mh. profesa simon mbilinyi sasa ni balozi honorari wa nchi ya croatia hapa bongo. anaonekana baada ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho kwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. dk. asha-rose migiro hivi majuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AHADI ZA KIKWETE ZILIKUWA ZA KWELI, HAKUMTUMIA TU ASHA-ROSE MIGIRO. KWELI BWANA KAMPA CHEO. PUNDE ALIPOPATA URAISI.

    ReplyDelete
  2. mbona mbilinyi anaonekana kalala..???

    ReplyDelete
  3. ni kweli kroashia tulitakiwa tuanze nao ushirikiano. Ila huyu profesa mke wako mkroashia, nini? Maana nakumbuka alikuwa na mke mzungu.

    ReplyDelete
  4. Binti wa Mbilinyi yule NALI hana noma totos ana-act kizungu, muulizeni ALI MAXI atawapa data zote.

    ReplyDelete
  5. BWANA MICHUZI,
    HII BLOG SASA INACHUKUA MUDA SANA KUFUNGUKA. FANYA MAMBO MZEE........

    HAPO KULIA UMWEKA 'TOVUTI MUHIMU' ZA AKINA KIKWETE NA SHEIN-MIE NASHAURI UZIONDOE-HIZO SIO TOVUTI MUHIMU KWA WATU WANAOTEMBELEA HII BLOG.. KWA MAONI YANGU

    ReplyDelete
  6. Kuna tofauti gani baina ya ajenti wa nchi ya nje na balozi honori, kama alivyo Prof. Mbilinyi?

    ReplyDelete
  7. Nakuunga mikono na miguu anony wa 5:33. Hii blog sasa imekuwa kimeo katka kufunguka. Au Michuzi una up load mafaili makubwa mno? Ukichanganya na u-slow wa internet ya Bongo ndo balaa kubwa. Pia kama alivyoshauri anony hapo juu, Kikwete Shein, na makala nyingine za miezi sita iliyopita hazina mpango, pengine nazo zinachangia kupunguza speed. MK naelewa unalea, lakini binti akilala tafadhali mrekebishie michuzi tuendelee kufaudu siye. Amina

    ReplyDelete
  8. MICHUZI MBONA BLOG YAKO INACHUKUA MUDA KUFUNGUKA NINI TENA MBAYA?.

    ReplyDelete
  9. Ni kweli wandugu hata mimi nilishaona Tangu takribani week 2 hivi hii blog imekuwa slow sana. Cha ajabu hizo habari hapo kulia haziko current

    ReplyDelete
  10. Au wabaya wa michuzi wameshatia mkono wao humu? Nasema washindwe kwa jina la YESU

    ReplyDelete
  11. kama nimeelewa vibaya nisahihisheni jjamani,
    hapa maana yake ni kuwa Prof Mbilinyi anaiwakilisha nchi ya croatia hapa nchini,kwa maneno mengine ni kuwa yeye ni balozi wa croatia hapa nchini au??
    inamaana kateuliwa na rais wa croatia??

    ReplyDelete
  12. Nashukuru kwa ushauri mzuri mlio utoa, Ata mimi nililiona hilo swala ila ndio muda sikuupata. Kwa Niaba ya Issa Michuzi napenda kuwahakikishia blog hii yenu muipendayo imerudi kama mwanzo yaani inafunga kwa haraka kama mwanzo.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  13. NI KWELI MICHUZI NAOMBA KUSAPOTI WATU HAPO JUU.
    BLOG YAKO SIKU HIZI IKO VERY SLOW, INACHUKUWA MUDA MREFU KU-LOAD. VIPI HUJALIPA FEE KWA GOOGLE?

    ReplyDelete
  14. Hivi yule binti wa huyu baba NALI MBILINYI yuko wapi siku hizi? na Je ameolewa?

    ReplyDelete
  15. Hayo ma-viti ni makubwa mno. hayafai kwa ofisi.

    ReplyDelete
  16. Bila shaka tatizo la ugumu wa blog ya michuzi kufunguka linaelekea kupata utatuzi. Labda ni kweli zilikuwa hizo link za kina Kikwete, Shein na makala kibao za miezi kadhaa iliyopita. Michuzi na MK endeleeni kuboresha kablog ketu haka. Michuzi hebu mwulize Joni mwaipopo yuko wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  17. Sijui ni matatizo ya kuukimbia umande au nini.SIMONI MBILINYI ATEULIWA KUWA BALOZI WA CROATIA NCHINI TANZANI!!!!!!.Kwa maana hiyo ameteuliwa kuwa mamluki ili kuisemea Croatia badala ya Tanzania?Hivi ikitokea mgongano baina ya Tz na Croatia huyu Mbilinyi atakuwa upande gani?Jamani wanablogu nitoeni gizani mie.Samahani msinitukane ni kwa ajili ya kutaka kuelewa.Chonde2.

    ReplyDelete
  18. Jamani,

    Huu utaratibu ni kawaida tu. Nchi inakuwa haina pesa za kumweka balozi wakati mambo yanayoendelea hapo labda sio makubwa sana. Tanzania tuna balozi wa namna hiyo
    pale Holland na labda nchi zingine.

    Nafikiri prof. Mbilinyi kasoma na kuoa Croatia kwahiyo anaijua nchi hiyo vizuri.

    Kuhusu Uzalendo unabaki wapi, yeye ni Mtanzania na kuwa mwakilishi
    wa Croatia ni kazi tu sawa na wewe kuteuliwa au kupewa kazi kwenye
    shirika la Makaburu hapo Dar, au kuwa mfanyakazi wa EU hapo Dar nk.

    ReplyDelete
  19. Asante sana anony wa 10:31am.Ama hakika nimeielewa mantiki nzima ya cheo cha BALOZI WA HESHIMA.Blog hizi zinaelimisha.

    ReplyDelete
  20. MHESHIMIWA VIPI BWANA, HII BLOG YETU NDIO INAFANYA WATU WANA KEEP TOUCH.
    KUNA SWALI LILIULIZWA KUHUSU NALI MBILINYI, MIE NAMFAHAMU NIKATOA JIBU KWA MUUSIKA ALIYEULIZA SWALI. LAKINI HUJAPOST MAJIBU YAKE MPAKA SASA KWA NINI? MAANA HATA HUYO MTU HAPO ATAONA MBONA HII BLOG SIYO RELIABLE TENA? MAANA SIKU ZOTE WOTE TUNAAMINI HII BLOG NI VERY RELIABLE SOURCE OF INFORMATION. USITUANGUSHE BWANA. KULIKUWA HAKUNA MATUSI ILA MAJIBU YA UHAKIKA KUHUSU HUYU BINTI. KULIKONI BASI WAAMBIE WATU WASIULIZE MASWALI. MAANA HAWATAPATA MAJIBU TENA.

    ReplyDelete
  21. Ni kweli hii blog imeanza kutokuwa reliable.Hivi maoni yetu mpaka uyapeleke state house yasomwe ndipo uyatoe michuzi? Blog hata USA Bush huzitumia sana kupata data na kujielimisha na kumsaidia.Sometimes anasaidiwa vilevile.Sasa Michuzi kama watu wanataka kukudhibiti kwenye hii blog tutaihama watu wakose source of some useful information.

    ReplyDelete
  22. Je Prof kasamehewa ile skando ya mafuta? Hivi bado tunadumisha utamaduni wa kuwalea wabovu au yeye alikuwa mbuzi aliyetolewa kafara?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...