pamoja na matatizo yetu mbalimbali bongo tunajivunia rasilimali za kipekee duniani alotuachia baba wa taifa mwalimu nyerere - utaifa, umoja, upendo, amani na uvumilivu katika shida na raha. hapa makamu wa rais dk. ali mohamed shein akiagana na mwenyekiti wa tlp mh. augustine lyatonga mrema baada ya kufuturu nyumbani kwa makamu. kulia ni mkuu wa mkoa wa dar mh. abbas kandoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Tanzania jinsi wanavyoshirikiana katika kufuturu wangelikuwa wanashirikiana katika kuleta maendeleo nchi yetu ingelikuwa mbali sana.

    lakini mambo kama haya wanashirikiana ikifika maendeleo huruma zinapungua.

    ReplyDelete
  2. Lyatonga babangu hakuna kiti moto kwenye futari babangu, labda upitie mburahati ukitoka hapo kwenye futari sheikh.

    ReplyDelete
  3. Mbona Mrema amekonda sana! Mzima kweli?

    ReplyDelete
  4. Mfunguapo mapicha haya mazuri ya sherehe za futari jijini Dar na kwinginepo, napenda mjiulize swali hili: Hivi ni lazima kula futari walaji wakikaa kwenye mikeka mikeka au mazulia zulia? Kwa nini wasikae mezani mezani? labda sijui maana yake hasa. Napenda kuelemishwa na kukombolewa na tatizo la swali hili ambalo hugonga gonga akilini mwangu.

    ReplyDelete
  5. MREMA: Aisee Ali, huu mtori lazima mtakuwa mmenunua kwa mcha mchaga tuu.. yaaani nimefurahi kweli babangu. Na ule uji pia leo nimekumbukia Moshi enzi za uto-utoto.

    SHEIN:Usijali August usijali. Kwetuu Pemba pia tuna ndizi vilevile. Nashukuru karibu tena.

    ReplyDelete
  6. Anony wa kwanza nakubaliana na wewe, hizi futari sijui nini ni unafiki tu. Kama kweli wangekuwa wanashauriana mambo ya maana na maslahi kwa taifa tungekuwa tunaona mawazo ya kujenga nchi yanakubaliwa.
    Michuzi be careful kumsingizia Mwl Nyerere, katika Tanzania yetu ya sasa hakuna alichotuachia. Mtu aliyecharangwa mapanga kwa ajili ya elfu 30 au anayetembea kwa miguu toka K/koo hadi Mbagala ana amani gani? Dar siku hizi inzbidi urudi nyumbani saa 12 sasa hapo amani iko wapi. Na hilo giza tulilomo sasa nayo ni upendo uvumilivu? Amani,upendo, uvumilivu sijui nini tena hayo yote yapo katika level binafsi.

    ReplyDelete
  7. Michuzi webste iko slow jamani!

    ReplyDelete
  8. Zanzibar adopts first-ever anti-HIV/AIDS policy

    ZANZIBAR, Tanzania (AFP) - Zanzibar's parliament has passed the islands' first-ever anti-
    HIV/AIDS policy but rejected conservative Muslim demands to shut all bars and ban skimpy clothing as part of the strategy. Lawmakers on the semi-autonomous Tanzanian archipelago also refused to endorse Muslim calls to screen all visitors for the virus that causes AIDS and segregate HIV-positive Zanzibaris from the non-infected population.
    By a vote of 40 to zero, with 20 opposition MPs who supported the bill abstaining for political reasons, the legislature adopted the "Zanzibar National HIV/AIDS Policy."
    The plan calls for a house-to-house anti-HIV/AIDS educational campaign, including instruction on how to prevent the disease in school curriculum and encouraging the use of condoms, Zanzibari officials said.
    "The immediate and best solution is to join hands and increase HIV/AIDS education to all areas," said Chief Minister Shamsi Vuai Nahodha, adding that the government could not support suggestions that might violate human rights.
    As such and keeping in mind the islands' dependence on tourism, he urged the rejection of calls from some conservative Muslim lawmakers to outlaw bars and pubs, ban "inappropriate clothing" and introduce mandatory screening.
    "Introducing laws to force people to have their blood screened for HIV/AIDS, to control people with HIV/AIDS, to ban all bars on the islands, to have all patients in hospitals and visitors, including tourists, checked, can be a big problem," Nahodha said.
    "I do not believe they can be the solution to combatting HIV/AIDS," he said.
    About 0.6 percent of Zanzibar's overwhelmingly Muslim population of some one million are HIV positive, according to the health ministry.
    But there are fears the disease will spread and some conservative Muslim clerics say moral decay, which they blame on the influx of foreign tourists, alcohol and drug consumption, has put Zanzibaris at greater risk.
    "The government must be serious in the fight against HIV," said conservative Muslim lawmaker Abdullah Juma. "Those women who move half-naked and the issuing of licenses for bars in Zanzibar should be stopped.
    "All bars in Zanzibar must be closed down," he said. "Only this will show that the government is committed to fighting HIV."
    Another, Ali Mohamed, said the government had a duty to segregate people who are HIV-positive to protect those not infected.
    "HIV/AIDS is not a disease but a curse from God for increasing sins," he said

    ReplyDelete
  9. Kukonda kwa Mrema kwaonyesha na kukauka, kunyong'onyea, na mwisho kufilisika kwa itikadi.

