KUNA MDAU KANITUMIA SALAMU HIZI ZA IDDI PAMOJA NA UJUMBE NA AMEOMBA SOTE TUUSOME. NATHIBITISHA KWAMBA MWENYE JINA HILO NDO MWENYE NALO BAADA YA KUONGEA NAMI KWA SIMU NA KUTUMA EMAIL YENYE UJUMBE HUO



EID MUBARAK.......

HESHIMA KUBWA NA NYINGI SANA KWA NDUGU WASOMAJI WA BLOGG YAKO KAKA MICHUZI.

NAOMBA NIJITAMBULISHE KWENU WADAU. MIMI NAITWA RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE.LEO WAKATI NASOMA NINI KILICHOMO HUMU NDANI NIKASHANGAA KUKUTA KWAMBA KUNA MTU ANAJIITA KWA JINA LANGU NA KWA USHAHIDI ALIPOULIZWA WEWE NI NANI AKAJIBU MIMI MWANA WA JAKAYA.

SASA NDUGU ZANGU NAOMBA NIWAAMBIE KITU.KWA KWELI MIMI NINASUMBULIWA SANA NA HILI TATIZO LINALOTUANDAMA KWA SASA NDANI YA TIMU NINAYOIPENDA LIVERPOOL. NAJUA KWAMBA HAWA NI WALE WATU WANGU WA KARIBU AMBAO WANAJUA MAPENZI YANGU KWA WANA ANFIELD , NAZUNGUMZIA LIVERPOOL FC.NI KWELI KWAMBA TUKO NA HALI MBAYA (MANENO YANGU.....)NA WAO WAMEAMUA KUTUMIA TATIZO HILO KUNIUMIZA.

NAPENDA KUKIRI KWAMBA NI KWELI MIMI NIMEKUWA NASHABIKIA LIVERPPOL TOKA MWAKA 1985 NILIPOJUA KUSOMA NA KUANDIKA.NA PIA NAOMBA NDUGU WATANI WANGU ,MSITUMIE JINA LANGU.NAWAOMBA MNIACHE NIPUMZIKE MAANA KWA SASA NAFIKIRI TUNAENDELEA KULIJADILI HILI SUALA NA UFUMBUZI WAKE UTAPATIKANA SOON.NINA IMANI KWAMBA YULE WAJINA WANGU SIYE ALIYEJIBU NA HUYU ALIYEJIBU ALIKUWA ANATAKA KUNIUMIZA.NIMEUMIA VYA KUTOSHA NA NAOMBA NIJIULIZE.

NISAMEHENI KAMA NIMEWACHUKULIA MUDA WENU.NAKARIBISHWA KUKOSOLEWA.

NDIYE MIMI.

"WE WILL NEVER WALK ALONE."

RIDHIWANI KIKWETE TOKA UK.
Express yourself instantly with MSN Messenger! MSN Messenger Download today it's FREE!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Sasa wadau kuna wakati tulijadili hoja ya nchi yetu kama inaelekea wapi sasa hivi. Kuna baadhi ya wadau wakasema hayo tunayosema hayamfii Kikwete, lakini ukweli wa mambo unathibitisha kwamba Kikwete anapokea hizi salamu zetu kila mara tunapoandika. Naomba wadau tuendelee kutupa madongo ya nguvu, ili hii Serikali ya Kikwete ya ujanja ujanja wa kudanganya watu kila siku mpaka ijirekebishe. Tanzania haiwezi kuendelea tu kwa kupeleka timu kwenye fainali za mataifa ya soka ya Africa, Ghana!.

    ReplyDelete
  2. Siku zote nilijua lazima atakuwepo mtu anayesoma taarifa na comment zetu na si ajabu akawa anapeleka kwa wakubwa. it doesnt matter...so long as Tanzania itajengwa na sisi wenye moyo

    Serikali yetu inaniogopesha maana ni ahadi kila kukicha, je tuute serekali ya ahadi, na je itaofautianaje na zile za kusadikika?

    ReplyDelete
  3. Point less,
    Who cares who said wat to u keep that btwn urself na manmbo yako ya kuwa na ushabiki wa timu za nje, who cares umeanza kuipenda lini, watu tuko huku US long time I still dont feel that the Knicks a my blood team I still feel way more Simba inaposhinda kuliko kulia eti Knicks hawakufanya vizuri last yr, U must b soo dumb kuelezea upuuzi wako huku, again its point less 2 me
    pEACE

    ReplyDelete
  4. Mimi naamini mtoto is just an extension of his or her parents. Kuna chochote alichosema hapa huyu RIdhiwani? Siku nyingine ajieleze vizuri maana mtu alivyo ndio anavyosema na kwa style hii tuna weza extrapolate vinginevyo

    ReplyDelete
  5. wewe ridhiwani baba si anagombea mkono taifa stars iwe mbele vipi wewe sasa humuungi baba mkono,unakaa na kushebukia team ambayo hujui chimbuko lake lipo wapi.

    man hupo mbali kuwa na akili endelevu mzeee.

