wengi wetu tulizaliwa hospitali hii ya osheni rodi ambayo sasa ni taasisi ya taifa ya saratani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Mizoou blog yako imekuwa nzito kinoma mjomba inachukua muda mwingi kufunguka, Punguza uzito ulio kuwapo mwambie admin wako atajua ninacho sema.

    Kingine usikose kuangalia game leo Man utd na KOP. Mzee wa The red devils.

    ReplyDelete
  2. Kanisa na Msikiti!

    ReplyDelete
  3. Naongezea:

    Hivi ninyi Wakristo na Waislamu, lini mtaacha kupiga makengele makanisani na kupaaza sauti kwenye vinara vya miskiti ili kuiita waumini kuudhuria ibada zenu? Kuna kitu siku hizi kinaitwa saa; chavaliwa mikooni, chawekwa ukutani na mezani, ki-kwenye vilongalonga vya baadhi ya matajiri, kinasikika redioni na televishenini. Nendeni na wakati. Tafadhalini sana tena saaaaaaaaaaaaana msipige makelele yanaudhi wengine, hasa wagonjwa!

    ReplyDelete
  4. Michuzi,
    Hii picha nitakuomba, maana na mimi nimezaliwa mahali hapa. Na sijui kwanini, sijaingia Ocean Road tangu nizaliwe. Ni kumbukumbu nzuri sana kimaisha!

    ReplyDelete
  5. Born Again Pagan - Umezungumzia sualka zuri- Ingawa haliendeana na hiyo picha juu- mimi bado nakuunga mkono. Sioni sababau ya kuendelea kupiga kengere au kutumia kipaza sauti kisikitini. Ni kweli inabidi tuwende na wakati- na sasa technology ni nzuri kwani hatuiitaji tena kukumbushwa wakati wa kusali au kuswali

    ReplyDelete
  6. Kweli wajameni blog imekuwa nzito kufunguka. Inachukua muda kufunguka ata hapa kwangu nina fast connection lakini bado tu. Fanya makeke michuzi

    ReplyDelete
  7. Kwenye picha nimeelekezwa wapi kuna catering, church, mosque & canteen - yaani huduma za maandalizi ya chakula, kanisa, msikiti na mahali pa chakula. Chakula na hospitali vyaenda pamoja. Lakini kanisa, msikiti na hospitali (ingawa wengine wakifa huombewa), hakuna uwianio. Kwa kuwa wametumia maneno ya Kiingereza, ngoja niandike kwa kimombo kidogo: There is what is called stupid talk (when the contents do not match with the context), and crazy talk (when a different context is conscripted to obey another context).

    Huyu ni Born Again Pagan akisema hadi tuonanapo tena, kwaheri!

    ReplyDelete
  8. We Michuzi umezaliwa ocean road mwaka gani?
    Na OR ilianza kuzalisha lini?

    ReplyDelete
  9. yallah! fmtimkubwa naomba nilinde na anony wa juu yangu...

    ReplyDelete
  10. anony 17:16:57pm ni kweli wikiendi hii blogu imekuwa nzito kiasi. jamaa walitambua hilo, wakalisema na sasa wamerekebisha na mambo mswano

    ReplyDelete
  11. Kumbe Maggid meti wangu, miye pia nilizaliwa hapo Osheni Rodi.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  12. Kuzaliwa ocean road ni sawa tuu na kuzaliwa sehemu zingine. Siku hizi imekuwa kama ni fasheni, hata aliyezaliwa sigimbi au dinduma pia anajifanya lazaliwa ocean road.

    ReplyDelete
  13. NA KWELI BWANA, OSHENI RODI OSHENI RODI---TOKENI HAPA. MNAONA NDIO UJIKO KUZALIWA OSHENI RODI??? JE WALIOZALIWA UGHAIBUNI JE, MBONA HAWATAMBI??? KUZALIWA NI KUZALIWA TU, WALIOBAHATIKA KUZALIWA HOSIPITALI NZURI WASHUKURU WAZAZI WAO KWA UWEZO HUO.

    ReplyDelete
  14. Mliozaliwa Osheni Rodi, Osheni Rodi, Osheni Rodi, mlitaka mzaliwe wapi? Mngechaguaje pa kuzaliwa? Kuzaliwa huko Osheni Rodi hakuna shidi not be consitruudi kuwa mna aikwu zaidi ya wale waliozaliwa kijijini miembeni, mama zao wakawazaa, kama vile nyamela, bila anastizia!

    ReplyDelete
  15. Kuna ubaya gani mtu kukumbuka alikozaliwa? Kuna wengine sio tu walikozaliwa, wanaona aibu kutaja hata vijiji walivyokulia. Mtu kwao, ni vema akajivunia.

    ReplyDelete
  16. Kwani kuna ubaya gani mtu kukumbuka alikozaliwa? Kuna wengine,sio tu wanaona aibu kutaja vijiji walikozaliwa badala ya kukumbuka na kujivunia asili yao.