    ReplyDelete
  10. Lau kama nisingekaa na huyu mwenye masoksi yanukayo!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Kweli naunga maoni ya jamaa hapo juu, laiti mshikamo huu ungeendelezwa mpaka kwenye mambo ya maendeleo, Watanzania tungepiga hatua.

    Ni mambo yale yale ya kujifanya mabingwa kwenye ulaji huku mambo ya maana tunatawaliwa na siasa, ukabila na udini.

    Sijui tutaamka lini, inatakiwa vyama vyote vishirikiane katika kutuletea maendeleo. Badala ya kumkaribisha Mrema kwenye futari, wangemkaribisha pia kwenye kamati ya kupambana na majambazi ili awasaidie.

    ReplyDelete
  12. Lyatonga Mrema pole kwa kufiwa na hawara yako.Mzee inasikitisha kwamba ulikosa muda wa kuhudhuria mazishi ya hawara yako.Bongo vigogo kibao wana mahawara kwa hiyo mzee usihofu wala nini.Hongera lakini kwa kujitolea kumsomesha mtoto ingawa unakataa kwamba si wako.Mzee wa TI-EL-P.

    ReplyDelete
  13. DUUUU!! JAMANI CCM SIYO MCHEZO JAMANI,YAANI WAMEMFANYA MZEE WA WATU KAMA VILE AMEBEMENDWA,MWILI UMECHOKA KAMA NINI AU NI DUA ZA WAISLAM AL-BADRI ALIYOSOMEWA NA WAISLAM AKIWA WAZIRI YA MAMBO YA NDANI INAMLA KAMA ANA NGOMA AU VIPI?

    JAMANI WANA bLGGER KUNA JAMAA HUYO ANAITWA ANONYMOUS SAID ANABOA SANA TENA SANA,KARIBU SEHEMU ZOTE KWENYE HII UKUMBI ANAANDIKA YEYE MPKA WATU WANAKOSA SEHEMU YA KUANDIKA COMMENTS ZINGINE PUMBA TUU

    INAONYESHA HUYU HANA KAZI KULA KULALA TUU NDIYO MAANA ANAPATA MUDA MWINGIN KUKAA KWENYE PC KUANDIKA MAMBO MENGI

    NATUMAI KIJANA UMENIELEWA PUNGUZA MANENO NA WENGINE WAPATE KUANDIKA

    ReplyDelete
  14. ndugu yangu BAP mimi ninavyoelewa ni kwamba utamaduni wa kukalia mikeka na mazuria ni wa kiarabu. siyo mikeka tu, ukiangalia hawa ndugu zetu hata viatu vyao wamevua, baraghashia vichwani na wanawake wamefunika vichwa vyao kwa ushungi. kumbuka kwamba dini ya kiislamu, futru nk vinaendana na tamaduni hizo. hata hivyo nadhani siyo lazima kufuturu mikekani, lakini ni uamuzi wao kukalia mikeka kwa hiyo wana hiari hiyo. wakiamua kupata futru mezani ni hiari yao pia. kwa hiyo naona tuwaachie wenyewe wakiamua mezani au mikekani yote ni sawa tu.

    ninao marafiki zangu ambao hawana sofa za kukalia sebuleni, siyo kwamba hawana uwezo wa kununua, la, ila ni uamuzi wao tu kukalia zuria.

    utamaduni wa kula kwenye meza na vijiko ni wa kizungu. na wewe kama unapenda kufuata namna hiyo, ruksa.

    ukija kwetu kuna vigoda na tunakulaga kwa vidole vya mkono. tunakunywa maji ya mtungini kwa kutumia kata (vibuyu) na hatutumiagi glasi wala hatuna friji.

    ReplyDelete
  15. Shingh'weng'we,

    Naomba nikuimbieko ka wimbo kafupi alakini kenye kina na mapana makubwa. Nakakumbuka miaka hiyo ya 1950's nikisoma kitabu cha kujifunza Kiswahili:



    Mayo. mayo, nabhulaga shingh'weng'we!

    Na wewe pia ukija kwetu kuna vigoda na tunakulaga kwa vidole vya mkono. tunakunywa maji ya mtungini kwa kutumia kata (vibuyu)!!!