    ReplyDelete
  6. anonymous nakupa pongezi kabisa na nakubaliana na wewe kabisa juu ya huyo mtoto hapo juu hakuna lolote aliloongea labda tuu anataka kutupiambia yupo UK wakati sisi tumeichoka kabisa tunataka kurudi home kwa kukaa muda huku

    Pia nakubaliana nawe Anonymous this guy has pointless,he doesnt knw wht he talking about,my advice to MICHUZi next b4 sending back to us individual comments trying check out how far gonna rewards good ma merits to others Bloggers.

    Thankc,kijana mtoto wa kikwete ukikuwa utaacha naona UTOTO bado unakutawala kichwan,mimi japo nipo mbali huku bado kila siku nipo Bege kwa bega na watz wenzangu katika kuishaingilia team yetu ya TAIFA STARS kwa mbele not LIVERPOOL AU MAN

    ReplyDelete
  7. Ridhiwani, NI UTOTO tu ukikua utaacha! Liverpool? Manu? Ndo nini hizi mbele ya mtanzania? Nilifikiri Tumbaku, Yanga, Simba au Coastal Union etc. ndo Tunazijua sisi waTz. Kuchora, kuchora nini BWANA! watu wamechora lakini ..... Hivi unajua ni watu zadi ya 5 kidogo ktk BLOG hii wamekuwa wakilalamika kuwa MAJINA yao yametumiwa na watu wengine either kukashfu au kutukana lakini sijasikia wala kuona wakibandika ki-special MESSAGE kama chako wewe! Kutaja baadhi ni Amina Chifupa, Michuzi, Zemarcopolo, Emergency poison na wengine wengi. Sasa wewe Ridhiwani unaleta za kuleta! AU ulikuwa unataka kutujulisha kuwa babako alipopata URAIS nawe ukapata CHANCE ya kwenda Ulaya!!??? Ahaaaa, nilifikiri JK atakuwa kama JKN (JK Nyerere), kwamba wanae tulikuwa tunabanana hapa hapa Bongo. Naona ninyi mmeamwua kutubakiza Bongo na ahadi za waandishi wa habari na etc...
    The Very Revd.

    ReplyDelete
  8. Ridhiwani....

    Nothing PERSONAL but usual BUSY-NESS,

    Naona.... ume blah blah tuu! Yaani ulichokiongea.... badala ya kukujenga imefanya kikushushe kimtindo (as if i care)

    Dare Obasanjo (Son of president of Nigeria) was ma Boss for few weeks (Ningekuwa wewe ningesema i chat with him weekly he is in my MSN & Yahoo Messenger list) SUCH a down to earth fool but u wouldnt imagine what he worth in his pocket leave alone his BRAIN!

    One of the very first originaly African to head a Microsoft project and such a serious and good programmer.

    Comparing the two of you (as President's son) unanifanya nitapike....... (nothing personal im just kipping it real)

    Cause when it comes to football.... Haayaah humwambi kitu huyu jamaa kuhusu Super Eagles, Kanu ni rafiki wa karibu sana na Dare... Yaani akifika UK, yeye ndio mshikaji (Najua hiyo, ndoto kwako!!!)... though out the time nimemuona Dare UK, amekwenda kuona March za Arsenal tena front rows lakini sidhani kama angeweza ongea ambacho unaongea.

    Siwezi kukulaumu wanasema Akili ni Nywele, eeh? But i just wish u were something we would all be proud of!

    Hilo swala la "kutoka UK" limenikera sana.... Mimi nimepita na kuishi UK more times than i can remember... i earned a full flight miles za London-New York, Na sio kwasababu baba yangu waziri au whatever..... kwani mama yangu ni low court magistrate hata mshahara wake wa mwaka haulipi nauli....

    Toka umepelekwa English Course UK basi kelele tupu.... Tukikaa kimya sio kwamba hatujuoi!!!!

    Nitarudia kusema tena....

    "Sikuchukii ila nakudharau" (Nyasinsiki wa Kleptomaniacs)

    Michuzi nisamee.... imebidi niseme!!

    Mdau.

    utajijunashule@yahoo.com

    ReplyDelete
  9. POINTLESS

    ReplyDelete
  10. Hapa ww mtoto wa Jakaya umebowa mzee.Kwa hiyo unataka tujue kama uko UK au unataka tujue kama ww ni mpenzi wa Liver?Anyway nilikuwa nafikiri upo hapa bongo unasoma maana nasikia watoto wa JK ni kama wa JK Nyerere,wote wanasoma bongo.!!!

    ReplyDelete
  11. Unategemea aandike nini cha maana wakati ame-graduate kutoka UDSM. Wanafunzi karibu wote waliomaliza degree zao pale Mlimani ni pumba kabisa yaani ukiwaona wanavyojieleza ni aibu kubwa kabisa. They are not articulate hata kwenye lugha ya kiswahili na ukiwaambia waandike Kingereza ndio kabisa wanachemsha. Wewe unadhani kwa nini wanakosaga kazi kwenye Makampuni mbalimbali??

    Halafu nasikia Kikwete alikwenda Boston kujaribu kuongea na watu wa Harvard University ili aingie shuleni pale. Hivi nani atamkubalia kuingia Harvard wakati hata akiambiwa aandike essay ya maisha yake na matarajio yake katika suala la kielimu atashindwa.Hawa ndio wengi wao wanakuwaga viongozi Bongo. Maana asilimia kubwa ya Viongozi pale Bongo wamemaliza University of Dar Es Salaaam na unaona pumba gani wanazozifanya kila siku.

