimtetea mama Salma, hapo nafikiri mwenyewe anajua anafanya nini. Brain kama yake haiwezi tetea lakini si unajua tena Dunia ya leo."RELATIVISM" ndio mtindo wa maisha. Simlaumu ila mama Salma kachemsha na kwa misingi ya kimaadili sijui ni maelezo gani yanaweza kumuweka pazuri.
    Sikusoma alichoandika ila niseme tu katumia umahiri wake kielimu kughilibu maadili.

    ReplyDelete
  20. It was refreshing to see Adam Lusekelo. I used to read his articles in late 80's and early 90's b4 I left Bongo. I used to work at Tea Blenders (Majani ya Chai pale Gerezani) and every Sunday I used to buy Sunday Papers just to read his articles. I guess he is still writing!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...