KUNA MDAU KANITUMIA UJUMBE HUU TOKA LANDAN NAMI KAMA KAWAIDA YANGU NAUMWAGA KAMA ULIVYO PAMOJA NA PICHA YAKE KATIKA KUTEKELEZA AHADI YANGU YA KUPOSTI CHOCHOTE TOKA POPOTE CHENYE MARASHI YA MAENDELEO. PIA NAPENDA KUWASHUKURU WADAU WA AINA HII WENYE KUONESHA IMANI NA BLOGU YETU HII. ASANTENI SANA KWA KUNITIA MOYO, NAMI NAHIDI TENA KWAMBA SINTOWAANGUSHA...



Michuzi,
Pamoja na ku-promoti wanamziki, Defunkadelic imekuwa ikipanga kutengeneza pamba kwa muda mrefu sasa. Niko katika harakati za kukamilisha website kwaajili ya huduma ya pamba za defunkadelic (www.defunkadelic.co.uk), natumaini itakuwa kamili wiki kadhaa (3 hadi 6) zijazo. Hii ni moja ya design ya logo niliyochapisha. Imeonekana kupendwa na wanaume kwa sana hapa mitaani London, kwahiyo niko katika harakati za kuwafurahisha dada zetu pia.
Defunkadelic ni ‘registered’ na ni ‘trademark’ pia. Ni kampuni changa, lakini ina mikakati mikubwa. Jina la kampuni limetokana na upendo wa aina ya muziki wa ‘Defunkadelic Jazz’. Ni jina ambalo ni rahisi kushikwa na kukumbukwa na watu wanaojua historia ya muziki kidogo, sana sana muziki wa kimarekani. Wengi wetu tutakua tumesikia miziki yenye mizizi kutoka Funkadelic Jazz (bila kujua). Kwa vijana wapenda hip hop, miziki mingi imetokana na Funkadelic Jazz. Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu Funkadelic Jazz, hebu jaribu ku-google na utafute miziki yake. Ukisikiliza funkadelic jazz, kwakweli utajua unasikiliza miziki ya nguvu (Kama Bootsy Collins au George Clinton, au Parliament Funkadelic (P-Funk kwa kifupi, kama prodyusa wetu wa nguvu hapo Bongo). Once you go Funkadelic, you cant go back!! Snoop na Dr Dre. Wametengeza majina kutoka Funkadelic Music (wenyewe wakaita G-Funk au Gangsta Funk).
Website ikiwa tayari, itatoa huduma nchi mbalimbali. Lengo langu ni kuhudumia watu wa asili mbali mbali. Dada zetu walio bongo, wapenda kujipamba, nitaweka spesho service kwaajili yenu (hata kaka zangu pia). Kwasasa naweza patikana (
info@defunkadelic.co.uk) – Maswali/michango yote ya pamba tafadhali naomba yaelekezwe hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Komfuzed ! unauza nguo ama muziki ? We nani na kwanini tununue nguo zako ?
    Michuzi kuwa mangalifu na wanao advataiz cheaply na bila skillz zozote !
    Chao

    ReplyDelete
  2. it's a good idea, but perhaps we should have waited for the launch date to talk about it.

    otherwise it remains an idea, just that.ever heard about daraja la kigamboni brother?yeah, hope you what i'm saying.it's never been a reality, so far at least.

    ReplyDelete
  3. michuzi umejaribu kukongoli kwenye hicho kiunganishi cha defundelic,mbona kinanipeleka kusikohusika na nguo wala muziki.otherwise ni vyema kama kuna mbongo atatoa pamba ili tuweze kukimbia pamba za kina TOMMY HILFIGURE.

    ReplyDelete
  4. Ungesubiri basi hadi utowe ndio uombe ku promote humu hizi sasa kwetu it is just other idea tuu .you only pre advatise kama umekwisha jenga jina (wewe hapo bado Make ideas to be visible first.

    ReplyDelete
  5. Kijana naona akili imetulia. Naona hapo juu hamjaelewa. Website iko katika matengenezo. Basi tusubiri tuone kinachaoendelea. Ila wazo zuri. Kutengeneza nguo sio lazima uwe Gucci, tutasubiri tuone product zako. Kwavile wewe Mtanzania, usiwe na wasiwasi tutakupa sapoti. Kwani Tommy Hilfiger alianza wapi? We anony wa kwanza, tumia akili yako. Muziki website ni www.defunkadelic.com. Nimekua namfuatilia huyu dogo. Kichwa kimetulia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...