    Kuna umuhimu wa Mtaala mzima wa kile chuo ubadilishwe. Maana inaonekana baada ya miaka yote wanayotumia pale shuleni mijitu inamaliza pale na akili za High School huku wakiwa hawana mitazamo yeyote ya kimaisha.

    Hivi umeshawahi kusikia alumni wa UDSM wanakutana kuchangia shule yao ya zamani kimaendeleo???? JIBU NI HAPANA.

    ReplyDelete
  12. michuzi sio lazima ututhibitishie kuwa umeongea kwa simu na Ridhiwan,tumeona ukiandika emails za wapenzi wengi wa blog hii ila hujala viapo kwa niaba yao,za wengine hukujali kabisa kujibu mfano mimi nilipokuomba radhi kwenye picha ya faraja kotta na muonyesha mitindo ya tarehe 17 may 2006 baada ya mtu kukukejeli kwa kutumia jina langu hukujibu kwa aina yoyote(je pia nilipaswa kukuvutia waya?) au ndio njia ya kutuarifu kuwa blog hii inafuata ITIFAKI za dodoma?kuna ukweli lazima nikwambie mkuu,your blog is irresistable ila ukianza kuruhusu matabaka humu utaipunguzia wapenzi kwa sababu wengi wetu tunatembelea humu kurelax and feel at home sio kuwafagilia watu fulani fulani.

    ReplyDelete
  13. wewe ridhwan nilijua kwa sababu umesoma kidogo utakuwa na akili kumbe bado unakuwa na akili za kimaskan za kwa macheni kama baba yako au na wewe ulikuwa unamsindikiza mtaa wa dosi kunywa kahawa ndio maana akili zenu na maneno ya kitapeli ili mdanganye watanzania na sifa za uongo na ahadi zisizotekelezeka,kwani ungesema mi nin ridhwan tu kuna ubaya gani hadi utaje sijui uk acha ushamba wewe azu europe umeanza kuijua baada ya baba kuwa rais,sasa ungekuwa unakaa europe yenye akili kama sweden au nchi kama australia si ndio ungetunga nyimbo kabisa kuelezea badala kuipenda simba au yanga unaanza kujitangazia kama wewe pia ni mtumwa wa wazungu kama baba yako.

    ReplyDelete
  14. I COUL NOT AGREE MORE NA MAONI YA WANANCHI WENGI HAPO JUU. RIDHIWANI KIKWETE --WHO CARES-- NA KWELI LIKE FATHER LIKE SON HAKUNA CHOCHOTE CHA MAANA ALICHOONGEA KAMA ALIVYOSEMA MWINGINE--POINTLESS.
    WATU KWELI BWANA WOTE TULIZANI JK (JAKAYA KIKWETE) ATAFUATA NYAYO ZA JKN (JK NYERERE) LAKINI HAMNA LOLOTE ALITUONYESHA HIVI TU ILI TUMPE KURA.
    NI KWELI JAMBO ALILOSEMA MWINGINE KUWA WATOTO WA NYERERE WOTE TULIBANANA HAPA HAPA BONGO. HAKUPENDELEA HATA SIKU MOJA NYERERE KUNYAKUWA PESA ZA SEREKALI TAX PAYERS MONEY KUPELEKA WANAWE ULAYA. LAKINI SASA TUNAONA KIKWETE MAMBO MENGI ANAYOFANYA.
    NINACHOKUSAPOTI TU RIDHIWANI NI KWAMBA CHOO SANA JAMAA ALIYEINGIA HAPA KWENYE BLOG KUJIFANYA YEYE NI WEWE KWA KUTUMIA JINA LAKO. WATU NI WAJINGA SANA, NA WAKOME MAANA BWANA WIKI ZILIZOPITA KUNA FALA MMOJA PIA ALIINGA HUMU KUJIFANYA YEYE NI MICHUZI. MPAKA MICHUZI AKAINGIA KUKANUSHA. NA KUNA MWINGINE FALA ALIINGIA AKAJIFANYA KUJIITA ATI YEYE PETER RUPIA. WAKAINGIA WANAOMFAHAMU HUYU JAMAA NA KUZOZA KUWA HAIWEZEKANI HATA SIKUMOJA AKAWA NA SAA WALA DAKIKA YA KUINGIA NA KUANDIKA UJINGA HAPA.
    KUWENI NA HESHIMA. NA ACHENI KUJIFICHA NYUMA YA MAJINA YA WATU. JITOENI WENYEWE LAA SIVYO WEKA ANONYMOUS BASI INARUHUSIWA. AAAAHH! MNATUCHEFUA HAPA.

    ReplyDelete
  15. HUYU BWANA TUMSAMEHE, HAJUI ASEMALO KWA SABABU SIKUONA AMEANDIKA NINI-

    BWANA MICHUZI JE NI KWAKUWA HUYU NI MTOTO WA KIKWETE BASI UNAMPA UWANJA HATA KAMA ANAANDIKA PUMBA TU???

