wadau wakuu wa mkurbita wa bongo wakibadilishana mawazo leo baada ya jk kufungua mkutano wao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Mimi nina wasiwasi kuwa hawa wote waliokohapa wanajua kusema tu mkurabita lakini hawahujui!!!

    ReplyDelete
  2. You are right Anony. Hawa wote Umaskini walishauacha na hawaujui sasa watatakaje kuondosha kitu wasichokifahaumu? Watoke hapa na ulaghai wao.

    ReplyDelete
  3. Michuzi naomba tuelimishe MKURABITA ni nini?

    ReplyDelete
  4. Mpango wa kurasilimisha rasilimali na biashara za WANYONGE Tanzania MKURABITA,Mimi leo nipo interested zaidi na hichi kipengele kinachosema za wanyonge,ila kwenye hiyo picha sijamuona mnyonge hata mmoja,na ninaamini wanaofaidika na huo mpango wa wanyonge ni watu kama kina simba ambao walishakua na mabenki nchi za nje tangu miaka ya sitini,achilia mbali hawa machinga wanaozagaa mitaani na kina mangi wasiojua hata kama kuna kitu kinachoitwa mkurabita,huu mkurabita zaidi ya kuyajua makao yake makuu pale ocean road karibu na kwa baba mkubwa(mzee ben) sijawahi kusikia tendo hai hata moja lenye lengo la jina hili,kwa hakika nasikitika sana,naamini hao walami(wazungu) wakiingia ndani watapigwa bonge la lecture si imeshaandaliwa?ni kusoma tu ngwini izo alaf watatoa chochote kitu,nao si wana interest zao?ila je?mangi kule tandale,chinga huko mitaani na mimi young tanzanian graduate,nitakurabitiwa kweli?si mtoto wa kibosile tu anaejua how to get hizi neema za inji hii?cjui!labda!au kuna njia gani za kutumia hizi fursa?michuzi hebu fuatilia,usijekuta kuna opportunities ambazo tunakosa kuzitumia becoz of lack of information.lakini isiwe kuhudhuria makongamano ttuuu na warsha za mara kwa mara bila kitu hai kuonekana,i sugest walau wafungue majengo makubwa ya kuelimisha na kuendeleza sanaa,kazi kama za useremala,ushonaji,ujenzi nk na kisha kuandaa jinsi ya kuwapatia masoko ndani na nje ya nchi na si politics tuu!hebu fikiri kingekuwa na vitu kama hivyo vijijini kuna watu wangekimbilia mijini kweli?and we could increase our gdp,rather than selling only chinese products,THINK GLOBAL,BUY LOCAL.Its me, mimi.

    ReplyDelete
  5. Wabongo kwa kutunga majina tu nawakubali, mara MKUKUTA mara MKURUMBITA. Hila njoo kwenye utelelezaji mmmmmmh.

    ReplyDelete
  6. Zulumati wakubwa !

    ReplyDelete
  7. Ili tuendelee tufanyeje maana hakuna anaekuja na solution ya hili tunabakia kuwataja tuu watu huyu mwizi huyu bepari na hili ninarirudisha huko nyuma tulikotoka mambo mtu kuwa na kitu ilikuwa haramu sasa ni mfumo wa uwazi na sekta huru za kibiashara tunabaki kuwabatiza watu uhujumu wewe kama unajua hujuma za Simba ,Mkapa na akina warioba si kuna vyombo vya sheria ni lini tutaacha kulaumiana maana ndo tatizo letu sasa hivi Watanzania na wapi uliona lawama zikaleta maendeleo tujinge nchi kwa vitendo jamani wewe una mtaji wa mitumba basi uza mitumba yako una wa maji uza maji yako sio ohhhh wanakwiba mwizi mshike halafu atafikishwa kwenye mikondo ya sheria , Ndo maana unaona matajiri wazalendo wa Kiafrika wakiwa nyuma kusindikiza wadosi na wawekezaji uchwara sababu tuu ya vijicho na fitna tulizokuwa nazo wazalendo tajiri anayejulikana na kuonyesha utajiri wake ni Reginald Mengi wengine wote wamekalia pesa zao hiyari wale na wake zao na jamaa zao wa karibu ntakupa mfano katika nchi kama Kenya ,Nigeria ,Ghana na Hata South Africa wazalendo wenye pesa zao wamejitolea kubuni miradi ya kusaidia wanyonge na kula nao kile kidogo kinachopatika kwa wale mliofika Nigeria watakwambia wahindi na waarabu hawafurukuti wamebanwa na wamebakia na biashara za maduka ya nguo na dhahabu zingine zote ni wazalendo Wahausa ,Wayoruba na Waibo bila kusahau Wafulani sasa lini tutaiga huko tuacheni lawama jamani maendeleo sio lelemama fungeni mikanda mtavuna tuu