    ReplyDelete
  16. halo mrema ana hali mbaya kiafya,afadhali arudi ccm wanaweza kumpa hata ukuu wa mkoa.kweli inasikitisha kumwona Lyatonga akiwa amekonda kiasi hicho

    ReplyDelete
  17. Hapana kumpa huyu mangi ukuu wa mkoa. Anafaa sana kupewa wadhifa wa balozi...tumpeleke Washington, DC, Amerika.

    ReplyDelete
  18. huyu mrema atarudi CCM maana njaa ishamuuma sana kapitwa na kula muda mrefu sio bure zitafutwa sababu fulani halafu na yeye atapewa kula tuu,Jamani kuna watu wankinyongo na balozi daraja kwa sie wengine tulio hapa muda mrefu tunaona huyu bora kuliko Nyang'anyi au hata Nyirabu

    ReplyDelete
  19. Mrema anajikomba sana kwa Kikwete siku hizi kwa kuwatetea waislamu kwenye hotuba akijua Kikwete atamtupia jicho la kumkumbuka kwenye ulaji.Mbatia wa NCCR naye kaanza hivyo hivyo.Askofu Gamanywa naye ni mwingine anayejikomba ili aendelee kubaki kamishna wa tume ya kudhibiti ukimwi na amekuwa akitumia gazeti lake la Msemakweli kujikomba kwa waislamu lakini ni tapeli. Alikuwa karibu na kibaka Sumaye. Alipoona Sumaye kaporomoka akamtoroka kichinichini sasa anajikomba kwa Kikwete kwa kuandika makala za kutetea waislamu lakini ni msanii na tapeli tu na yeye.

    Mkoa wa Kilimanjaro una wasanii wengi wanaovizia noti.Ukitaka kujua jiulize Kwa nini asilimia 90 ya wagombea Uraisi kwenye uchaguzi uliopita wa Tanzania walitoka mkoani Kilimanjaro.Wote walikuwa wanazengea Ruzuku tu wala si kwamba mkoa wa Kilimanjaro una wapizani wengi.

    Kikwete Chunga Mrema,Mbatia na Askofu Gamanywa walishaanza kujifanya wakereketwa wa waislamu. Matapeli hayo yanatafuta ulaji na hizo futari.

    ReplyDelete
  20. Kukaa kweli mkeka sio dini ni utamaduni. Hata kuvaa kanzu sio imani ila utamaduni tu. watu wa maeneo ya jangwani wanavaa kanzu halafu hawavai chupi, kaptula wala surali ili hewa ipite.

    Sasa tamaduni zilizo ambatana na imanai huchukuliwa kama sehemu ya imani.

    Kwa mfano wakristo wanafuata ustaarabu wa mzungu kwa sababu ukristo ulienezwa na watumishi wa kizugu

    ReplyDelete
  21. nakuunga mkono anony wa 1:52.kweli huyu Nyan'ganyi hafai maana hana msaada kwa wa Tz hapa wanapokuwa na shida.Binafsi niliwahi kuwa na problems and then nikawasilana na ofisi yake DC but sikupata msaadda wowote na wala hawakunipigia simu.sasa kama moja wapo ya kazi ya ofisi ya ubalozi ni kusaidia Tzn citezens wanapokuwa na matatizo iweje hawa watu wanakuwa na kiburi kiasi hicho??????? je wanamwakilisha nani hapo DC??? Kwa kweli ofisi hiyo inamfaa Lyatonga kwa maana huyo jamaa pomoja na mapungufu yake but ni mtu mwenye moyo wa huruma sana na ni mchapa kazi.

    ReplyDelete
  22. Wewe, Saa Monday, October 23, 2006 10:18:20 PM...Balozi Mustapha Salim Nyang'anyi sasa si Balozi wa TZ Amerika. Ni balozi wetu huko United Arab Emirates tangu 2002.

    ReplyDelete
  23. kwani unaona lyatonga nguvu za kuingia ikulu hana? kwa nini unapendekeza ubalozi? siasa za bongo vichekesho ukichoka unajisalimisha kama Lamwai, watakufikiria tu.

    ReplyDelete
  24. Balozi Mustapha Salim Nyang'anyi hayupo tena DC. Alihamishiwa United Arab Emirate mwaka 2002!!!!!

    ReplyDelete
  25. Lyatonga atashindania kuingia Ikulu hadi lini? Amefilisika ki-itikadi na kisera!

    ReplyDelete
  26. Lyatonga amefilisika ki-itikadi na ki-sera sera!

    ReplyDelete
  27. Jamani! Mrema ana Ukimwi nini? hebu cheki mikono iliyokuwa membamba1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...