    ReplyDelete
  16. Wajameni hata kama ni pumba lakini kitu kimoja ni faida hapa. Walau sasa tunajua Mkulu JK anaweza kuambiwa yanayowasibu wananchi wake,kwani wasaidizi wake hawana ubavu wa kumweleza chochote. Kwako weye mwana wa JK, niliwahi kutoa maoni kwenye picha moja huko nyuma wakati Mshua alipobadilisha baraza la mawaziri. Mwambie Pops kipindi cha miaka mitano kinamtosha kabisa kwani ameonekana ni Rais bomu hakuna maelezo. Kama ni tamaa ya Urais si ameshaupata nini tena anataka? Kwa ufupi nikuwa anaipeleka nchi ndiko siko.

    ReplyDelete
  17. Kaka Michuzi,Tafadhali naomba usiweke message ambayo itachochea matusi!Nafurahi kuona kuwa message ya Ridhiwani imeheshimiwa sana!!kuna maeneo mengi ya kutupa maneno machafu ktk message hiyo ambayo imejengeka vibaya!!Labda UTOTO lakini next time Ridhiwani jaribu kupost kitu kinachoendana na wakati na mapenzi ya walio wengi.Usipoangalia utachafua jina KIKWETE humu!

    ReplyDelete
  18. Wewe Riwa nafikiri umechoka kufikiria. Sisi sasa hivi watanzania tunachotaka ni maendeleo mambo ya kutwambia Livapool na kutubadilishia muelekeo hatutaki hujasikia mugabe anakataza vijana wa zimbabwe waache kuangalia mechi za ugaibuni? Tunachotaka ungetuandikia hapa mambo ya Tanzania Simba na yanga siyo akiri za ukichaa.

    Next time usiweke comments za namna hii za kitoto hacha wazee wa blog waongee. After all watanzania wanaitaji maendeleo siyo mambo ya kuhemea yamepitwa na wakati tangu baba wa taifa ni kuemea mpaka leo wakati maendeleo hakuna, tumechoka. na maendeleo yanaletwa na fikira sahii na zilizokwenda shule. Wakati watu wanajikwamua na kufikiria maendeleo ya kuachana na nchi zinazotunyonya wewe bado unafikira finyu za live-poor.

    Naomba next time tuma maoni yenye ushawishi ili tusije tukakuita muhuni. Anyway ndiyo hali halisi

    Thanks for understanding

    ReplyDelete
  19. Ridwan, wosia kwako ndugu...."It is better to keep your mouth shut and appear stupid than to open it and remove all doubt."~Mark Twain Ukishakaa huko baada ya miaka kadhaa usome tena hii e-mail ujione ulivyo mpuuzi na ulivyochemsha kwa hali ya juu. Hakuna lolote la maana ulilosema kama walivyosema wengine hapo juu.

    ReplyDelete
  20. Calm down..... i say calm folks, dont you guys see a point on the so called mtoto wa presider! whatever way his message is, there is point that concerns using other people identity. Please stop using his name, i say stop thats a crime. I know that every one if not kila mwananchi regard Ridhiwani as an intelect but critical writtings troubles loads of people in this world and that includes George Bush junior. Supporting liverpool is something else and above all its a choice. Remember just like you and me he the citizen of the world, free to express his opinion. Capish!!!

    ReplyDelete
  21. Anony wa saa 7:20(TRH 26-2006) wewe ni ch**i ya wadhungu, aliyekuambia kuwa kusoma UDSM kunaashilia kuandika pumba nani? Nina wasisi na wewe ni m2 wa kwanza kusoma nje ya nchi ktk family yenu ndio maana unamtazamo wa kujumuisha mambo, K**a we! Na wewe ANT-STUPIDIT hiyo tabia ya kutuletea sifa za mabwana zako wa Ki-nigeria humu ndani ukome matak* mkubwa. Watu tumemaliza hapo UDSM na tumepokelewa hapo Harvard na hizo essay zetu.( For more details toa e-mail yako tukope details za elimu) au wewe ni kati ya disco za bongo ulikimbilia nje?
    ANT-STUPIDIT na watoa maoni wengine, yeye Ridh kausishwa na Liverpool sasa nyie mnataka aongelee Yanga au simba au siasa hamuoni kuwa ni kutoka nje ya mada. Kikubwa mkaribisheni katika yale mnayopenda achangie na ndipo mjue muelekeo wake.

    ReplyDelete
  22. Ni aibu....ni aibu!Michuzi huitaji kutuambia umethibitisha umeongea na huyo jamaa....it's no a big deal!We don't care.

    Niliposikia Jakaya Kikwete anafananishwa na Mwalimu Nyerere,nilifadhaika sana.Sioni busara ya Mwalimu inafanana vipi na jamaa huyu ambaye alikuja na mkewe Marekani kutalii.Hakuwa na lolote la kufanya.Nyerere asingeweza kufanya upuuzi wa kutumia mamilioni ya nchi yetu maskini kuja vacation.

    Kila siku nasoma ahadi nyingi za 'rais' huyo mpya....sioni vitendo,ahadi nyingi ambazo hazina kichwa wala miguu.Kama alivyo waziri mkuu wake ambaye anashindwa(anaogopa?) kuchukulia hatua za wazi viongozi wazembe wanaokutana nao kwenye ziara zao,ndivyo alivyo Kikwete.