    ReplyDelete
  8. Hawana lolote hao waizi tuu tuu,miaka yupo hiyo wapo madarakani hawana lolote walichofanya juuu ya umasikini leo wanasema nini,Au wamegundua Kamtaji cha kula hela za watu kwa kusingizia wanataka kusaidia watu,hawana lolote hao waizi tuu honest to be with them!!

    ReplyDelete
  9. Du, sasa hawa jamaa kwenye picha si ndio wenyewe wamejimilikisha kwa kurasimilisha rasilimali na biashara kibao zilizokuwa zinaendeshwa na serikali hapo awali!
    Hii mikakati mingine ni wazi kupima mafanikio yake ni vigumu mno.
    Watu vijijini huko tangu enzi za Adamu na Hawa wamekuwa wakifanya biashara bila kutunza kumbukumbu wala kutumia fedha na mambo yamekuwa yakienda na wanaishi hivyohivyo. Sasa ukianza kuwaambia sijui wa-rasilimishe hizo biashara zao si mtakuwa mnawachanganya tu! Ndio mwanzo wa kuwazamisha katika umaskini zaidi wasiotarajia.
    Hii mipango yote, sijui MKURABITA, MKUKUTA, MKUYATI nk ni mchanga wa macho tu! Wao watoe elimu na mitaji yenye riba nafuu kwa wafanyabiashara wadogowadogo watu wafanye kazi!
    Na haya mambo ya kuwakumbatia Watasha eti watusaidie kuondoa umaskini naona yamepitwa na wakati sasa. We should come up with our own solutions!

    ReplyDelete
  10. sasa jamani kama sio suluma na mazaha hawa wathungu nao fipi?Hao wazungu nao wako kwenye wanyonge?Damnnnn.Watatumaliza hawa wadudu.

    ReplyDelete
  11. Safi sana mheshimiwa unaejitambulisha kama (mimi) kwanza kwa kutupa ufafanuzi wa mkurabita na kutoa dukuduku lako kuhusu hii mambo,naridhishwa sana kuona kuna watu wenye upeo na wanakubali kuna vitu wanahitaji kujua bado,labda michuzi sasa atutafutie taarifa ya jinsi ya kutumia hizo fursa,nimesoma baadhi ya comments zako haswa ile ya the game supermarket na tamaduni zinazojengeka za wazawa kudhani kutumia bidhaa za makopo ni maendeleo,nakuunga mkono mimi,tupende vya nyumbani.

    ReplyDelete
  12. MKURABITA wanyonge wengi niliowauliza walisema wanachofahamu ni mradi wa kutambua mali za wanyonge kwa kuzisajili kama vile nyumba na mashamba ambayo hayakupimwa na kuwapa hati miliki ili waweza kuwabana wa kulipa kodi za majengo na mashamba ili wapate pesa za kuendeshea mabenzi ya Serikali.Huo ndio Mkurabita wanaoujua wananchi sasa hivi ambao hapo mwanzo walikuwa hawalipi kodi yoyote kwa ajili ya nyumba au mashamba lakini sasa wameanza kutiwa umaskini kwa kudaiwa kodi wakati mashamba na majengo hayo hayawasaidii lolote hata hawawezi kupata mikopo kwani hata wakienda kwenye mabenki hayakubali hati hizo walizopewa chini ya Mkurabita.Mkurabita umewafanya wanyonge kukamuliwa zaidi kuliko mwanzo.