    ReplyDelete
  17. Jamani narudia tena samahanini,
    Michuzi umezaliwa mwaka gani na hospitali gani?
    Mbona sijapata jibu mpenzi?

    ReplyDelete
  18. HALAFU HAWA WATU WALIOZALIWA OCEAN ROAD WANAJIFANYA WAJANJA SANA ETI KWA SABABU HAWAKUJA DAR KUTOKA MIKOANI!!! MIKOANI PIA KUNA HOSPITALI NZURI TU..MOUNT MERU,KCMC, BUGANDO NK MBONA HAWAJIDAI MWISHO MTAKUJA KUSEMA NA SHULE OOH TAMBAZA, AZANIA... NI ULIMBUKENI TU WA MAWAZO UNAOWASUMBUA!!!

    ReplyDelete
  19. Maggid, tatizo sio kukumbuka kuna kiasili cha kujiona wewe ni bora eti tu umezaliwa hapo OR, wakati mtu hajichagulii mahali pa kuzaliwa mbona kuna watu kibao wamezaliwa ng'ambo na hatuwaoni wakipiga domo kama nyie wa OR??

    ReplyDelete
  20. Kwa kuwa ni majivuno kuzaliwa Osheni rodi, basi mliozaliwa hapo mtafia hapo kwa namna moja au nyingine, si ndiyo????????????????

    ReplyDelete
  21. Nani kajidai kwa kwenye hizo posti jama? Mbona viroho korosho!!! Mimi pia nimezaliwa Ocean Road Dr akiwa Andrew, enzi hizooo...Hatujidai, tunaelezana. Hatukuchagua kuzaliwa hapo, wazazi ndio walichagua:-)

    ReplyDelete
  22. Yafaa sana vyama vya siasa viundwe vikitenagnaisha wanaojiona na wasiojiona wala kupenda makuu kwa kukoga wengine.

    ReplyDelete
  23. Yafaa sana vyama vya siasa viundwe kulingana na wanaojiona na kupenda makuu kwa kukoga wengine na wale ambao wanapinga sifa hizo.

    ReplyDelete
  24. Jamani tunaongozwa na mtu aliyezaliwa kwa wakunga wa jadi.
    Sasa kuna ubaya gani na umuhimu gani ulipozaliwa au kukulia?
    Wewe Michuzi kama ulizaliwa kama JK poa kabisa! Tena ndio watu wenye vismart kweli nyie basi kama hawajui!

    ReplyDelete
  25. Hata JK atasema kuwa alizaliwa O/R Hospito ingawa tunajua alizaliwa huko Lugoda.

    ReplyDelete
  26. Stekiholda: Tunachosema ni mtu kukumbuka mahala alikozaliwa, hata kama umezaliwa ughaibuni kuna ubaya gani kuikumbuka hospitali uliyozaliwa huko ulaya au Marekani. Ni suala la kumbukumbu ya maisha tu. Ni vitu vya kawaida sana.

    ReplyDelete
  27. hebu toeni upuuzi wenu hapa, kuzaliwa ocean road so what?? ndio mna brain nzuri au?? this is nosense. and by the way you can end up at OR with severe advanced stage cancer of da prostate if not lung carcinoma!!

    ReplyDelete
  28. Tuzungumzie Umoja wa Afrika Mashariki unaoandaliwa na wakina KKK (Kaguta-Kibaki-Kikwete!

    Mimi binafsi siutaki kwa sababu: MOJA, dharau ya hao wa-Kenya wa-Uganda bado inaendelea kichini chini kwa visingizio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujidai kuwa elimu yetu ni duni sana. Tunaweza kufanya vyetu (na kuimarisha elimu yetu) na wenzetu wa Kusini na huku tunaheshimu udugu wa karibu yetu na Kenya na Uganda! PILI, tujenge utawala bora katika nchi zetu: Uganda iache vishawishi vya kujitawala kimajimbo (kunakoongozwa na falme za jadi baguzi). Ni lazima ilete uelewano na amani ya kudumu (peace and security arrangement and management) huko Kasikazini ili wa huko Kasikazini wajione ni wananchi wa Uganda pia (ndio maana walimkataa M-7 katika uchaguzi uliopita. Kenya bado inatafuta moyo wa uongozi (a search for a heart). Tanzania bado tuna tatizo letu na ndugu zetu wa Zanzibar (Zanzibar Factor) hasa katika kisiwa cha Pemba. Wapemba hawana budi kujiona kuwa ni sehemu ya Zanzibar/Tanzania. TATU, gulio la wazi (globalisation) linajaza vya kisasa kutoka nje; hatutengenezi na hatuuzi vingi vyetu nchini, na tutajenga soko kubwa kwa hivyo vya nje. Ni vigumu sana kwa vyetu kupenya masoko yao---hata kama ni kwa mipango ya AGOA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...