    Tanzania bado itaendelea kuwa miss viongozi kama Edward Moringe Sokoine na Baba wa Taifa ambaye hawezi kuwa replaced na mwingine yoyote kama Jakaya Mirisho Kikwete anavyofikiri.Sijawahi hata kumsikia jamaa huyo akimwongelea Mzee Nyerere hadharani!

    Ridhiwani...unawakilisha mawazo ya Mzazi wako.Hivi huko Ikulu hakuna protocal?How come wanakuruhusu kutapika utumbo huu hadharani!???

    Mwambie Mzee wako aache ujanja wa mdomoni wa kudanganya mamilioni ya watanzania.Tunajua kama viongozi wengine waliopita...mission yake ni 'kula tu'.Mwambie tunajua hilo,he won't be able to cheat everyone!

    ReplyDelete
  23. I seriously dont understand us Tanzanians this would probably include myself cause i dont understand you people.Here is a guy who is just shows he is a Liverpool fan and writes a comment about a team he likes and people start attacking him just because he is the Presidents Son?? I just dont seem to understand how that is supposed to determine what he expresses?? I have read a 1000 posts and most of the comments are insults directed to other TZ's.Is this inferiority complex or just ignorance of a few individuals? How can any sane Tanzanian come up with the idea that UDSM graduates cant even speak or write in English?I for one am proud of graduating from UDSM and dont see the difference from working in a Government institution or an International Company as long as the package is right.Being a liverpool supporter or a Simba supporter is ones choice or desire,just as it is someones choice to use CK cologne or marashi ya Zanzibar.If all these comments were printed and posted in every country in the world, can you imagine what picture of Tanzanians will other citizens of world get...

    ReplyDelete
  24. michuzi,is dat JK son does know what is it be President son!!! Let him be careful wat he says publicly!! bcoz we have unparented guyz who have been using profanity and defamatory information to satisfy their envious and covetous heart. We dont want Our President to caught up in that silly debate!! Remember Jk is remain the favourite president in Tanzania Political history!! TRUE TANZANIAN

    ReplyDelete
  25. We Pakamcheshi soma vitu uelewe kabla ya kuanza kuongea oumba zako na wewe, No body said its wrong 4 him to like watever team he likes, but who cares bout that we dont c y he should post that up here.

    2 Michuzi hivi kweli tunavyosema kwamba unababaikia watu na wewe unataka kutuonyesha ukweli wako, sasa huyu mtoto mdogo na anayeonekana kwamba akili hana unamuogopea nini mpaka kutuwekea hii msg ya kipumbavu au kwa kifupi wewe uliona inamaana au msg gani kwetu mpaka kuiweka na kutuhakikishia kwamba umeongea nae, au ndio unafikiri utaonekana wa maana kwa kuongea na toto pumbavu la rais.Pls tumeshajua kwamba hili toto ni jinga so naomba usituelezee ujinga wako tena siku nyingine, unayo Email ya m,ichuzi mtumie muongee wenyewe upuuzi wenu

    ReplyDelete
  26. Watu hawana tatizo na huyu kijana kuipenda Liverpool, ni uamuzi wake na haki yake kupenda timu yeyote. Tatizo limekuja kutokana na kujieleza kwake. Kusema ukweli kijana amechemsha kwani kwa mtu ambaye ana degree ni aibu kubwa sana ukisoma alichoandika. Taani hakuna kinachoeleweka au mtiririko sahihi wa alichoandika. Nadhani weni ndio maana wanampigia kelele.

    Na kuna mtu amezungumzia wanafunzi wanaosoma UDSM,kuna ukweli ndani yake kuhusiana na wanafunzi wanaosoma/kumaliza UDSM kuhusiana na wengi wao kushindwa kujieleza ingawa kushindwa kujieleza hakumaanishi umbumbumbu wa mtu. Nilikuwa na Kampuni kubwa hapo Tanzania upande wa Human Resources na nime-interview vijana wengi wa UDSM.Wengi walikuwa wana-perform hizo interviews below standard tuliokuwa tumejiwekea kwenye kampuni.

    ReplyDelete
  27. SINA KAWAIDA YA KUINGILIA MIJADALA, NA WALA SINA NIA YA KUMTETEA MASIKINI RIDHIWANI. MIE PIA NI LIVAPUU DAMU, NA YEYE AKIWA LIVAPUU MWENZANGU, NAONA DONGE KUONA ANASHAMBULIWA HIVI. HAPA WADAU MWENZETU AMEJARIBU KUTUMIA LUGHA NYEPESI INAYOENDANA NA BLOGU YENU HII. KAULI YAKE HAIMAANISHI LOLOTE ZAIDI YA KUENDELEZA NA KUONYESHA HADHARANI MAPENZI YAKE KWA TIMU AUPENDAYO, NA SI VINGINEVYO. MIE PIA NAMUUNGA MKONO KWA KUWA JASIRI NA KUJITOKEZA HIVI. KWA KUWA ALIKUWA HAFANYI DEZETESHENI, SIONI KUWA NI VIBAYA KUWA NA MTIRIRIO KAMA HUO. NAJUA FIKA WENGI WENU NI MANI YUU AMA ASENO, KAMA SIO CHALSII AMA CHAMA INGINE, HIVYO SISHANGAI NA NAJUA RIDHIWANI HAONI JIPYA, NDO MAANA AMEKARIBISHA KUKOSOLEWA. VINGINEVYO, SEMENI MPENDAVYO, LAKINI SIE LIVAPUU AMA BWAWA LA MAINI HATUTAWOKI ALONI. NA MKUMBUKE BAHARI MAJI HUPWA NA KUJAA. IKO SIKU NA SISI TUTACHEKA.