    ReplyDelete
  13. Gongo mbaya sana inaweza mfanya mtu anayeinywa aonekane kwenye picha mwembamba,mrefu halafu mzee mwenye mvi nyingi.Gongo mbaya hasa inaponywewa na mtu mkubwa.Nasikia harufu ya Gongo kwenye hii Picha au Michuzi umemwagia gongo kwenye kamera yako.

    ReplyDelete
  14. Kuna wengine hata watu wa vijijini hawawajui, nilikuwa nasoma the guardian ya jana niliona kitu kimoja kikubwa sana mdau analalamika kuwa wakati akipresent pepar yake ya kitaalamu hakuna hata policy maker hata mmoja anayemsikiliza. Wakati yeye amefanya utafiti wa hali yetu na mazingira yetu ya kitanzania.

    Lakini angelikuja mzungu na malipoti yaliyofanyika OCklahoma na Qito akayaleta hawa wadau wote utakuta wamejazana wakitunga maneno magumu magumu ya Mkurunguta na mkurambita. na kukimbia kutafuta misaada kutoka kwa hao.

    Nafikiri sasa hivi nchi iliyoelimika ktk Africa na kuamua kuachana na mambo hayo ya kwanza South Africa, ya pili Botswana na sasa hivi Kenya wamebadilika. Zilizobaki bado wana matongo tongo machoni hawajaweza kuona vizuri.

    Sasa hivi wanasema bila kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo, Kufikilia kutengeneza hata zana zetu za kilimo, kutengeneza vitu vyetu vido vidogo na kuweka sheria ambazo zitalinda masoko yetu kwa vitu tunavyozalisha. Wadosi kuwakumbatia na kubatiza majina mbali mbali ya kiswahili(yanayoashiria ulaji) hakuna maendeleo kwa miaka 100 ijayo.

    Siyo kwamba tunalalamika kama aliyesema hapo mwanzo hila strategy zetu bado ziko mbali sana kulinganisha na hali harisi mpaka sasa hatujaweza kupata direction ya kujikomboa kutoka lindo la Umasikini. Wamachinga kuna siku waliulizwa je tuwape pesa? wakasema pesa siyo tatizo tatizo ni mazingira. mazingira kwanza ni kitu muhimu sana katika maendeleo kuliko kukimbilia misaada wakati hatujapanga mikakati madhubuti/hatujajenga mazingira ya kuweka hiyo misaada.

    ReplyDelete
  15. Mkutano wa kujadili mustakabali wa wanyonge unafanyia FIVE STAR hotel, Kempinski.....

    hii si sawa...

    ReplyDelete
  16. Mkurabita una maana gani wakati hati za mali za wanyonge zinazotolewa na serikali hazikubaliwi na mabenki Tanzania? Hivi hizo hati ni za nini?

    Pili mkutano huu ulikuwa ulaji tu mngewaita wanyonge waje watoe ushuhuda jinsi Mkurabita Ulivyowasaidia kama kweli mko serious.Mimi nimeomna tu Kimwana Anna MAKINDA akibwabwaja vitu anavyojua mwenyewe tena akiongea bila mpangilio! Mngewaleta wanyonge waje waongee kuhusu Mkurabita mngekoma ubishi sababu haujazaa chochote cha maana ambacho huyo mnyonge aweza akasema hiki hapa nimefaidi.

    ReplyDelete
  17. Nani anamla Anna Makinda?Mama mzuri na ametulia kwa muda mrefu bila issue

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...