kikosi cha taifa kilichobeba kombe la ubingwa wa afrika mashariki na kati mwaka 74. f. mtimkubwa hebu tusaidie kahistoria kidogo na majina hapa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Je nami nipo? Nilikuwa Kipa hodari enzi hizo!

    ReplyDelete
  2. Dilunga, je?

    ReplyDelete
  3. Kibadeni, je?

    ReplyDelete
  4. Sunday Manara, yule "komputa", je?

    ReplyDelete
  5. Michuzi naomba uwe makini na miaka unayoandika.Hii timu sio ya mwaka 1974 hii ni timu ya miaka ya 1960.
    Katika picha hiyo namuona Marehemu Kanali Aziz ambaye mwaka 74 alishastaafu kucheza mpira.

    ReplyDelete
  6. Michuzi kaishiwaaaa, huna jipya na wala huna la maana tena huku kwenye nlog yako ndio maana unaangaika kuweka picha ili watu watukane coz atleast inafanya watu warudi kuangalia huku, muda umeupata lakini naona maendeleo hakuna na mimi hii ndio mara yangu ya mwisho kuingia huku coz hakuna la maana ninalolikuta.

    Kwa wabongo wenzangu tunaopenda kuangalia mambo mapya kila siku ingieni kwenye website zenye maendeleo kama, tanzatl.com, bongoradio.com na huko mtakuta mapicha ya maana na hata ku-upload picha zenu kama mnataka achananeni na huyu masikini wa akili Michuzi

    ReplyDelete
  7. Muhidin,

    Kitendawili hiki kukitegua hata ukinipa mji kimeniwia vigumu. Sasa ngoja nikipeleke kwa wanasoka wa zamani kina Bakari Wagadugu au Mzee Miraji Mataruma wanisaidie kupata jibu.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    PS/ Halahala Novemba mosi mbaya zitaanza kuanguka toka juu ya MtiMkubwa.

    ReplyDelete
  8. Michuzi nasikia owner wa Oxford city football club na stadium ya Kassam ni mbongo !
    Naomba wadau wako wanaoweza kutupigia picha watuwekee kwenye blog yetu tukufu ?
    Labda siku moja ataona aibu aisaidie soka ya bongo ama amnunue angalau Njohole !

    ReplyDelete
  9. f mtimkubwa nimekuapata. nitafanya hivyo. tafadhali wewe na wengine msikose kutembelea tanzatl.com na bongoradio.com, kuangalia mambo mapya ya kila siku

    ReplyDelete
  10. We anony wa 4:45 inaonyesha unamatatizo kichwani mwaka. Ukitaka kuacha kuingia huku ya nini kuutangazia umma? Hebu tukumbushe post yako uliyoutangazia umma kuwa unaanza kutembelea blog hii? Acha hizo kama unaona tanzatl na bongoradio yako havitembelewi sasa unaamua kuvipigia debe? Wahenga walisema "Kizuri cha jiuza kibaya ..." Acha kutuchefua na coz, coz, coz, nyingiiiiiiiii utafikiri ndo umelifahamu leo hilo neno>

    ReplyDelete
  11. nyie wenye akili finyu endeleeni kupigiana mama na mwana ya kujibu maswali ya kijinga ya timu za mipira, na kuangalia watu wakila daku kila siku, na matusi yasio na sensor, wenye akili timamu tutaangalia yanayovuma pengine

    ReplyDelete
  12. by the way ni atl.org sio com, lakini mi sioni ubaya wa aliyokisema ndugu yangu hapo juu, cha maana ni kwa michuzi kujua kwamba anaanza kuwa boa watu na picha unazoweka na kama unataka maendeleo utasikiliza maoni ya watu

    ReplyDelete
  13. mhhhh, michuzi kaka hii ya leo kali, tumeangalia hii picha ninakumbuka kikosi cha 74 walikuwamo kina Leodgar Tenga, Chuma, Kibaden, Zaharan, Marehemu Sembuli,Kompyuta,Ngulungu, Mambosasa,Abdulrahman Juma, Wakiwa ni baadhi tu, na sio siri kwenye hii picha yako HAWAMO! sana sana namuona mtu mmoja tu ambaye namfahamu HEMEDI SEIF, tena yaaanki, ambaye nina uhakika 74 alikuwa keshastaafu zamaani, vipi blaza??!!

    ReplyDelete
  14. Michuzi mwenyewe alikuwa hajazaliwa bado. Hii ni mwaka 1958 wakati huo kombe la challenge likianzishwa nalilikuwa likijulikana kama Gossage Cup. Mwaka huo Tanganyika ililitwaa kwa mara ya kwanza (na ya mwisho adi ilipokuja kufanya hivyo tena 1974)

    ReplyDelete
  15. Hizi ni enzi za akina Yunge, Jabali na wenzake wa Sunlight Cup ya Tanganyika na Gossage ya Afrika Mashariki!

    ReplyDelete
  16. Mpaka Haji Lesso yumo! Hiyo ni mwaka 47

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...