    RIDHIWANI MWANANGU, POLE KWA YOTE, LAKINI NDO VILE TENA. USIKATE TAMAA NA WALA YA WADAU WASIO WAPENZI WAN LIVAPUUU WASIKUKATISHE TAMAA, WE WILI NEVA WOK ALONI, IKO SIKU MWANANGU...

    ReplyDelete
  28. Mimi na yule wa kusema UDSM wanaperform chini ya kiwango namwambia pole sana na kuwa na akiri finyu ya kizungu nakushauri ukasome. Na kama ulikuwa na kampuni kama human reso ni kwa sababu hukufanikiwa kusoma pale hivyo ulikuwa na negtive altitude.

    Mimi mwenyewe nimesoma UDSM na nimekwenda vyuo vyingi duniani ikiwemo USA, JAP., Urope, RSA, Kenya na pia nimeona vijana wengi waliosoma UDSM pia ninachojua wanajua mambo mengi sana.

    Najua tu wewe unafukiri kujua sana kingereza ndiyo elimu hila labda nikwambie siyo kweli wajapani mpaka mtu anafika PhD hajui Kiingereza na wanafanya mambo makubwa. Na wakati mwingine kama ni mikutano mikubwa huwa wanaongea kisonche na kuna mkarimani. Hata mkarimani wake anaweza kugongwa mambo mengine lakini wako mbali kila nyanja. Kwa hiyo acha kutwambia sijui avadi sijui nini.

    naona bado hata kama ulikuwa unafanya kijiwe gani lakini naweza kukupima vizuri nakuona kuwa bado ulipata hiyo kazi kibahati ujabobea kweli. Kwa kifupi nakushauri ukasome tena(Watu kama wewe ndiyo wanarudisha maendeleo ya nchi nyuma eti anajua kibonbo). samahani naomba usinishambulie mzee samahani sana, unajua kwa michuzi hapa ni kuelimishana.

    ReplyDelete
  29. Wote mliomshambulia Ridhiwani hamna lolote zaidi ya wivu wa kijinga tu, mkikua mtaacha!

    Kuhusu wahitimu wa UDSM, kusema hawajui lolote siyo sahihi na siyo kweli. Wamehitimu vizuri na wanazielewa vizuri fani zao, upungufu(kama naweza kuuita hivyo) upo kwenye eneo la kujielezea au kujinadi, utakuta mtu amefuzu na kuhitimu vizuri tu shahada yake lakini kwenye mahojiano ya kuomba kazi hasa katika haya makampuni ya kimataifa anashindwa kuonyesha kujiamini pamoja na kwamba anaijua kazi aliyoomba vizuri tu.

    Hili kwa mtazamo wangu mara nyingi linachangiwa na ule unyenyekevu wetu sisi Watanzania, maana hatupendi kujikweza, mfano tukiulizwa "una uhakika uweza kuifanya kazi hii?" tunajibu
    "nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu" tukiamini kwamba eti tukishaipata hiyo kazi basi ndio watajua kuwa tumebobea kwenye fani husika vilivyo.

    Sasa wenzetu wanajinadi kweli kweli mtu ana ka-stashahada lakini anavyojipamba kwenye mahojiano manjonjo kibao utasema mfanyakazi si ndio huyu! Akiajiriwa ndio kwanza anajifunzia kazi hapo hapo tena kwa wahitimu wa UDSM walioko chini yake. Sasa na sisi inabidi tujifunze kujinadi na kujisifia sana kibao kigeuke.

    ReplyDelete
  30. naona mjadala sasa umehamia kwenye chuo kikuu cha dar es salaam!naomba tuwe realistic.chuo chetu kinaelemewa na kiko katika hali mbaya,tena mbaya sana.mahojiano ya mkuu wa kitivo cha sheria na waandishi wa habari katika siku ya kuhitimisha miaka 45 ya chuo yanadhihirisha hili.imefika hatua kitivo kinaondoa seminar zote,yaani wanafunzi wanafunzwa kwa lectures tu(zaidi ya wanafunzi 300).VC Luhanga anamaliza muda wake,kazi imetangazwa na hakuna prof anayeitaka mpaka sasa.wanaogopa lawama.baada ya prof Chachage kututoka wakufunzi wenge wa UD wamenukuliwa wakisema hakuna mwingine atakayeweza kukielekeza chuo kwenye direction sahihi.kama kuna kitu tunachoweza kufanya kukiokoa chuo chetu basi tafadhali tufanye hivyo.Hata hivyo sijafurahishwa na watoa maoni waliosema wahitimu wa UD hawawezi kujieleza,ili kufikia kutoa sentensi kama hii inahitaji kufanyika utafiti kwa representative sample.siwezi kuwatetea wahitimu hao kwa kuwa hata mimi sijafanya utafiti wa kuiprove nul hypothesis wrong.Ila ninakiri kuwa nimeshuhudia wahitimu wa UD wa aina zote mbili,wapi ni wengi zaidi?THE TOPIC IS OPEN TO RESEARHCERS.

    ReplyDelete
  31. Zemarcopolo kimsingi nakubaliana na hoja yako kuwa inabidi ufanyike utafiti kuthibitisha madai hayo. Inasikitisha kuona Mlimani mambo yanazidi kuzorota.

    Kwa uzoefu wangu mdogo ninaweza kusema kuwa "mangwini" wengi zaidi ni mahiri katika kujielezea ukilinganisha na watu wa biashara, sayansi au uhandisi.

    Pengine hivi vitivo vingine vineweza kunufaika na mitaala ya "kingwini" japo kidogo ili kuondoa hali hiyo.

    ReplyDelete
  32. Wadau wa blogi hii nimesoma maoni ya wengi kuhusu huu mjadala. Sidhani kama watu wanamshambulia ndugu Ridhiwani kwa nia mbaya. Wanametoa maoni yao kutokana na maandiko aliyoyatoa yeye.

    Kwa kweli ukisoma huu waraka aliotuma, utajiuliza mara mbili anataka kusema nini kwenye huu ujumbe.

    Yaani amejikanyanga sana. Binafsi simjui mwandishi wa huu waraka, ila kutokana na habari na picha zilizokuwa zinatolewa na vyombo vya habari wakati amehitimu chuo kikuu cha Dar-es-Salaam mwaka jana, nadhani watu kama mimi tusiomjua tulikuwa na matumaini ya juu (Higher expectations) angalau anaweza kujieleza kwa sentensi mbili tatu kuwa mimi ni mshabiki wa Liverpool na aeleweke vizuri.

    Ila ujumbe alioandika hapo juu ni kituko, labda ndio maana watu wameanza kushambulia moja kwa moja shule aliyosoma kuwa haina kiwango.

    Lawama zangu pia zinaenda kwa Michuzi. Wewe kama mwandishi wa habari, je ulivyopokea huu ujumbe uliona unafaa kabisa? Yaani mtu atasoma mara moja na kuelewa bwana mdogo anasema nini?

    ReplyDelete
  33. Mimi labda nitaongelesa kiujumla ni kwamba hapa duniani kwa miaka minne watu wanayosoma vyuo vikuu siyo tu tanzania hila ni duniani kote huwa wanapata general knowledge.

    Baada ya muda ndipo mtu anapata experience au anaweza kupata uhelewa mzuri kama atasoma masters. Ni vyuo vichache sana duniani ambapo mtu anamaliza tu shule anakuwa competent sana. Hata huyu aliye andika ujumbe mimi ninachojua bado anajifunza.

    Katika kupata elimu mwanzo huwa ni pale mtu anapokaa darasani baada ya kuwa amepata hiyo ni elimu kubwa tunaipata makazini, masters na PhD. Ndio maana utakuta mtu ana first degree na mwingine anadipoma lakini diploma anamzidi first degree sababu ni uzoefu alionao. Lakini degree anapata uzoefu haraka sana kulinganisha na diploma.

    Sasa huyu Riwa degree yake ni ya juzi hajapata challenges za kunoa kichwa chake sawasawa anasoma. Ndio maana hata usome havard ukimaliza tu shule bila kupata kazi/challenges unakuwa kama mkulima wa kijijini baada ya muda.

    Kwa kuona hilo nchi kama south Africa zinaweka utaratibu ambapo unakuta watu wanabaki chuo baada ya first degree kupata more challenges na u masters wakati mwingine.

    Unajua ni vigumu kujifunza mambo yote pamoja. unatoka nyumbani hujui kitu huwezi kukisoma miaka mitatu na hapohapo ukaweza bobea kwa kipindi kidogo. Pia kama unalimitaions na knowledge ni vigumu kuongea chochote nijuavyo university of UD huwa wanatoa general knowledge lakini baada ya kumaliza tu huwa ni vigumu watu kupata kila kitu at a time, lakini baada ya muda mfupi wa kumaliza shule(within three to four yrs) kwa kutumia general knowledge wamekuwa watu wazuri sana, na hata wale waliopata orportunity baada ya hapo kwenda ngambo wamekuwa tishio(kama kweli wanaamua kusoma).

    ReplyDelete
  34. Nyie watu mlio na mtazamo hasi, lini mtajifunza kuheshimu (sio kukubali) mawazo ya mtu mwingine? hivi si ndiyo nyie ambao hamtotaka kusikia mwenzi wako ana kushauri jambo au hata mtoto wako? Badilikeni, unaweza usikubaliane na mawazo ya mtu mwingine na ukachangia mjadala kwa kuonyesha kabisa hukubaliani naye. Lakini kuheshimu mawazo ndiyo kitu kikubwa cha kuonyesha jinsi gani u-mstaarabu.

    ReplyDelete
  35. I'm deeply hurt and dissapointed by comments aired by one of the contributors regarding quality of UDSM graduates. I completed my first degree there in 1999 and I'm currently enrolled in an MBA programme in the same institution. I totally disagree that there is a problem of producing graduates who are of inferior quality relative to those from other Universities.UDSM has always strived to attain high academic standards, and this can be corroborated by a recent report issued by a reputable university-ranking organisation, which ranked UDSM as the 11th university in Africa in terms of academic excellence. Of course UDSM has always acknowledged a problem in the area of communication skills, however, any intelectual can not use that as the only basis to discredit the quality of degrees ofered. I would therefore like to urge all Tanzanians in the diaspora to disregard such baseless claims which I believe can only come from those who have failed to excel within our academic system which is acknowledged world wide as one of the toughest. Of course UDSM is not Harvard, or Cambridge, or MIT or Wharton, but it is a reputable institution with graduates who have scored a lot of success in their careers. One last comment: All UDSM graduates who later pursued their postgraduate studies abroad have always passed with distinction. That speaks for itself about the foundation they receive from UDSM.

    ReplyDelete
  36. Hivi nyinyi wa TZ wenzangu mbona mnatia aibu? mmekuwa kama wasenge bwana angalau najua kwamba katika nyinyi mlioandika haya maona kuna mmoja au wawili wasenge, kwanini mna chuki binafsi? hivi huyu Rizwani amewakosea nini? au kwa sababu baba yake ni Rais? ndiyo maan mna wivu? alichokosea yeye hasa ni nini, au kusema kwamba anaipenda Liv? mbona nyinyi kila kukicha mnaandika vitu vingine havina hata maana wala hamtukanani hivi tutaendelea lini? tupendane wa TZ tuache wivu wa kijina yeye ni mtoto tu wa rais wala hakupa baba yake hicho cheo ni nyinyi wenyewe na wazazi wenu na majirani zenu ndie mliompigia kura yeye wala haimuhusu mnaandika vitu vya kitoto tu K**ma nyie, na wewe K**MA uliyesema kuwa watu waliosoma mlimani ni ma pumba hivi huyo aliekuajiri kwenye hiyo kampuni yeye ni pumba kukupa wewe kazi, kwanza soma ulichokiandika utajijua kuwa wewe ni pumba wa kwanza ulikuwa na kampuni kubwa je ni ya kwako? sema niliajiriwa kwenye kampuni kubwa kwa sababu hukusoma mlimani ndiyo maana hata kujieleza hujui K**MA wee!! na kwa sasa hiyo kampuni iko wapi? kwa nini unasema nilikuwa na kampuni kubwa au imekufa na kama imekufa ni kwa ajiri ya kuajiri watu kama wewe au kama ipo na wewe haupo hapo ndiyo utajijua kabisa kwamba wewe ni pumba mpaka umefukuzwa kazi kwanza hiyo kampuni kubwa ni ipip ambayo haijulikani?
    Michuzi na Riziwan endeleeni na ushabiki wenu wa LIV msiwasikilize hwa wanafki wengine hawakuwa na uwezo wa kufika mlimani wakazamia meli kwenda nje na sasa wanabeba mabox na kujilipia shule za online eti wanasagia milmani wasenge kabisa, Ninawasubiri

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 11, 2007

    jamani...je ukijibizana na kichaa wewe utakuwa nani?na kama huyo ridhiani amejosea kupost ingekuwa bora mkamsahisha kistaaraabu...yeye kutokea kuwa mtoto wa rais sio kigezo na wala msimuhukumu kwa hilo...je mbona michuzi mwenyewe alishaomba watu wasitumie jina lake in the same way na hamkutukana?...sawa kuna vigezo ambavyo naye huyo ridhiwani amekosa kama kuandika ridhiwani from uk,maaana kw kweli ni ushamba...ila kama ikionekana mtu kaandika pumba ni bora kum-ignore maaaana kuanza kupost ma comment na nyie mtaonekana walewale..ila pia msi-mjudge kijana wa wa2 kwa makosa ya baba yake..

    ReplyDelete
  38. Naomba nipingane na huyu jamaa aliyeikandia UDSM kwamba wahitimu wake hawajui kiingereza. Kwanza inaonyesha huenda huyu jamaa hakufika chuo kikuu na hii inaonyesha chuki dhidi ya wale waliofika au wazee walimng'oa katika mkao wa kwanza (first sitting) na kukimbilia huku kubeba maboksi. Inatakiwa ajue kwamba kuongea kingereza siyo kigezo cha uelevu au kufika chuo kikuu kwani ingekuwa hivyo waingereza wote au wamerikani basi wote wasoma chuo kikuu. Kumbuka kiingereza ni lugha tu kama ilivyo kiswahili, kisukuma n.k. Uzoefu wangu unanionyesha kwamba watoto wengi wa wakubwa wa enzi hizo waliofeli UDSM walikimbilia nje kusoma na wengi nahisi ndiyo hawa wanaoilamu UDSM. Kitu kingine naona wadau wengi mmeonyesha mnachuki binafsi kwani uraisi wa JK na upenzi wa Liverpool wa mtoto wake vitu viwili tofauti, msirushe mawe wakati mpo kwenye nyumba za vioo, huenda wengi wa wanaolamu wazee wao ndiyo waliohusika kuifilisi nchi na ndiyo na wengi wamepata nafasi za upendeleo ambazo hawakuwa na sifa nazo. Tutaumbuana humu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...